Mgoyangi , humu JF ni uwanda wa penguin, lakini nashukuru kwa kuleta mada hii.
Gharama za ujenzi wa barabara hapa bongo ni balaa.
Chakula cha wazee ni tatizo kubwa sana na hata ukiwapatia wazee bado wadogo wakipata habari watakutoa upepo mpaka basi.
Kwa vile hakuna mkandarasi anapenda kupata hasara kinachotokea ni kujenga kazi hafifu na isiyo na viwango.
Tatizo la rushwa kila mtu analifumbia macho ingawaje lipo tena kwa wingi sana.
Suala lingine ni uamuzi wa serikali kufunga kiwanda cha TIPER.
Sasa hivi lami ambayo ni a by product ya fractional distillation ya crude oil inaagizwa toka nje .Kitu ambacho tungeweza kupata toka Kigamboni.
Gharama kubwa ya lami ni katika kuisafirisha , gharama ambayo isingekuwepo kama kiwanda cha TIPER kingekuwa kinafanya kazi.