Ushuhuda wa Injili
JF-Expert Member
- Nov 12, 2012
- 427
- 160
Wiki iliyopita kabla ya jana, yaani tar 8-11 mwezi huu 5 waumini wa Kikristo walikuwa na mkutano wa Injili katika viwanja vya kanisa la Africa Inland Church Kigamboni, nyuma tu ya Kituo cha Polisi Kigamboni. Waumini hawa walikutanika katika mkutano ule baada ya kupewa kibali na Manispaa kwa kufuata taratibu zote za kiserikali. Pamoja na kupewa kibali cha kufanya mkutano huo wa Injili, waumini hao walikatazwa kutangaza mkutano wao kwenye mitaa mbali mbali ya Kigamboni kwa kutumia gari la matangazo, na badala yake waliruhusiwa kutangaza mkutano huo kwa njia nyingine. Waumini hao walitangaza kupitia kituo cha redio cha Wapo na kutumia vipeperushi.
Siku ya tar 8 Mkutano ulifanyika vizuri pasipo matatizo, lakini ghafla siku ya tar 9 jioni waliletewa katazo la kutoendelea na mkutano huo na Mkuu wa kituo cha Polisi Kigamboni kwa madai kuwa wamepewa maelekezo toka kwa wakubwa Serikalini.
Mhubiri mwenyeji wa mkutano Mwinjilisti Yohana Marko pamoja na Mhubiri mgeni Mch. Jarvas toka Kenya waliamua kwenda katika kituo hicho cha polisi na kuuliza kwa nn wapewe katazo la kuhubiri injili wakati walifuata taratibu zote na kukubaliwa na Manispaa?
Viongozi wa kituo kile cha polisi walibaki kutoa majibu mepesi kwamba wamepewa amri toka juu.
Waziri Mkuu katika kutoa angalizo la vurugu za kidini alipiga marufuku kufanyika kwa mihadhara ya kidini (Sio Mikutano), ambapo kimsingi mihadhara huwa ni majibizano ya kidini kati ya dini mbili au zaidi tofauti. Dini za Kikristo na Kiislamu zimeongoza kwa kuwa na mihadhara yao ya kidini.
Mwinjilisti Yohana akiongea na Ushuhuda wa Injili anasema "Tuliwaambia viongozi wa polisi kilichokatazwa na Waziri Mkuu ni Mihadhara ya kidini na SIO mikutano ya kidini. Na tuliwaambia kama mnataka vurugu za kidini zitokee turudi kwenye mkutano tuwatangazie watu kuwa polisi wamekataza tusiendelee na mkutano, muone vurugu zitakazotokea" .
"Walivyoona ujasiri wetu wakabaki kutuambia tuendelee na mkutano lakini tusitumie sauti kubwa" anasema Mwinjilisti Yohana.
Mchungaji wa Kanisa hilo la AICT Kigamboni alipoulizwa kwanini walikatazwa kuendelea na Mkutano alisema hajui hasa kwanini pamoja na kuwa walifuata taratibu zote.
"Nadhani adui alitaka kuvuruga mkutano wetu. Sikuwepo wakati katazo hilo linakuja, lakini nawashukuru sana waumini ambao ni viongozi Serikalini walioingilia kati suala hili nadhani bila Mungu kuwatumia wao tungepata shida kidogo" alisema Mch. Emmanuel Mchembe.
Waumini hao waliendelea na Mkutano wao wa nje na tar 12.05.2013 waliendelea na semina ya neno la Mungu kwa siku 7 mfululizo hadi tar 19.05.2013.
Kuna taarifa za kamata kamata za watumishi wa Mungu wiki iliyopita ambao wamekutwa wakihubiri injili maeneo mbali mbali nchini. Mikutano ya injili ni njia muhimu sana katika uenezaji wa injili mahala popote duniani. Kama ilivyo katika siasa, dini navyo ni hivyo hivyo.
Kwa namna ambavyo Serikali imekuwa ikijaribu kuminya vyama vya siasa kufanya mikutano yao, je na sasa Serikali imehamia kwenye dini? Je huu si upokwaji wa uhuru wa kuabudu kwa dini?
Zaidi --> http://ushuhuda.blogspot.com/2013/05/uhuru-wa-kuabudu-umepokwa-na-serikali.html