Uhuru ni kitu mhimu sana katika maisha. Unakupa kufurahia upekee wako, unakupa umiliki wa utu wako na mambo yako, na kukufanya ujione unayo haki ya kufanya utakacho bila kuathiriwa na mtazamo au hisia za mtu mwingine.
Kumekua na kasumba ambayo ujitokeza pindi watu waingiapo kwenye Mahusiano au ndani ya ndoa. Pale mwenza anapotaka ku-push na ku-control uhuru wa mwenzake. Mwenza utamani kumiliki muda, mipango, hisia, na mienendo yote ya mwenza wake, na kumfanya mwenza wake kuwa wazi na at critical risks pale Mahusiano yasipoenda vyema.
Japo wengi utaja sababu za Mahusiano kuvurugika ni kukosa uhaminifu, ukweli ni kuwa sababu kuu ni wapenzi kuhisi mapenzi kuwa ni kifungo na jela ya uhuru wao.
Ni vizuri kutambua mtu yuko radhi kupoteza vyote ili apate uhuru, hivyo kujaribu kubana uhuru wa mwenza katika mapenzi ni sawa kumlazimisha mtu apigane vita vya kudai uhuru.
Ebu fikiri mtu anapoingilia uhuru wako kwa kupekua simu yako, kutaka kujua Leo umeongea na Nani, ulienda wapi, Nani alikupigia, mlikua mnaongea Nini, mbona ulichelewa sokoni au kazini etc. Je ukutanapo na fujo hizo nafsi na akili yako uwa inapatwa na hali ipi ?
Je Mahusiano ni sababu ya kuua uhuru wa mtu ? Je Mahusiano ni kuzika haki ya asili ya uhuru wa mtu juu ya maisha yake?
Ikiwa Mungu anaheshimu uhuru wa binadamu aliyemuumba ,je ni sahii mpenzi kujichukulia haki ya kubaka haki hii ya uhuru wa maisha ya mtu ( personal privacy).
Sent using Jamii Forums mobile app