Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 19,947
- 34,433
BOMBA la Mafuta la Afrika Mashariki kutoka Kabale, Uganda mpaka Bandari ya Tanga, litafanya kazi kwa miaka 27 bila kusimama hata kama kiasi zaidi cha nishati hiyo hakitagundulika, imefahamika.
Aidha, kwa mujibu wa taarifa kwenye mtandao mmoja wa kijamii ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo aliyeko Uganda amejionea maandalizi ya uchimbaji na usafirishaji, visima vimeshachorongwa "tayari kwa uzalishaji wa mafuta ghafi" hayo.
“Makisio ni kuwepo kwa mapipa bilioni 6.5 (ardhini) na yanayoweza kuchimbwa ni mapipa bilioni mbili,” amekaririwa Prof. Muhongo katika mtandao huo.
Bomba la Kabaale-Tanga litasafirisha mapipa 200,000 kwa siku, Prof. Muhongo alikaririwa juzi.
Endapo bomba hilo litasafirisha kiasi hicho tu cha mapipa “yayoweza kuchimbwa” Uganda, matumizi hayo yatachukua siku 10,000 sawa na miaka 27 na miezi minne.
Hata hivyo, Prof. Muhongo alipozungumza jana na Nipashe kwa simu, alisema si rahisi pasiwepo na mafuta zaidi yanayoweza kuchimbwa kwa sababu kuna nchi nyingi ambazo zimeanza kuchimba mafuta miaka mingi iliyopita lakini mpaka leo bado zinachimba.
Akitolea mfano, Waziri Muhongo alisema Tanzania imekuwa ikichimba madini miaka mingi iliyopita na hadi leo madini hayo bado yanaendelea kuchimbwa na hakuna dalili ya kuonyesha yanakaribia kumalizika.
Aidha, Prof. Muhongo alisema matumizi ya bomba hilo ni endelevu kwa kuwa linaweza kutumiwa na Sudan Kusini na
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kusafirisha mafuta yanayochimbwa katika nchi hizo.
“Sisi si wa kwanza kugundua mafuta, kwanza nikuambie (kazi ya) 'exploration' (utafutaji) itaendelea na haiwezi kumalizika. Pia fahamu kuwa kuna nchi kama Sudani Kusini, Shelisheli, Kongo, tuna mafuta pale ziwa Tanganyika, hivyo wataweza kulitumia bomba hilo,” alisema.
Tanzania na Uganda zilisaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa bomba hilo Oktoba 12, mwaka jana.
Mwaka jana pia, Kenya na Uganda zilikuwa zikishauriana kuhusu mpango wa kujenga bomba hilo kutoka Hoima, magharibi mwa Uganda, hadi bandari ya Lamu katika Pwani ya Kenya.
Bomba hilo la mafuta lilikusudiwa kusafirisha mafuta ghafi kutoka eneo la Ziwa Albert nchini Uganda na kutoka eneo lenye mafuta Kenya la Lokichar.
Rais Kenyatta na Rais Museveni walikutana nchini Uganda, Agosti, mwaka jana na kuafikiana kwamba ujenzi wa bomba hilo ulifaa kuharakishwa.
Hata hivyo, Rais John Magufuli alikutana na Rais Museveni Machi, mwaka huu mjini Arusha na kukubaliana kujengwa kwa bomba hilo kutoka Kabaale mpaka Bandari ya Tanga.
Chanzo: Nipashe