Uislam na hekima ni vitu pacha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uislam na hekima ni vitu pacha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jobe ayoub, Oct 21, 2012.

 1. jobe ayoub

  jobe ayoub JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 206
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hakuna tukio kubwa la ushindi kwa waislamu kupita HIJRA.
  Tukio ambalo Mtume SAW alihama katika nchi ALIOZALIWA ya Makka na
  kuhamia nchi ya ugenini ya MADINA baada ya mateso mengi aliyoyapata
  kutoka kwa jamaa zake kwa kipindi kisichopungua miaka KUMI baada ya
  Mtume SAW kuanza rasmi kazi yake ya Kutangaza Uislamu.

  Jee Waislamu tunajifunza nini kutika HIJRA???
  Jee Mtume alihama kwao Makka kwasbabu alikuwa hana nguvu ya kupigana???
  Alikuwa hana Msaada wa Allah???
  Watu wa Makka walikuwa hawahitaji Uislamu???
  Jee Mtume na waislamu walikuwa waoga ndio wakakimbilia Madina???

  Basi kama hatujui,
  basi ile ndio ilikuwa ndio HEKMA kubwa kuliko zote katika safari ya Uislamu
  na kwa tukio lile ndio nyota ya ushindi kwa waislamu na Uislamu kutawala dunia ilipochomoza.
  ...
  Hakuna Uislamu bila ya HEKMA na kila mwenye Hekima basi huyo ndie Muislamu wa kweli na ndie atakaepata KHERI NYINGI.

  Na panapokosekana HIKMA basi hakuna Uislamu na matokeo yake ni KUJIANGAMIZA.

  Quraan 4:97""""
  Hakika Malaika watawaambia wale ambao wamewafisha nao WAMEJIDHULUMU NAFSI ZAO:
  Mlikuwa vipi? Watasema:
  TULIKUWA TUNAONEWA. Watawaambia:
  Kwani ardhi ya Allah haikuwa na wasaa wa KUHAMIA HUMO?
  Basi hao makaazi yao ni MOTO, nayo ni marejeo mabaya kabisa.""""""

  Imesimuliwa kutoka kwa Anas bin Malik kuwa kuna Bedui mmoja aliingia msikitini
  na kukokojoa hadharani basi Msahaba wa Mtume wakaanza kumtolea maneno na kutaka kumzuia na kumpiga.
  Lakini Mtume aliwazuia masahaba zake na kuwataka wamwachie amalize haja yake.
  Alipokwisha kukojoa Mtume alimwita yule Bedui akamwambia Huu ni MSIKITI KWA AJILI YA IBADA SIO SEHEMU YA KUKUJOLEA Kisha akawamuru masahaba zake wachukue ndoo ya maji wasafishe ili sehemu iliyokojolewa.

  Hadithii hii inapatikana katika SAHIH BUKHARI NA SAHIH MUSLIM.

  NB;imefika wakati sasa tutofautishe kati ya uislam na mvaa kanzu ya kiislam..
  vurugu za sasa ni matokea ya udini unaopandikizwa na wanasiasa ili kufikia malengo yao..
  mahakama ya kadhi kwenye ilani ya ccm,ni ya nini?kwa manufaa ya nani?
  wakati chama ni cha dini zote..
  TAFAKARI.
   
 2. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,771
  Likes Received: 6,104
  Trophy Points: 280
  Napita kwa kasi ya ajabu hapa; nawahi kule Nyasa kushusha kitu ntarudi baadaye.
   
 3. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Tatizo uislam umevamiwa na WAHUNI akina Mohamed issa,ponda,al-nuur,radio iman n.k
   
 4. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Pia uislam nadhani unakitu.
   
 5. K

  KIRUMO JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 25, 2012
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hekma ni kujua jambo la kufanya;
  Jinsi ya kulifanya;
  Wakati wa kulifanya;
  Nani wa kulifanya;
  Na mahali pa kulifanya!
  Mtu alipoingia kukojoa msikitini mtume alijua nini cha kufanya na jinsi ya kufanya na wakati wa kufanya pamoja na nani wa kufanya. Mkojo ukasafishwa na ibada ikaendelea. Bila shaka aliyekuwa anakojoa msikitini alailimishwa na hapakuwa na tafrani. Wanaojiita wanaharakati wa Kiislamu, Hekma kama ya mtume iko wapi? Nina hakika mtume hangechoma makanisa, wala hangeagiza makanisa yachomwe kwa sababu tu mtoto fulani kakojolea kitabu kitakatifu. Kama alivyojaa hekima, angetumia hekima. Hekima yenu iko wapi? Uislamu ni dini ya amani kama jina lake lilivyo. Je hayo matendo ndiyo amani? Tusiuabishe uislamu wala kuudhalilisha kwa sababu uislamu na hekma ni mapacha!
   
 6. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Uandikeni msahafu kwa kiswahili, ondokaneni na utumwa wa kuwaabudu kina "qabus"

  wakiwazuia waambieni "inawezekana hii kitu haituhusu" ni pendekezo tu jamani!!!
   
Loading...