Uhuru pasipo ukombozi ni sawa na kujilisha upepo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhuru pasipo ukombozi ni sawa na kujilisha upepo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Vox Populi, Mar 20, 2012.

 1. Vox Populi

  Vox Populi Member

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3

  Siri ya furaha ni kuwa na ukombozi na siri yaukombozi ni ushupavu. Hakuna ukombozi unaopatikana kwa gharama rahisi. Uhuruunawezekana lakini ukombozi unapiganiwa. Naweza kusema kwamba uhuru ni hatua tu kuelekeakwenye ukombozi. Ni kasumba ya wapigania uhuru kujiona siku zotekwamba wao ndio wanaofaa ama lau kujisikia kwamba wao ndio msingi wa kusimamakwa taifa. Na wa ndio hujisikia kwamba wao na vizazi vyao na ama jamaa zao ndiowanahaki ya kuendelea kuliongoza taifa. Hao wanaojiita wapignia uhuru siku zote huaminikwamba nje yao hakuna awezaye kuongoza nchi. Wengi wao huendelea kupandikizavibaraka au vipandikizi vinavyojengwa kwa lengo la kuendelea kulinda maslahiyao. Si jambo la kushangaza kuona kwamba wengi waviongozi wa taifa au nchi ambayo haijakombolewa hutaka kuona kwamba wanalindamaslahi. Naam nasema maslahi. Utawasikia mwenzetu huyuuu! Naam, mwenzao huyookwasababu huiba pamoja, hukaa katika vijiwe vya wasioridhika, miguu yaohukibilia katika kumwaga damu ya wasio na hatia, hunyonya mali za wanyonge nakuwaacha hohehahe. Hawa ndio wale wanyonyao maiti damu. Huja nimipango mingi ya maeneleo ambayo huishia kwenye makaratasi, ni hadithi zaalinacha, miaka hamsini ya mafanikio yasiyolingana na uhalisia. Ni kama tunadhamira ya dhati ya kupima miaka mafanikio ya miaka hamsini (50) ya uhuru mimininasema tunapasa kujipima kwa kuangalia mataifa ambayo wakati wa uhurutulikuwa karibu sawa kiuchumi kama vile Indonesia, Malaysia nk. ili kuona wenzetu wako wapi na wanafanya ninisasa kwa kullinganisha nasi. Jambo moja ambalo naamini hatujafanikiwa naambalo limechangia kuwepo hapa tulipo nikiamini ni nyuma ya matarajio ni kwambapamoja na kupata uhuru, nchi bado haijakombolewa. Kwa kawaida na kimsingiukombozi wa kweli hufutia uhuru. Kama nchi haitakombolewa furaha yetu ya uhuruni ubatili mtupu na kujilisha upepo. Wanayofuraha siku zote watawala watawalio watuwasiofikiri, ukombozi una uhai wake katika mioyo,matendo na undani wao na hivyo ni lazimauhalisia huo kuhuishwa kila siku il kupata na ama kuleta msukumo mpya kwamabadiliko ya ukombozi makini, kama ilivyo kwa ua likatwapo kutoka katika shinana ama mzizi ulipao uhai, litanyauka na hatimaye kufa, hivyo ndivyo anavyopaswakuwa mpigania ukombozi, kwamba anapaswa siuku zote kuhuisha misingi yake nauhalisia wake katika kutafuta ukombozi bila kuchoka ama lau kurudi nyuma. Kama nchi itapata uhuru tu na bila kuelekeakatika ukombozi inaweza baki ni nchi ya kiimla nchi yenye viongozi kandamizi nawalafi wa mdaraka, wasiopenda kuambiwa ukweli na zaidi wasio na hata chembe yaheshima ya kuongoza. Heshima ya kuongoza ni pamoja na kutii mamlaka ya umma,umma na kushughulikia mahitaji na ama maslahi ya umma huo uliowawekamadarakani.
  Ni aibu na fedheha kwa watawala kuepamajukumu na ma wajibu wao katika kuwaletea wananchi maendeleo na zaidi kufikirikwamba wao kazi yao ni kutawala na kupanga bajeti zisizotekelezeka; ni aibu.Uwajibikaji wa viongozi haupo. Ninafikiri kwamba kutowajibika huku nikwasababu kuendelea kuwepo kwa kile kizazi cha wanaojiita au naweza kuwaitakizazi cha wakati wa uhuru cha jamii tenganifu iliyojitwalia uhalali wa kulakeki ya taifa kwa ubinafsi wao. Kuna jambo ambalo kizazi cha baadhi ya watawalakatika Tanzania wamefanikiwa, naam nalo ndilo hili, kuweka matabaka ya wahodhiutawala na watawaliwa. Wahodhi utawala ni wale wanaoona kwamba utawala utatokakwa kizazi cha fulani ama fulani. Taifa linahitaji ukombozi kutoka kwa hao,ukombozi halisi utakao wapatia wananchi uwezo wa kuwaongoza watawala na amakuwatawala watawala. Pale hilo litakapotokea ni wakati ambao ukombozi halisiutakapokuwepo. Ni hii ndio maana ninayothani inashabihiana na ya “nguvu yaumma”. Nguvu ya umma inaposhika hatamu hakuna kuhodhi madaraka na hakunakutawala bila nidhamu. Kuna msemo wa Kilatino unaofahmika kwawatu wengi kwamba “Vox populi Vox Dei,”ikiwa na maana, sauti ya watu ni sauti ya Mungu, hivyo basi ni vema ikatmbulikakwamba watu wanapawa kuwa na nguvu zaidi juu ya watawala ambao kimsingi ndilokundi la wachache. Ukombozi wa kweli utakuja paleambapo kilamwananchi ataamua kupaza sauti ya “tumechoka na sasa inatosha” dhidi ya utawaladharimu wa kundi la wachache na wauza nchi. Katika hilo kinachohitajika sasa niHASIRA YA WANANCHI dhidi ya kuibwa na kuuzwa kwa nchi yao. Nasisitiza HASIRADHIDI YA UNYANYASAJI, UTAWALA WA KIIMLA, UTAWALA USIOJALI KUWAJIBIKA KWA AJILIYA WALIOWAWEKA MADARAKANI. Ni hasira tu inayotosha kuleta ukombozi wa kweli,naam hasira tu. Katika kutafuta ukombozi ni heri kaburichakavu la shujaa kuliko nyumba angavu ya mwongo na mnafiki. Historiainaonesha kwamba watawala wetu wengihawana uzalendo, ni waongo na ni wanafiki, wamejivisha ngozi ya kondoo wakatini mbwa mwitu wakali.Mikono yao imejaa damu ya watu wasio na hatia, mioyo yaoimejaa ubinafsi, ukatili na unyanyasaji,macho yao yamepofushwa na rushwa,nyumba zao zimejaa anasa, nao hufurahia manyanyaso ya wanyonge. Nikwa hali hiyo nashawishika kusisitiza kwamba yale yanayoendelea katika taifahili, ufisadi na matatizo mbalimbali yanayoendelea kulikumba taifa ni zao lakutokuwepo na ukombozi wa kweli. Na ukombozi wa kweli ni pamoja na mambomengine kuondoa tabaka la wale wajionao kuwa na haki juu ya wengine, haki yakuendelea kutawala, kujikasimu mamlaka yasiyo na kifani na zaidi kuwasahauwananchi na kujali maslahi binafsi. Tabaka la walewa madaraka wasio na nidhamuya uongozi na wala uzalendo hata chembe. Niwakati mzuri huu, wakati wa kusema tumechoka tena tumechoka sana na tunahitajimabadiliko. Kuna msemo usemao, “huwezi kufundisha mbwa mzee mbinu mpya” na fikra za ukale hubaki na msingi wa ukalezaweza kutumika kujifunzia namna ya kuimarisha fikra mpya na fikra mpyazinapaswa kuwa ni zao la ukombozi. Ugumu wa maisha unaoendelea sasa ni zaola fikra za ukale, fikra mgando za enzi za uhuru. Tunahitaji enzi mpya, enzi zaukombozi. Dhahabu hutakaswa kwa moto, uhuru huimarishwa kwa ukombozi. Chakulahunogeshwa na chumvi, ukombozi hunogeshwana mapinduzi ya fikra mgando na ya/za tabaka la wana wa uhuru. Uhuru ni mzurilakini kuna neema zaidi katika ukombozi. Kwakuwa taifa lilipata uhuru miakahamsini sasa, tunaweza kusimama na kusema inatosha, tuelekee katika hatuanyingine ya kuondokana na mawazo mgando ya ukale wa wa kale kwa ajili yamustakabali mzuri wa taifa hili ambao watu wake ni maskini mno katika nchitajiri mno. Kama muwindwaji atajifunza mbinu zote zamwindaji wake, uwindaji haupo tena. Mateso na shida zilizopo sasa zinapaswakutumika kujua mbinu za tabaka mgando, na jinsi ya kuliepuka ni kutafutaukombozi wa kweli. Tuko hivi tulivyo na hapa tulipo kwasababu hatuja pataukombozi. Uhuru, na mwisho uwe ukombozi wa kweli. Ile kauli ya miaka 50 ya uhuru, inatiachangamoto. Kwamba tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele, katika hilolazima kila mmoja wetu atambue kwamba tunapaswa kusonga mbele kuelekea kwenyeukombozi, na ukombozi huja tokea katika kilele cha matatizo, ubinafsi, unyongena unyanyasasaji wa kundi la wengi kutoka katika kundi la wachache. Pamoja na kujikomboa kutoka katika utumwawa kufikiriwa na sio kujifikirisha, utumwa wa akili tunahitaji ukombozi wa kuondokana na fikra zaukale, fikra mgando, woga na ama hofu ya kushindwa kufanya maamuzi ya msingi nabadala yake kubaki tukishabikia vitu ama hoja zisizo na msingi. Tunapaswa kuogopa kuogopa kwenyewe kwaniwoga hupenda kujifanya rafiki wa kila mtu na kumfanya mtu huyo kushindwakufanya yale yampasayo kufanya na mwenye uwezo thabiti wa kufanya.
  TUNAPASWA KUBADILIKA, TUUTAFUTE UKOMBOZIHUKU TUKIKUMBUKA KWAMBA UHURU PASIPO UKOMBOZI NI UBATILI MTUPU NA KUJILISHAUPEPO. TUNAWEZA TUBADILIKE WOGA NI ADUI WA MAENDELEO.
   
 2. Vox Populi

  Vox Populi Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wanajamii mnapenda fupifupi eee!
   
Loading...