Say no to actors
JF-Expert Member
- Aug 9, 2016
- 637
- 641
Habari za mchana wadau,
Mimi "say no to actors" baada ya kusikiliza mjadala unaoendelea katika mitandao ya kijamii, vyombo vya habari, makanisani, misikitini pamoja na mitaani juu ya tuhuma za baadhi ya wateule wa Mheshimiwa Rais kutumia vyeti vya taaluma visivyokuwa vya kwao mmojawapo akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ndugu Paul Makonda, napendekeza uhakiki wa vyeti ufanyike kwa wateule wa huyu mheshimiwa.
Hii inatokana na serikali kupitia wizara ya elimu na wizara ya utumishi kuutangazia umma kuwa kunafanyika uhakiki wa vyeti kwa watumishi WA umma zoezi ambalo limepelekea watu kuachishwa/ kuacha kazi, kushushwa vyeo, watumishi kutolipwa stahiki zao, na hata kusitisha ajira.
Ni matumaini yangu kama mtanzania ambaye nami naguswa na hili jambo kuona haki inatendeka kwa wateule wote wa Mheshimiwa Rais kufanyiwa uhakiki na ikishabainika kuwa Kuna mtu/watu wanaotumia vyeti vya watu basi hatua Kali zichukuliwe dhidi ya:
1: mhusika anayetumia vyeti/ cheti kisichokuwa cha kwake.
2: usalama wa taifa uwajibishwe kwa kutokuwa makini katika hili mpaka kupelekea taifa kupata aibu ya kuongozwa na viongozi vilaza na wanaostahili kumtumikia kifungo magereza.
3: Mheshimiwa Rais kujitokeza hadharani kuomba wananchi msamaha kwa kuwadanganya kuwa alitumia muda WA kutosha WA kuwafuatilia watu wanaofaa kuteuliwa na mbele ya vyombo vya habari kasema amejiridhisha VYA kutosha na elimu zao na pia amekagua na vyeti.
4: Wizara zinazohusika kuhakiki vyeti zichukuliwe hatua dhidi ya ubabaishaji WA makusudi walioufanya mpaka kupelekea hawa watu ambao mbali na kuteuliwa na Rais kwa mjibu wa sheria Ni watumishi wa umma ambao tungetegemea hizi wizara ndizo ziibue madudu Haya kabla ya wananchi wa kawaida.
Pia katika kuhakiki vyeti vya hawa watu hizi wizara zisihusike na badala yake liundwe jopo la wataalam wasiofungamana na upande wowote ili tupate majibu sahii na kwa wakati. Narudia kuwa natilia shaka serikali kuhusika kwenye uhakiki huu kwani kutskuwepo na uwezekano mkubwa wa kufanya kitu "Funika kombe mwanaharamu apite".
By Kamanda wa KIRIBA kwa sasa ARUSHA kuhakikisha LISSU anakuwa Rais wa TLS.