Mpwa umekuja na mada nzuri sana ila umekuja na vitisho pia! Hakuna kitu duniani kisichokuwa na changamoto... kikubwa ni kuwa committed na kufanya research ya kutosha pia kuwa na interest na hicho unachokitaka na sio kufuata mkumbo!
Kwa mfano umekaa mahali; kijiweni, Bar, Msibani, n.k kwenye story za hapa na pale unakuta watu wanasema ufugaji wa kuku unalipa sana! Unavutiwa na mada hio kwahio unachotakiwa kuangalia ni je ntaweza na sio ku conclude kuwa itanilipa!
Kama kweli imekuvutia unatakiwa kufanya yafuatayo, tulia, jipe muda wa kuwaza kwa kina na kusoma na kuuliza kwa watu ambao ni wafugaji! Wanasemaje? Kisha jihoji wewe mwenyewe.
Pili, andaa mazingira ya kuwezekana na sio ya kujaribu!
Tatu, muda ni muhimu sana kwa kila kitu! Hakikisha una dedicate muda wako mwingi kwenye hio business kuliko kwenye starehe na vitu vingine.
Nne, epuka kujipa excuse za kijinga.
Tano, Usichanganye kazi yako hio au biashara yako na undugu au urafiki uliopitiliza.
Suala la mtaji ni muhimu sana na ukiamua kufanya jambo fanya na sio kujaribu! Hapa wengi ndio tunapotea njia.
Zijue zile main challanges kabla ya kaunza na jinsi unavyoweza kuzikabili.... i am sure tutafanikiwa tukifanya sehemu yetu na Mungu akiwa upande wetu