Dah! Sio siri, niliisahau kabisa hii forum baada ya kuzani uchaguzi mkuu umeshaisha!!!! Anyway, bado nina kumbukumbu kwamba humu jamvini watu hatuna uvumilivu wa kuona maoni yanayotofautiana na yale tunayoyaamini! Wataalamu wanasema kwamba pasipo na tofauti ya mawazo basi hapana elimu!!! Napenda kuwapa changamoto ndugu zangu wa CHADEMA ambao kimsingi hadi leo hii hawajakubali kwamba wamekuwa defeated kwenye general election iliyopita!! nina hofu kwamba, kadri watakavyoendelea kutoamini kwamba walishindwa ndivyo watakavyochelewa kufanya upembuzi yakinifu wa kwanini walishindwa!!! Na kwavile watachelewa kufanya tathimini ya kwanini walishindwa basi kuna hatari ya kushindwa tena kwenye chaguzi zitakazofuata!! Mtu akipimwa HIV na kukutwa na virusi, kinachofuata ni ushauri unasaa. Msingi wa kwanza wa ushauri nasaa ni kumfanya muathirika kukubali matokeo. Yule anayekubali matokeo mapema ndie anayekuwa katika nafasi mzuri zaidi ya kuishi kwa usalama kuliko yule anayechelewa kuyakubali matokeo!! CHADEMA bado hawataki kukubali!!
Changamoto ya kwanza ni lazima tujiulize ni kwanini CHADEMA ina nguvu kwenye maeneo ambayo wanatoka viongozi wa juu wa chama peke yake! mathalani, CHADEMA ina nguvu Kilimanjaro, ambako ndiko nyumbani kwa muasisi na mwenyekiti wa sasa! Aidha wana nguvu Arusha, ambako ndiko nyumbani kwa Katibu Mkuu! Ukiacha Arusha, CHADEMA wana nguvu Kigoma ambako ndiko katibu mkuu wa zamani Dr. Amani Warid Kaborou na naibu wa sasa Zitto Kabwe wanatoka! Vilevile CHADEMA ina nguvu Mara. Nazani vuguvugu la mageuzi lilishika kasi mara tangu zamani kv mmoja wa waasisi wa mageuzi nchini Dr. Mabere marando katokea kule. Hata NCCR ilipokosa mwelekeo, tayari wananchi walishavutiwa na mageuzi. Aidha, Mara huko huko ndiko nyumbani kwa makamu mwenyekiti hayati Chacha Wangwe!!!
Zipo sehemu ambazo hazitabiriki kama vile Mbeya, Mwanza na Iringa ambako uchaguzi uliopita CHADEMA walipata viti!! Sitaki kuamini kwamba mikoa hiyo nayo inafanana na mikoa niliyoitaja kabla.
Kutokana na hilo, CHADEMA wanajifunza nini? Kwanini chama kinachodai kina nguvu kina nguvu sehemu ambazo wanatoka viongozi peke yake!!! kwa mara ya kwanza, Singida wameichagua CHADEMA, bila shaka kutokana na kugombea Tindu Lissu ambae nae ni kiongozi wa juu wa CHADEMA! Je, kwa staili hii ya ujenzi wa chama tutarajie CHADEMA kufanya yale ambayo wana mageuzi wanayataka? Je, CHADEMA iunde nafasi nyingi zaidi za uongozi wa juu zitakazosambazwa mikoa mingine ili nako iwe na mashiko?