hekimatele
JF-Expert Member
- May 31, 2011
- 9,889
- 2,805
Sasa, suala la supervision likoje hapa? I mean, ukishaweka mafundi na wameanza ujenzi, unasimamiaje kuhakikisha kuwa kila kitu kimeenda sawa sawa linapokuja suala la uchanganyaji?
Sijui kama haka kanakula tumilioni tungapi.... AMAFUMU ?
Nimevutiwa na hii mada sana, napenda nyumba ya ghorofa tatizo mifuko imechakaa.
Kwenye sekta ya ujenzi ,Haas ghorofa mkuu nakuaminiaga sana kwa kweli. Umatusaidia sana, na labda ndio anga zako hizi za kujidai.
Tatizo lipo ukihamia tu lile jukwaa pale juu unabadilika kabisa
Naangalia option kujaribu kujenga kighorofa kimoja japo nilale juu, fundi ameniambia nichague kati ya option mbili
Namaanisha kama nikilaza matofali floor slab ya juu itakua supported na hayo matofali bila nguzo. Kama nikiopt nguzo nitasimamisha matofali kawaida, niko tutani naombeni ushauri wataalamu ujenzi nitaanza soon ndio nafanya site clearance na kukusanya vifaa. Niko jijini
- kulaza matofali
- kutumia nguzo
Mkuu hekimatele unanihakikishia kwamba nukiwa na 100m namiliki mjengo wa namna hiyo hapo juu?Duuh
Kaka hapa kiukweli jiandae na kama 100. Ila hiyo mia unahakikisha unaenda na mafundi sawa mwanzo mwenga. Ikiwezekana kushinda site kabisa. La sivyo utalia kwa gharama.
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Mkuu hekimatele unanihakikishia kwamba nukiwa na 100m namiliki mjengo wa namna hiyo hapo juu?
Jee wewe ni engineer?
Usikonde kaka ngoja nitafute hiyo 100m kwanza.mKuu mi sio engineer ila nilishawahi kufanya kazi kwenye real estate company so naelewa hii makitu kwa kiasi kikubwa tu.
Usikonde kaka ngoja nitafute hiyo 100m kwanza.
Thanx a lot mkubwa ngoja nizidi kuzichanga nipate pa kula upepo juu.
Gharama ya vile vibao ikoje na vinalipiwa wapi na kiasi gani?Sio rahisi sana kutoa ushauri hapa kuhusu jambo hili. Kwanza huyo "fundi" unayemzungumzia ni "Architect" au "Structural Engineer" (ama ni "Mason" tu)? Hao wawili kama walihusika katika kusanifu jengo hilo basi unahitaji ushauri wao.
Uamuzi wa kutumia nguzo ama la unaweza kuwa ni structural au unaweza kuwa achitectural (or both!). Kwa hivyo, hao watu wawili ni lazima upate ushauri wao kwa sababu wao ndio wanalijua jengo lango linavyotakiwa kuwa na pia wanaijua site yako (na zaidi wanao wajibu wa kitaaluma/kitaalamu). Kama kwa sababu moja ama nyingine hukuwatumia wataalamu hawa katika kusanifu jengo lako,basi ushauri wangu ni kuwa fuata mchoro kama ulivyo (usifanye mabadiliko, unless mmoja wapo wa wataalamu hao ametizama (review) kazi yako na kukushauri/kuafiki mabadiliko hayo). Kama hata mchoro huna, basi hiyo ni "shughuli" nyingine tena!
Tukizungumzia nguzo, watu wengi wanafikiri zaidi zege na nondo! Wanasahau kuwa nguzo inaweza pia kujengwa kwa hayohayo matofali kutegemeana na aina ya mzigo au forces inayozatamiwa kukabiliana nazo na pia muonekano unaotegemewa.
Kwa ujumla uamuzi wa suala lako unahitaji kuzingatia pamoja na yafuatayo:
(a) Site - aina ya udongo na uwezo wake (bearing capacity)
(b) Aina na kiwango ya mzigo unaokusudiwa kubebwa (dead loads, live loads)
(c) Kiwango na ukuwa wa matofali unaotegemea kutumia (6", 5" etc, ya mkono/ya machine, mangapi kwa mfuko wa cement - kuna matofali unaweweza kukwaruza kwa vidole tu unaona linapukuchika!)
(d) Muonekano uanotegemewa - Wakati mwingine nguzo zinaongeza "ladha" ya jengo!
(e) Flexibility (nimeona wadau kadhaa wameligusia hili)
(f) Ukubwa/upana wa vyumba (spans) - kama ni span kubwa kuna uwezekano wa kuwa na tensile stress kubwa kwenye vertical members. Matofali hayawezi kuhimili tensile stress.
Kwa hayo machache, unaweza kuona umuhimu wa kuongea kwanza na wataalamu wako kabla hujafanya mabadiliko.
Nakutakia mafanikio mkuu.
Vibao gani mkuu? Au unazungumzia stickers? Kama ni stickers inategemea ni vya bodi ipi na gharama ya mradi pia! Kuna ma engineer, wakandarasi, na wasanifu/wakadiriaji no wote hao nadhani wanatakiwa kuweka sicker kutoka kwenye bodi zao. Kama ni vibao kwa maana ya vibao tu, hiyo ni kazi ya fundi selemala na painter ili mradi yale maandishi yakidhi viwango/ matakwa tu.Gharama ya vile vibao ikoje na vinalipiwa wapi na kiasi gani?
safi sana mkuu, napenda kujifunza practical stages za ujenzi wa ghorofa
vipi umeamua kutumia nguzo au kulaza matofali?
hivi unaweza kumimina slab ya first floor bila kumalizia ground floor kwanza? hapa nina maana first floor itakuwa imebebwa na nguzo tu so inategemea uimara wa hizo nguzo
Hii mkuu jiandae si chini ya TZS 150m kama unataka itoke kama ninavyoiona pichani hapo!Duuh
Kaka hapa kiukweli jiandae na kama 100. Ila hiyo mia unahakikisha unaenda na mafundi sawa mwanzo mwenga. Ikiwezekana kushinda site kabisa. La sivyo utalia kwa gharama.
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums