Babafetty
Senior Member
- Nov 11, 2013
- 107
- 108
Kwanza napenda kutoa pole kwa Jeshi la Polisi, familia na watanzania wote juu ya vifo 8 vya polisi vilivyotokea kwa ndugu zetu na walinda aman wetu, karibia na Kibiti, mkoa wa pwani.
Kwa muda wa miaka mitatu mfululizo, kumekuwa na hali ya sintofahamu kwa jeshi letu hasa kwa mkoa wa Pwani, wanashambuliwa na watu wasiofahamika tena wakiwa na mavazi ya jeshi, mbaya zaidi wakiwa wanasilaha, kuna baadhi wamekua wanapoteza maisha na wengne wanapata ulemavu wa kudumu .
Ila kinachonitia hofu zaidi ni pale nnaposikia mkoa huo huo polisi weshambuliwa tena, na kupelekea kupoteza maisha kisha washambuliaji/ majambazi/magaidi kuchukua silaha na kutokomea nazo,
Tumeona hili hata kituo cha polisi cha Stakishari, ambapo walivamia, kuua polisi na kuiba silaha na matukio meng yenya karba hiyo.
Hii kwangu ni ishara mbaya saana kwa usalama wa raia na taifa kwa ujumla, kwani kuna maswali ya kujiuliza:
* kwa nn wawalenge polisi hasa wakiwa na silaha,
*Ni akina nani na wanalengo gani zaidi la kukusanya silaha,
* Je ni majambazi kwel, ama ni kikundi cha ugaidi,
* Wanaofanya haya mauaji ni kwel Watanzania ama kuna raia wa kigeni,
Hii kwang ni red alert ili kufanikiwa ni lazima serikali na vyombo vyake vya usalama walichukulie kwa uzito wa kipekee, Watanzania kwa pamoja tutoe ushirikiano kwa mamlaka husika, tuweke itikadi zetu za kisiasa pembeni ili kukomesha matukio ya kinyama yasijirudie.
Tanzania kwanza, mengne badae...
*tafadhali ukijiona hauna cha kuchangia nyamaza, kejeli na kauli za kukela hazitakiwi hazitakiwi*
>Nini maono yako...