Uhuru wa kutafuta habari ni jukumu la Wananchi na si Wabunge

Tulime

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
248
104
Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatambua vyema sema uhuru na haki wa kila Mtanzania kutafuta na kupata habari.

Ibara ya 18.

Ibara ndogo ya (1),
Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.\n\n

Ibara ndogo ya (2),
Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.

Katika ibara hizo hapo juu hakuna hata sehemu moja inayosema habari tutakazopata lazima ziwe za moja kwa moja.
Ila katiba inasema tutazipata na tuna haki ya kuzitafuta, nawakumbusha waheshimiwa wabunge wafanye majukumu yao ya kuisimamia serikali na sisi wananchi tutafuatilia kwa ukaribu ni jinsi gani gani wameisimamia, wametunga sheria na kutuwakilisha.

Wabunge mmesahau kazi yenu na mnaingilia yale ambayo hatukuwatuma, mmeshindwa kusimamia serikali katika haya,

Sasa hivi.. kwa mujibu wa taarifa ya CAG ya mwaka 2014/2015, deni la taifa linakua kwa trilioni 7 kila mwaka na sasa Deni la taifa hadi juni 2015 limefikia trilioni 33.5... Wabunge wetu mnapaswa mtoe mawazo mbadala ya kuzuia ukuaji wa deni na siyo kutaka live coverage.


CAG anasema Manunuzi ya bilioni 27 yalifanywa na mashirika ya Umma bila ushindani., hivyo sheria ya manunuzi ya umma (public procurement act) imevunjwa...Wananchi tunataka tukitafuta habari tujue ni jinsi gani mmeisimamia sheria mlioitunga wenyewe na siyo tuwaone live mnauza sura bila kufanya kazi tuliowatuma.


CAG anasema Sh milioni 827 za vifaa vya upigaji kura zilitumika kwa kazi isiyo na tija.. anaendelea kusema, nakala 158,003 hazikusambazwa kwa walengwa wakati wa kura za maoni... tunapaswa kujua wajibu wenu unafanyika na sio kulia na live coverage ambazo sisi wananchi wa kawaida hazitusaidii.


CAG anasena, Milioni 700 za makato ya watumishi kwa katavi na kilimanjaro hayakuwasilishwa kwenye mifuko.. Tunataka kujua ni kamati ipi inahusika hapo ya bunge na kwann haikuisimamia vyema serikali na sio live coverage.


CAG anasema, Mishahara hewa katika taasisi 16 ni bilioni 390 na Mishahara ambayo haikulipwa na haikurejeshwa hazina ni bilioni 2.. Tukitafuta habari tupate majibu ya namna gani bunge linafanya na sio kususia na kuendelea kula posho na kodi zetu bure.


CAG anasema, halmashauri 40 pekee ndiyo zenye hati safi kati ya halmashauri zaidi ya 160 zilizokaguliwa..

Wito wangu nawaomba wabunge wafanye majukumu yao,na sisi wananchi tuna uhuru wa kutafuta habari tutazipata habari...
 
1. Wabunge ni wananchi & 2. Wabunge ni wawakilishi wa wananchi na wanahusika na sera za nchi pamoja na kuisimamia serikali.
 
Back
Top Bottom