Uhuru wa Mahakama: Uteuzi wa Jaji Mkuu

Mto_Ngono

Mto_Ngono

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
688
1,000
Uhuru wa mahakama zaidi unatakiwa kuonekana katika maamuzi. Ila mtu mmoja anaweza akawa na nguvu kuharibu au kubadilisha maamuzi husika hasa anapopewa maelekezo kutoka kwa aliyemchagua au kwa matakwa yake mwenye kutokana na uwezo alionao.

Mahakama naingalia katika pande mbili moja ni upande wa maamuzi (majaji na mahakama), pili ni upande wa utawala ambapo pande zote mbili zinapokea maelekezo au maagizo kutoka kwa Jaji Mkuu. Maswali ya kujiuliza tu ni Je Jaji Mkuu hawezi kuathiri kwa mamlaka aliyonayo, maamuzi ya watoa haki chini yake? Je Jaji Mkuu hawezi kupata maelekezo kutoka kwa aliyemteua na kuyatekeleza na wenda utekelezaji wake unashinikiza watoa haki kufanya maamuzi tofauti!! Nadhani tumekuwa tukiona maamuzi mengi ya mahakama yakiingiliwa na muhimili mwingine wa nchi hasa Executive. Na mwisho ni Je mteuliwa anaweza kukataa kutekeleza maelekezo au maagizo yaliyotoka kwa mamlaka ya uteuzi.

Pamoja na jitihada nyingi ambazo zinalenga kuonesha kwamba maamuzi ya mahakama ni huru bado ipo haja ya kuangalia namna bora ya kuepuka ili mamlaka ya uteuzi isiwe kama ilivyo katika katiba ya Tanzania sasa. Jitihada hizo ni uwepo wa sheria na kanuni zinazoongoza utendaji na miiko ya watoa haki japo hizi zenyewe hazitoshi bila kupatikana kwa uhuru wa mamlaka ya juu katika muhimili huu i.e Jaji Mkuu anatakiwa kuwa huru kabisa bila influence kutoka katika muhimili mwingine wowote au mamlaka nyingine zozote. Anaweza akateuliwa na Rais lakini mchakato wa kumpata hampi nafasi Rais ya kutoa maelekezo/maagizo yoyote kwa Jaji Mkuu ambayo yanahitaji utekelezaji wa lazima na zaidi haumpi nafasi ya kumtoa kwa namna yoyote (security of tenure). Hivyo, ili kubadili mfumo huu wa uteuzi ni lazima kubadili/kufanya maboresho katika katiba hususani ibara inayozungumzia uteuzi wa Jaji Mkuu [Ibara ya 118(2)].

Yawezekana mifano michache hapa chini inaweza kusaidia kuonesha namna wenzetu katika nchi nyingine wanavyofanya kwenye uteuzi.

USA

Sio Katiba wala Sheria ya Mahakama (Judicial Act) inayoeleza moja kwa moja uteuzi wa Jaji Mkuu bali Katiba imempa mamlaka Rais kuteua majaji wa Mahakama ya juu ndani ya USA (tafsiri ya majaji inamjumuisha na Jaji Mkuu). Rais pia hana mamlaka ya moja kwa moja ya uteuzi huu, Katiba inamtaka kupendekeza jina na kulipeleka katika Senate, endapo Senate italikubali hapo ndipo Rais atamteua mhusika aliyempendekeza. Hivyo, maamuzi makubwa yapo kwa Senate kukubali au kukataa pendekezo (maamuzi ya wengi). Article II Section 2 Clause 2 ya Katiba

UK

Jaji Mkuu huchaguliwa na jopo la uchaguzi (Selection Panel) ambayo inaundwa na Tume ya Mahakama. See Constitution Reform Act

Kenya

Jaji Mkuu anapendekezwa na Tume ya Mahakama na kupitishwa na National Assembly then Rais anamteua. Hivyo, Rais kama muhuri hawezi kukataa kuteua baada ya aliyependekezwa kupitishwa na National assembly. See Article 166 (1) ya Katiba

Uganda

Jaji Mkuu, Jaji Mkuu Msaidizi, Jaji Kiongozi na majaji wa Mahakama ya juu, wanapendekezwa na Tume ya Mahakama na kupitishwa na Bunge then Rais anateua. Hivyo, Bunge lina nguvu ya kukataa au kukubali. See Article 142 ya Katiba.

Tanzania

See Article 118 (2). Jaji Mkuu anateuliwa na Rais. Katiba ina ukimya juu ya mchakato wa upatikanaji wake tofauti na vigezo. Haihitaji maamuzi ya wengi.

Mwisho, huu ni mtazamo tu wa namna ya kuupata uhuru wa mahakama kutokea kwenye shina. Yawezekana ukawa na mtazamo tofauti ambao si mbaya ku-share.
 
Barbarosa

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
21,073
2,000

Lakini Kenya bado walisema Jaji Mkuu wao aliiiba uchaguzi, Uingereza kitu ambacho haufahamu kila kitu liko chini ya Monarchy, huo Ufalme ndiyo Alfa na Omega na hauchaguliwi na mtu yoyote yule, mengine yote usanii tu na danganya toto!!
 
Mto_Ngono

Mto_Ngono

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
688
1,000
UK soma hiyo Constitution Reform Act inaweza pia kukusaidia namna ya CJ anavyopatikana.
 
Top Bottom