Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,700
- 1,853
Uhusiano wa Iran na Tanzania ya kisasa ni wa miaka arobaini hivi, tangu kufanikiwa kwa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran mwaka 1979.
Lakini Waajemi walikuwa wanakuja pwani zetu tangu miaka elfu nyingi. Ni vizuri kuona Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Iran, Abdullahian, akizuru Tanzania hivi sasa.
Hii inaonesha uwelewa mpya wa diplomasia, hasa ukijua kwamba mataifa kama Marekani, Israel, Saudi Arabia nk watachukia ukaribu huu, na huenda wakatishia!
Imenipa moyo zaidi kuwa ziara hii ilikuwa kwa mwaliko wa Tanzania.
Tangu mapinduzi ya 1979, Iran ilipenda sana kujikurubisha na Tanzania, na hata ikatoa ofa ya kujenga mtambo wa kusafisha mafuta bure bila malipo katika miaka ya 80, lakini pendekezo hilo likatupwa chini kwa 'kuwahofia wakubwa'.
Imagine! Kama tungekuwa na mtambo huo hivi sasa pengine bei ya mafuta ingekuwa Shs. 1,700 kwa lita, si zaidi.
Iran pia ilikuwa inaendeleza bonde la Rufiki na ilijitolea vifaa vingi vya kilimo, yakiwemo matrekta, Mabuldoza, Malori......vyote hivyo aidha bure au kwa bei ndogo sana! Lakini hii pia iliminywa na wakubwa!
Matokeo yake Iran ikatoa fursa hizo kwa Senegal, Congo Brazzaville, Cote D'ivoire..... kiasi kwamba Senegal hivi sasa ina assembly aina tatu za magari ya Iran na pia hatua ziko mbali za kutengeneza hata drones!
Kenya, wajanja wake wameweza kuizunguka Marekani na inapata misaada mingi ya Iran hadi mahospitali, ingawaje ina uhusiano madhubuti zaidi na Marekani kuliko Tanzania.
Sijui kwa nini tunakuwa 'clueless' namna hii! Hivi Marekani itaiomba ruhusa Tanzania ya kufanya urafiki na nchi ambayo Tanzania haiipendi?
Hadi Mandela anatoka jela, Marekani ilikuwa inapinga kabisa kuwawekea vikwazo Makaburu.
Zaidi ya hayo, ilimweka Mandela katika orodha ya 'magaidi' hata baada ya kuachiwa, kwa vile tu mfumo wa Afrika Kusini ulikuwa wa Wazungu. Ni vizuri hivi sasa tukasaka maslahi yetu tu bila kujali 'wakubwa' wowote.
Katika mambo machache niliyompendea hayati Magufuli mojawapo ni lile la kusema: ' jamani, siye Watanzania hatuna wajomba huko nje'!
Kweli kabisa.