Ujasiriamali mgumu jamani

Haviuziki, wateja hakuna, hujala ,famili inakusubiri home na una mkopo finca au pride
 
Umesahau moja mkuu na baba kamkimbia hapo lazima aongee peke yake kwa sauti wakati anarudi home

Unaweza kufikiri ni chizi lakini yamemfika yamemzidi
 
Acha wakusimilie tuu sio ukutwe hivyo utalia na kusaga meno
 
Hali hii ishanikuta saana,
muhimu ni kuhamisha kijiwe.
 
Halafu bank wanataka riba 25%

Finca na Pride wao hawataki maelezo wanasomba vitu vyote ndani wanapiga mnada na bado wanaendelea kudai riba hapo ndipo ninaposhindwa kuwaelewa yaani mtu anatoka kwenye uchizi anakuwa mwehu
 
Mikopo ni headache wee acha hasa usiku wa rejesho

Alfajiri mtu anakujia na kandambili zote mguu wa kulia anakuomba umkopeshe hela ya rejesho hapo usiku kucha hakulala anawaza pa kuipata maana biashara ndio hiyo imebuma mkuu mbaya sana
 
Alfajiri mtu anakujia na kandambili zote mguu wa kulia anakuomba umkopeshe hela ya rejesho hapo usiku kucha hakulala anawaza pa kuipata maana biashara ndio hiyo imebuma mkuu mbaya sana

I can feel the situation naiman64
 
Last edited by a moderator:
Umesahau moja mkuu na baba kamkimbia hapo lazima aongee peke yake kwa sauti wakati anarudi home

Bora hilo la kukimbiwa na baba, kodi ya nyumba, mwenyewe anataka kodi ya mwaka mzima kesho. Halafu mwalimu wa mwanae shuleni anamdai hela ya ubuyu wake aliolazimishwa kukopa.
 
Bora hilo la kukimbiwa na baba, kodi ya nyumba, mwenyewe anataka kodi ya mwaka mzima kesho. Halafu mwalimu wa mwanae shuleni anamdai hela ya ubuyu wake aliolazimishwa kukopa.

Mkuu acha tusiendelee umenikumbusha dada yangu aliletewa deni na mwalim shs 95,000 ya ubuyu na pipi toto linaulizwa linajibu ndio "nimekula"
 
Mkuu acha tusiendelee umenikumbusha dada yangu aliletewa deni na mwalim shs 95,000 ya ubuyu na pipi toto linaulizwa linajibu ndio "nimekula"

Heri hilo toto lililokubali kuwa lilikula,mitoto mingine inakataa na kwa kukataa huko inasababisha uhasama mkubwa kt ya mwalimu na mzazi. Pole zake.
 
Mkuu acha tusiendelee umenikumbusha dada yangu aliletewa deni na mwalim shs 95,000 ya ubuyu na pipi toto linaulizwa linajibu ndio "nimekula"

Mwalimu dhulmati huyo na hana maadili hata kidogo, huwezi kukubali mtoto awe na deni lote hilo, mtu mzima tu mwenye kazi yake bado ni kasheshe
 
mshana jr maisha ni magumu kuliko tunavyofikiria,acha mama alale akiamka aanze upya!!!
 
Kadamka huyo saa tisa za usiku kaenda kufuata bidhaa hajapata muda wa kujipumzisha kwa kweli lazima uchoke hakuna mapumziko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…