Uhuru wa vyuo vikuu tanzania upo msalabani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhuru wa vyuo vikuu tanzania upo msalabani

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mwankuga, Jan 14, 2011.

 1. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Kwa muda mrefu sana kumeekuwa na mijadala hapa JF kuhusu ubora wa elimu vyuo vyetu vikuu.Wengine wamefika mbali sana na kudhani kuwa vyuo vingine ni bora kuliko vingine.Mjadala mkubwa ni kuhusu Chuo Kikuu cha Dodoma,huku wengi wakikiita kuwa ni chuo cha kata au chuo cha CCM.Kabla ya yote niseme mimi ni miongoni mwa watu waliosoma UDSM.Siafiki kwa UDOM kuitwa chuo cha kata au cha CCM.UDOM ni chuo kama vyuo vingine,japo kimsingi tunakubaliana kuwa uanzishwaji wa chuo hicho una kasoro kadhaa ikiwemo mihemiko ya kisiasa kuchukua mkondo.Wanasiasa hasa wa CCM wanakichukulia UDOM kama karata ya kuombea kura.

  Pia nimekuwa nikishangaa (pengine kwa sababu sijui) kuanzishwa kwa baadhi ya course au degree ambazo zina mwerekeo wa masharti kwa wahisani(wanyonyaji),kama vile degree ya kichina and the like ambazo hazina mchango wa moja kwa moja kwa maisha ya mtanzania.Sijui mwelekeo ni kuwa na wahitimu wengi wa degree au ni nini hasa?

  Kwa utangulizi huo,niseme tu utandawazi kama (sio uwizi) umetufikisha sehemu ambayo kutoka itakuwa ngumu.Tangu tuanze kutekeleza sera za soko huria hasa kipindi cha Mwinyi mambo yamebadilika sana.Serikali nyingi za Afrika zinatekeleza sera za Washington na London zinazosimamiwa na IMF NA WB bila kuangalia hali halisi.

  Lengo kuu la kuanzisha vyuo vikuu kama vile UDSM ENZI ZILE ILIKUWA NI KULETA UKOMBOZI kwa maisha ya watanzania.Kwamba wanafunzi wanapomaliza chuo wakiwa na maarifa ya kutosha wasaidie kuijenga nchi yao.Lengo la vyuo vikuu si tu kuwafanya wanaohitimu shahada zao wapate ajira bali watusaidie kujua chanzo cha matatizo yetu na jinsi ya kutatua matatizo hayo.Kwa maana hiyo wahitimu au wanafunzi wafanye tafiti ambazo matokeo yake yatatue matatizo yetu.

  UDSM enzi hizo kilikuwa chuo kinachoheshimika sana,kwa sababu wanafunzi na walimu walishiriki moja kwa moja katika harakati za maisha ya mtanzania.Walishiriki ukombozi wa nchi nyingi za kusini,wanafunzi wa kutoka nchi zingine walikuwa wengi wakifuata msingi mzuri wa chuo hicho.Inasemekana Mwalimu Nyerere alikuwa anawakaribisha wageni wengi UDSM hasa aliokuwa anatofautiana nao kiitikadi,akijua wazi wanafunzi watafanya kazi kwa niaba yake.

  Kwa mfano,mwaka 1978 wanafunzi wa UDSM walifanya maandamano makubwa wakipita maeneo ya Manzese wakiungwa mkono na wananchi wa kawaida,wakipinga wabunge kujiongezea mishahara huku wananchi wakifunga mikanda kwa maisha magumu.Mijadala mizito na yenye masirahi kwa umma ikifanyika bila woga.Walimu wakifanya tafiti zenye kugusa masilahi ya umma pasipo kutegemea ufadhili kutoka makampuni ya kibwenyenye.

  Hali sasa imekuwa tofauti sana,msukumo wa sera za soko huria umeua uhuru wa vyo vyetu.Leo tunakitu kinaitwa Bodi ya Mikopo(ambayo sio sera yetu) imevuruga kabisa utaratibu wa elimu.Bodi imewafanya wanafunzi kuhangaikia mikopo zaidi kuliko masomo.Bodi imewafanya wanafuzi kuwa wabinafsi na kuona kama serikali imewatenga.

  Mkazo wa elimu za vyuo vyetu ni kutoa wahitimu wengi kwa njia zozote,uzalishaji wa maarifa umebinafsishwa na matunda ya maarifa yamekuwa bidhaa.Vyuo vikuu vinazalisha wafanyakazi badala ya wasomi.Vyuo vinazalisha wafanyabiashara ndogondogo na makalani katika kampuni za kibepari.Mifumo ya ufundishaji imelenga kwenye kufaulu mitihan badala ya mwanafunzi kupata maarifa.Elimu tumeibinafsisha,serikali haina habari na ubora wa elimu.

  Kwa mfano,wakati wanafunzi wa UDSM wanapata shida ya kupata sehemu za kulala,menejimenti ya chuo hicho imeruhusu makabulu kujenga supermarkets au shoprites kama za Mlimani City.Mpango sio wanafunzi kupata elimu katika mazingira ya utulivu bali watawala wetu kupata utajiri.

  Watawala wetu wanaogopa sana mabadiliko,ndio maana wanahakikisha menejimenti za vyuo vyetu zinakaliwa na watu ambao ni rahisi kuwaendesha.Safu za Uongozi zinakaliwa na maswahiba wa watawala ili kuzuia harakati katika vyuo.Mfano mzuri ni Mukandala wa UDSM na Mlacha wa UDOM.Leo hii,tunasema ni maarufuku kwa wanafunzi kujihusisha na siasa katika vyuo,zote hizo ni njama za kuua fikra pevu katika vyuo na kuwafanya wanachuo wawe kama wanafunzi wa sekondari,wawe watiifu hata kwa mambo ambayo hayana maana.Vyuo vimegawanywa,wanafunzi wamegawanyika,wengi wanajali kumaliza masomo yao kuliko kipata maarifa.Hapa ndipo tulipofikia.

  Nihitimishe kwa kunukuu maneno ya Mwalimu Nyerere aliyoyatoa katika chuo kikuu cha Liberia,tarehe 29/2/1969.
  "Afrika inahitaji ukweli kutoka katika vyuo vyake vikuu.Tunapambana na matatizo mapya,na tunahitaji ujuzi wote unaoweza kupatikana katika kuyatatua.Lakini vilevile vyuo vikuu lazima viwe vyombo vilivyojitoa kutumikia taifa;vijitoe katika kutafuta maendeleo ya nchi zetu.Lazima vitoe huduma ya kizalendo,na kwa sababu hiyo itakuwa huduma ya kizalendo,na kwa sababu hiyo itakuwa huduma ya kweli na ya moyo".

  Naomba nihitimishe kwa kuwakaribisha wadau kuchangia mada hii,ili tuangalie ubora wa elimu inayotolewa katika vyuo vyetu vikuu na kulinganisha na hali halisi ya maisha ya watanzania.Naomba tutulize munkali,tuchangie bila jaziba.Nomba kuwasilisha.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Much of what is hapenning in our universities and the products is lack of seriousness in everything we do, attributed by colonised minds!
   
 3. m

  mwandishe Member

  #3
  Jan 16, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  :A S 27: Ahsante sana Mwankuga kwa message yako nzuri na yenye manufaa kwa taifa endapo kila mdau atachukua nafasi kuifanyia kazi.. Ninachopenda kuwasihi wanafunzi wa vyuo vikuu popote pale walipo plz watambue kwamba wao ni kiungo muhimu kwa maendeleo ya taifa hili no matter what & no matter how
  They have to know kwamba wao ndio wenye nguvu kubwa kufanya mabadiliko yatakayoleta tija kwa maendeleo ya taifa hili....My message to you all guyz ni kwamba"Tumepewa dhamana ya kuleta mabadiliko yote yanayohitajika na serikali iliyopo madarakani inalitambua hilo plz asiogopwe mtu wala cheo let us be a front line na wananchi wengine watatuunga mkono" OVER!
   
 4. m

  mwandishe Member

  #4
  Jan 16, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  :A S 27: Ahsante sana Mwankuga kwa message yako nzuri na yenye manufaa kwa taifa endapo kila mdau atachukua nafasi kuifanyia kazi.. Ninachopenda kuwasihi wanafunzi wa vyuo vikuu popote pale walipo plz watambue kwamba wao ni kiungo muhimu kwa maendeleo ya taifa hili no matter what & no matter how
  They have to know kwamba wao ndio wenye nguvu kubwa kufanya mabadiliko yatakayoleta tija kwa maendeleo ya taifa hili....My message to you all guyz ni kwamba"Tumepewa dhamana ya kuleta mabadiliko yote yanayohitajika na serikali iliyopo madarakani inalitambua hilo plz asiogopwe mtu wala cheo let us be a front line na wananchi wengine watatuunga mkono" OVER
   
Loading...