Fugwe
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 1,676
- 663
Wakazi wa chamazi na viunga vyake kwa kipindi kirefu sasa wanaishi kwa wasi wasi sana kutokana na hofu ya kuvamiwa na majambazi. Siku ya Jumapili tarehe 17/01/2016 majambazi yakiwa na siraha za moto yalivamia kituo cha kuuzia mafuta ya gari maarufu kama petrol station na kuua walinzi watatu (3) kwa kuwapiga risasi. Tukio hilo lilitokea mida ya saa 2 usiku hivi. Baada ya kuua walinzi, majambazi hayo yaliingia kwenye Mini supermarket na kukusanya fedha za mauzo kisha yakatokomea. Vilio na simanzi bado vinaendelea kutawala eneo hilo.
Tatizo ni hili ni kubwa, Mmiliki wa kituo hicho kwa jina maarufu mama mchina (Alimilikishwa kituo na mchina ambaye ni bwana wake) siku za nyuma alikuwa akifuatwa fuatwa na majambazi nyumbani kwake mpaka akahama kurudi kuishi maeneo ya Posta. Tukio hili si kwa mama mchina tu, kuna mfanyabiashara anayemiliki maduka ya hardware kwa jina bw. UWESU naye amekuwa akivamiwa mara kwa mara nyumbani kwake kitendo kilichosababisha ahame nyumbani kwake na kutafuta mazkazi mengine. Hali kama hii si njema, binadamu wamegeuka wanyama, kwani katika uvamizi huo mara nyingi pesa inayochukuliwa ni kidogo sana lakini maisha ya watu hupotea na kuleta simamanzi kwa familia.
Kuna mtandao wa ujambazi unaofanya kazi kuanzia chanika, Mvuti, Msongola, Mbande, chamazi hadi mbagala. Majambazi haya, hayajifichi utakuta kwenye baa za pombe wanatumbua maisha na jioni wapo kazini. Nyumba nyingi zimeshavamiwa watu kujeruhiwa, kuuawa na kupoteza maisha.
Kamanda Sirro, tupia jicho eneo la chamazi please, haiwezekani watu hawa washindikane, bunduki wanazotumia wanapata wapi? Makamanda wa Patrol wako wapi? Ibuniwe mikakati mingine ya kupambana na majambazi kama iliyopo imeshindwa