Ujasilia mali Tanzania ni Adhabu, Benki Zatumika kutumaliza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujasilia mali Tanzania ni Adhabu, Benki Zatumika kutumaliza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mgt software, May 28, 2012.

 1. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  Katika hali isiyo ya kawaida jasilia mali Tanzania ni adhabu kubwa kwa wa Tanzania jambo ambalo ni tofati na nchi nyingine, ni jambo la kushangaza kwa nchi kama Tanzania ambayo ina zaidi ya watu millioni 40 to 45, bado hatuwezi kujitegemea, Tanzania kila siku inazalisha lundo la watu wasio kuwa na ajira, huku mradi wa MKURABITA na MKUKUTA ukiwa hauna njia dhabiti ya ksunusu Taifa ili.

  Kwanza kabisa naanza na Benki zetu hizi, kumekuwa na Utitili wa Mabenki mengi hapa nchini ambayo hayana udhibiti wowote juu ya utoaji mikopo, kuna benki nyingi za kigeni ambazo mpaka upate mkopo,kweli utasota utadhani unatayalishiwa mashitaka kufungwa. Watakuzungusha kweli kweli wakitafuta visababu vidogo vidogo ili wakukwamishe.

  Mfano : Umemaliza shule ya VETA, umejifunza ujasilia mali, malengo ya VTA ni kukufanya huweze kujitegemea, inapotokea umepata sehemu ya kufanyia kazi, hapo ndipo shughuli huanza, watadai uzoefu, Bank statement ya Miezi sita, Nyumba, Kiwanja, gari na mali isiyohamishika, mdai hayo eti yalitolewa na masharti ya Benk Kuu.
  Kumbe benki kuu inatuhujumu sisi tuliotupwa kwa kukosa ajira? kumbe ndio inawaambia watuzungushe kiasi cha kukata tamaa?
  Ukienda Benki nyingi utakuta mkopo fasta siku tatu, nenda ukaone ni miezi miwili.

  Sisi wafanyabishara wa ngazi aina yoyote tunanyanyashwa na TRA, Wenye Nyumba, Benki.

  TRA.
  Bila kujali kuwa kwa sasa biashara imeshuka sana au unaitaji kubadilisha biashara baada ya kuona haina tija, wao hendelea kukudai kodi yao waliokupangia.

  Wenye Nyumba.
  Kumekuwepo dhuluma sana na hawa watu, nyumba zimejengwa kama miaka ishirini au kumi , wao kila mwaka wanapandisha wakidai gharama zimepanda. Tena huwa wanafanya udanganyifu sana katika ulipaji kodi, ulipa w/t ndogo sana,mlango ndogo anataka millioni kwa mwezi alafu anataka kodi ya miaka miwili, ukimpa hizo hela karatasi ya
  mkataba anakuletea ya sh. laki moja na nusu kwa mwezi, pia anakuchaji hela za w/t za laki moja na nusu, kwa kuwa hakuna jinsi wewe ndio mhitaji unaacha tu serikali hiibiwe. Kwa hili wa kulaumina ni W. ya Ardhi na Nyumba kwani hawapiti kupeleleza wapangaji mbali mbali na kuweka mitego ya kuwabana.

  BENKI.
  Benki nyingi sana wamejiwekea kiwango cha juu sana kuanzia millioni 30 na kuendelea ili kukwepamlolongo au utitili wa waombaji. Kuna Benki kama Bank M, Standard Charted, stanbic UFC na nyingi za kiindi balaa tupo, ukifika utapokelewa na tusichana tumetoka shule, tunakushutua na kingereza, tiyari washakutenga hapo. kwa kukuangalia kataanza masharti magumu mpaka unageuza kisogo na kuondoka.
   
 2. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  saccos nyingi zimekufa kwa sababu nyingi zilikuwa zoa zoa, vigogo wanajichanganya na kukwapua hela zote alafu hawarudishi. Hii ilikuwa janja ya serikali kuteka vijana, kwa hivi sasa mpka ukapate mkopo utajuta.
   
Loading...