Uingereza Yapunguza Kodi - Tanzania Yaongeza Kodi

Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
1,649
2,911
Waziri anayeshughulika na masuala ya Fedha wa Uingereza, amewaambia wawekezaji na wafanyabiashara waliopo Uingereza kuwa serikali li kukabiliana na uwezekano wa kuanguka kwa uchumi na kuyumba kwa biashara kufuatia Uingereza kupiga kura ya kujitoa EU, watapunguza kodi kutoka 20% mpaka 13%. Hatua hiyo itafanywa ili kuvutia uwekezaji na kulinda ustawi ya biashara ndani ya Uingereza.

Source - BBC

TAFAKARI
Tanzania ili kukuza uchumi wanaongeza kodi, Uingereza ili kukuza uchumi wanapunguza kodi. Hivi kama hatuna akili za kufikiria na kutafakari, hata kutazamia tu hatuwezi?
 
TAFAKARI
Tanzania ili kukuza uchumi wanaongeza kodi, Uingereza ili kukuza uchumi wanapunguza kodi. Hivi kama hatuna akili za kufikiria na kutafakari, hata kutazamia tu hatuwezi?

Wewe ndio huna akili.Uingereza kuna wawekezaji kibao toka nchi zingine za ulaya ambao wamepania kuondoka zao baada ya uingereza kujitoa muungano wa Ulaya.Katika kuwabembeleza wasiondoke ndio inawashushia kodi.Tanzania hilo TIshio hatuna na wawekezaji wengi wanatutaka, tushushe kodi tunajikomba nini? The higher the demand the higher the price.

Si kila anachofanya mwingereza na sisi lazima tuige.Wasomi koko mna shida.
 
Tanzania si sawa na uingereza,wao wana hazina kubwa ya kiuchumi,toka enzi hizo yule mkoloni ameplunder mali toka kila pande ya dunia,amepiga hatua kubwa kiuchumi na kiteknolojia,itatuchukua muda mrefu kufanya wao wanayofanya hivi sasa. Pia kumbuka hata wao walifanya hiki tunachofanya sasa hivi katika kuongeza mapato,historia ya uchumi wake inasema yote.
 
Nani amepania kuondoka we? Mtu kawekeza london aondoke aende Austria au Hungary?
Hizo ni kelele za wanasiasa na wabunge wa EU
Kuitisha uingereza
Hapo wameshusha zaidi ili kuvutia wawekezaji wapya kutoka nje
 
Mbona husemi kilio cha watu wa uk walivyofunga mikanda miaka sita sasa na unalalamika Ugumu wa maisha tz wakati serikali inapotaka kurekebisha uchumi. Tatizo lenu mnachagua lipi tz iige na lipi isiige
 
Mkuu hujaeleweka

Miaka sits ipi unayoizungumzia uingereza kufunga mkanda au unasimuliwa

Uingereza haijawi kwenda depression kubwa yeyote baada ya london exhibition na second world war

Hizi zinazotokea ni changamoto ndogo ndogo tu kutokana na competion ya
nchi zinazochomoza kiuchumi

Kwa hiyo Tanzania imefunga mkanda nayo? Unachekesha wewe

Nchi inayodhamiria kufufua uchumi haiwezi kuwa kama Tanzania

Utafufuaje uchumi wakati unalipa watu wasiofanya kazi mfn wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa, mbio za mwenge,

Wadanganyika mnajua kijifariji
 
Waziri anayeshughulika na masuala ya Fedha wa Uingereza, amewaambia wawekezaji na wafanyabiashara waliopo Uingereza kuwa serikali li kukabiliana na uwezekano wa kuanguka kwa uchumi na kuyumba kwa biashara kufuatia Uingereza kupiga kura ya kujitoa EU, watapunguza kodi kutoka 20% mpaka 13%. Hatua hiyo itafanywa ili kuvutia uwekezaji na kulinda ustawi ya biashara ndani ya Uingereza.

Source - BBC

TAFAKARI
Tanzania ili kukuza uchumi wanaongeza kodi, Uingereza ili kukuza uchumi wanapunguza kodi. Hivi kama hatuna akili za kufikiria na kutafakari, hata kutazamia tu hatuwezi?

Uingereza pia imefuta jinsia yaani Ke na Me au Baba na Mama na kuna Wazazi tu ina maana mzazi anaweza kuwa Ke na Ke au Me na Me, Je na sisi tufute pia jinsia tulizonazo yaani tufute Baba na mama na kuweka Baba na Baba na Mama na Mama kwa kuwa Uingereza pia imefuta?
 
Wewe ndio huna akili.Uingereza kuna wawekezaji kibao toka nchi zingine za ulaya ambao wamepania kuondoka zao baada ya uingereza kujitoa muungano wa Ulaya.Katika kuwabembeleza wasiondoke ndio inawashushia kodi.Tanzania hilo TIshio hatuna na wawekezaji wengi wanatutaka, tushushe kodi tunajikomba nini? The higher the demand the higher the price.

Si kila anachofanya mwingereza na sisi lazima tuige.Wasomi koko mna shida.
Ujinga mbaya zaidi ni pale unapofikiria kuwa unakili wakati hujui. Hivi una ushahidi wowote kwamba wawekezaji wanapigania kuja kuwekeza Tanzania?Takwimu zinaonesha uwekezaji nchini Tanzania umekuwa ukishuka mwaka hadi mwaka. Wawekezaji kwenye sekta ya madini wamekuwa wakiondoka kwa kasi ya ajabu. Kama hujui nenda wizara ya madini na nishati, ukaulize. Usiwe mropokaji kwa kitu usichokijua.
 
Tanzania si sawa na uingereza,wao wana hazina kubwa ya kiuchumi,toka enzi hizo yule mkoloni ameplunder mali toka kila pande ya dunia,amepiga hatua kubwa kiuchumi na kiteknolojia,itatuchukua muda mrefu kufanya wao wanayofanya hivi sasa. Pia kumbuka hata wao walifanya hiki tunachofanya sasa hivi katika kuongeza mapato,historia ya uchumi wake inasema yote.
Dubai ilijenga uchumi wake kwa kasi ya ajabu kwa kupunguza sana kodi.
 
Our motherland Tz siyo koloni la Uingereza! hatuwezi fanya kila kitu wanachokifanya!
 
Waingereza wana mahitaji yao, na sisi tuna ya kwetu. Kuna wakati watapandisha na sisi tutashusha kufuatana na mahitaji yetu.

Kodi kwenye suala la utalii limeelezwa vizuri na Dr. Mpango. Makampuni mengi hayalipi kodi toka kwenye mapato yao.

Kuikomoa serikali wataipeleka kodi hiyo kwa watalii. Wakumbuke kwamba suala hili ni kisu chenye ncha mbili. Watalii wakigoma kuja, kweli serikali itakosa mapato na wao watakosa vile vile.

Kila mtu lazima alipe kodi.
 
Nchi kwa sasa inaongozwa kwa formulae za burnsen bunner xaxa izo sheria zenu za kiuchumi hazimuhusu mkuu
 
Mkuu hujaeleweka

Miaka sits ipi unayoizungumzia uingereza kufunga mkanda au unasimuliwa

Uingereza haijawi kwenda depression kubwa yeyote baada ya london exhibition na second world war

Hizi zinazotokea ni changamoto ndogo ndogo tu kutokana na competion ya
nchi zinazochomoza kiuchumi

Kwa hiyo Tanzania imefunga mkanda nayo? Unachekesha wewe

Nchi inayodhamiria kufufua uchumi haiwezi kuwa kama Tanzania

Utafufuaje uchumi wakati unalipa watu wasiofanya kazi mfn wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa, mbio za mwenge,

Wadanganyika mnajua kijifariji
Nasimuliwa naomba wewe uliye huko niambie hali ya maisha ikoje na vipi kuhusu mtu kulipia ile inayoitwa bedroom tax ina maana gani halafu nitakujibu vizuri
 
Wape ukweli mkuu kujiondoa tu UK uingerza imeaaza kujikomba kwa kushusha kodi hawa watu hawaelewi nn maana ya,ebu wape mfano mdogo wa mseven na mrusi,mrusi aliingia mkataba na Uganda wa mafuta lkn kabla ya akaona aongeze vipengele vya masherti magumu lkn yoeli kachana karatasi ya mkataba akampa mkorea,sasa ndo watu wajiulize kila mtu anataka faida kulingana na mfumo uliopo
 
Waziri anayeshughulika na masuala ya Fedha wa Uingereza, amewaambia wawekezaji na wafanyabiashara waliopo Uingereza kuwa serikali li kukabiliana na uwezekano wa kuanguka kwa uchumi na kuyumba kwa biashara kufuatia Uingereza kupiga kura ya kujitoa EU, watapunguza kodi kutoka 20% mpaka 13%. Hatua hiyo itafanywa ili kuvutia uwekezaji na kulinda ustawi ya biashara ndani ya Uingereza.

Source - BBC

TAFAKARI
Tanzania ili kukuza uchumi wanaongeza kodi, Uingereza ili kukuza uchumi wanapunguza kodi. Hivi kama hatuna akili za kufikiria na kutafakari, hata kutazamia tu hatuwezi?

Mkuu samahani, labda huelewi uchumi [Economics], masoko [Marketing] , na ushirikiano wa kikanda [Regional Integration ] ndiyo maana unaandika na kunukuu BBC bila uchambuzi wa kina, ama hutaki kutumia vizuri ufahamu wako wa mambo kama umesoma

Kwanza, UK imejitoa EU wewe unafikili itafanya nini zaidi ya kuwadanganya wazungu wenzao ili warudishe imani na serikali pamoja na kuleta watu wengi kununua toka uingereza? ni kutengeneza soko la nje na la ndani maana katika regional integration kuna marketing theory na economic theory ambazo zinamlinda aliye ndani ya jumuiya

Kwa mfano. uwe na nchi A, B, C kama mchele katika nchi A, ni 1000/kg basi nchi B atanunua toka A endapo nchi B bei yake ni 1500/kg ila siku nchi B ikaaingia katika jumuiya ambayo nchi C ni mwananchama na anauza mchele kwa 1600/kg basi nchi B atalazimika kununua kutoka katika nchi C hata kama ni kwa bei kubwa

Maana nchi B na C zitatumia principal za Trade Creation and Trade Diversion ili kuua soko la nchi A katika jumuiya yao ambayo sasa A siyo mwananchama. Maana wataweka vikwazo vingi vya kuzui nchi A kuuza nchi zote wanachama yaani B na C, kwa economic theory yaitwa Customs Union.

Na hapo bado kunakuwa na kitu kinaitwa Trade Deflection [ni kama udanganyifu katika jumuiya, yaani mwananchama anaweza akanunua kitu nje ya jumia kwa bei ndogo na kuuza katika jumuia kwa bei kubwa] ila bado kinazuiliwa na principal yaitwa 'rules of origin'' ambacho ni kusimamia bidhaa zinazouzwa katika jumuia kuelewa bidhaa hiyo imetoka nchi ipi, ili kuzuia nchi mojawapo kununua toka nchi A na kuuza kwa bei ya juu ndani ya jumuiya ya B na C.

Sasa hapo nchi A italazimika kufanya mbwembwe nyingi sana kama vile, kuondoa mashariti kwa wawekezaji, kuondoa kodi ili kupata soko na wateja, kwa hiyo sasa hivi pale EU , UK ni sawa na nchi A , ila B na C ni zile nchi 27 zilizobakia EU [katika huo umoja wa Ulaya]

Pili, Tanzania siyo UK kwamba kila wanachofanya nasi tufanye sawasawa na wao. [UK is not our Bench mark and role model for Tanzania''s progress and economic development]

Tatu rejea Tamko la Prof. Maghebe pale Arusha alilitoa juzi kuhusu kodi za watalii hapahapa Afrika hata usiende mbali alisema Tz siyo koloni la Kenya kufanya kama Kenya wanavyofanya kuhusu kodi zao kuwa chini.

Pia, kwa kukusaidia zaidi, elewa kuwa kinacholeta maendeleo ni sera na siyo kodi hiyo pekee, unaweza ukaweka kodi kubwa na sera nzuri bado ukaendelea au kodi kidogo bila sera nzuri bado ukashindwa kuendelea au kupata wateja wengi wa kulipa hata hiyo kodi kidogo.

Kwa hiyo usichukulie tu hiyo taarifa ya BBC kama ndiyo kila kitu, pia kumbuka katika media hasa Europe, USA wanatumia propaganda kubwa sana kuleta taarifa katika jamii kupitia vyombo vya habari ila wakificha ukweli wa jambo lenyewe.

Kwa mfano, Tz tunahitaji sera nzuri na mazingira mazuri na hata kama kodi ni kubwa bado tutapaa sana kiuchumi.

Ninaongea na kuandika kwa fact maana nimesoma marketing na na regional integration na ninaelewa vizuri sana tena sana kile UK wanachokifanya katika wakati huu ambao kwao siyo rahisi kuuvuka bila kuwadanganya wananchi wao na wazungu wa nje pia.

Asante kwa kuelewa. hasa soma pale penye rangi ya blue, nyekundu na kijani utaelewa japo ukitaka zaidi nitafute nikufafanulie zaidi ndiyo utaelewa vizuri ambacho UK anakifanya na anavyokuwa na wakati mgumu kujimudu pale Europe.

Asante.
 
Sasa boss mtoa mada kwanini usiende kuhamia Uingereza na wewe ukapata kufaidika na hilo salo.
 
Our motherland Tz siyo koloni la Uingereza! hatuwezi fanya kila kitu wanachokifanya!
Umesema vyema
Tena muongezee na Taarifa ya Prof. Magebhe ,waziri , kuhusu kodi ya watalii alisema juzi pale Arusha '' namnukuu '' Tanzania siyo koloni la Kenya, kenya ni kenya na sisi ni Tanzania''

Pia, mwambie mleta uzi kuwa siyo kila jambo la Ulaya - UK/USA ndiyo kipimo cha maisha na kwa kufanya hivyo ndiyo maana tunapotezwa sana.
 
Back
Top Bottom