mechard Rwizile
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 1,571
- 873
Jan huko Devos, Switzerland; rais wa China ya Mao alitetea utandawazi wakati Waingereza na wamerakani wanatetea kulinda viwanda vyao. Wamebanwa mbavu, hawana njia nyingine ya kupumua, na kwa bahati mbaya hawataokoka.
Waingereza na Wamarekani wanadhani, kufunga milango ya uchumi wao kama walivyokuwa wamefanya China ya Mao, ndiko kutakowaokoa kumbe sio kweli.
Mambo makubwa mawili nimejifunza, ni kwa vipi kushusha thamani ya fedha yako kunaweza kuchangia kukua kwa uchumi wa nchi yako. jambo la pili; nini thamani ya kuzalisha mali kwa kutumia watu badala ya mashine.
Rais mteule wa Amerika, Mheshimiwa Ronald Trup, anailaumu China kwa kushusha thamani ya fedha zake kwa kiwango cha juu sana. Na dhana hii inasaidia kukua kwa uchumi wa China kwa sababu wanacho cha kuuza nje. Wana vitu vingi vilivyozalishwa kwa gharama ndogo dhidi ya bidhaa ya za Amerika na ulaya ambazo ni aghari sana. Mtu akiwa na $ 10 anaweza kupata vitu vingi kutoka china, ukulinganisha na vile ambavyo vimezalishwa na viwanda vya ulaya na Amerika.
Nimalizie kwa kusema sera za ujamaa zilizolenga mapinduzi ya mila za kichina zimehakisha kuwafikisha hapa walipo, kiasi kwamba sasa wanatetea ambayo yalikuwa yanafanywa na wanyonyaji wa dunia na wele waliokuwa wanayatetea sasa wanayapinga.
Unapotumia watu wako kuzalisha bidhaa, unawawezesha kuuza ujuzi, maarifa na jitihada zao nao wanapata kipato. Tabia hii ina nguvu nyingi China kwa maana watu ni wengi sana na wanashindana kila kukicha. Mashindano hayo ndiyo chachu ya kukua kwa uchumi wa nchi yao.
Trump na May wajue Amerika na Wingereza hazitakuwa zilivyokuwa hapo awali.