The boy tz
Senior Member
- Sep 25, 2018
- 116
- 103
Kwa nini serikali inakubali tunaibiwa kwa kuuziwa bidhaa feki zenye viwango duni? kila mwaka unanunua kitu kile kile tunashusha thamani pesa yetu mf unanunua tv laki tatu na nusu baada ya miezi au mwaka inaharibika unarudi tena kununua nyingine wakati pesa hiyo unaweza kupata tv og na ikadumu. Pia kuna simu feki zinaaribika mic sipika betiri kuvimba enzi nokia inatamba hazikuwepo kesi kama hizi. Kuna vyombo vya muziki hapa ndipo shida zaidi unanunua vyombo vya m.100 kwaajili ya bend au kanisa kumbe amp ya yamaha uliyonunua sio yamaha kweli na watt zilizoandikwa 3000 sio ni 700 baada ya muda vinaanza kuungua drums hata uzituni siku nzima bado zitalia kama makopo. Mi nashauri serikali iruhusu bidhaa zinazokubalika kimataifa tu kuuzwa nchini kwetu na ziwe na nembo inayoonyesha kiwango cha ubora cha bidhaa unayoinunua je? ni cha kwanza cha pili au cha tatu ili mnunuaji ujue. Kama ni simu wanaweza kuruhusu kampuni kama nokia htc huawei iphone motorola hata kama zitafika kampuni 100 lakini ni zile zinazokubalika kimataifa kwa ubora na sio zile zinazoletwa kwa majaribio afrika ambazo hata kiwanda hakijulikani kilipo. Hivyo hivyo kwenye tv kwenye vyombo muziki na vifaa vingine vya kieletroniki tbs watakachofanya ni kwenda kukangua tu je hiki kifaa ni cha sony kweli kama tfda walivyokuwa wanafanya kwenye dawa, uone kama bidhaa feki hazijapotea kwenye soko kama mifuko ya pilastiki.