Mbowe, Dk. Slaa watofautiana timuatimua
BY MWANDISHI WETU
11th June 2012
Freeman Mbowe
Ziara ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika mikoa ya Kanda ya Kusini, imehitimishwa kwa viongozi wa juu wa chama hicho, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk.
Willbroad Slaa kutofautiana.
Hali hiyo ilisababisha msuguano mkali ndani ya kikao cha ndani cha tathmini kilichofanyika mjini Ruangwa muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi
Likangara mjini hapa.
Kutibuana huko kulitokana na Mbowe kukataa mpango wa Dk. Slaa kutimua viongozi katika maeneo mbalimbali ambako ziara hiyo imefanyika wakiwemo viongozi karibu wote wa wilaya Ruangwa mkoani Lindi.
Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu (CWT) wilayani Ruangwa, ambapo Mbowe alipinga hatua ya Dk. Slaa kutaka baadhi ya viongozi akiwemo Mwenyekiti wa Wilaya Abdallah Mang'onyola na mlezi wa chama hicho wilayani hapa Juma Lichonyo ambaye awali alikuwa mwenyekiti wa mkoa wa chama hicho waachie madaraka.
Kikao hicho kilichoanza majira ya saa 2: 30 usiku hadi saa tano, kilifanyika baada ya kumalizika kwa mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali na kupata mafanikio kidogo.
Habari za ndani za uhakika zinasema kuwa mahudhurio hafifu ya watu ndiyo yamemsukima Dk. Slaa kuamuru kufukuzwa kwa baadhi ya viongozi hao akidai wamekisaliti chama hali iliyomfanya Mbowe kupinga, akisema
mpango huo unasababisha chama kulegalega.
Kwa mujibu taarifa za uhakika mkutao huo ulilenga kufanya thathmini baada ya ziara ya viongozi wa Chadema wilayani hapa kukosa watu wengi katika mikutano yao tofauti na matarajio yao hivyo kudai ni hujuma zinafanywa na
viongozi waliowatimua.
SOURCE: NIPASHE
[/QUOTE]
inauma sana habari ya uongo inapogeuzwa na kuaminishwa kuwa ya kweli, na uandishi wa habari wa namna hii kwa kweli si tu unadhalilisha taaluma ya uandishi wa habari lakini pia unakidhalilisha chombo cha habari husika kilichotumika kuripoti habari za uzushi.
kwanza niseme kuwa mimi ni mzaliwa wa ruangwa, nilikuwepo katika ziara ya M4C wilayan ruangwa, nilibahatika kuhudhulia mikutano 3 ya chadema ngazi ya kata (chienjere, makanjiro na likunja) na mkutano mkuu wa viongoz woote uliofanyika jion uwanja wa cwt (sio likangara kama mwandishi alivyoripoti).
katika mkutano huo, si kweli kwamba chadema kilipata idadi ndogo ya wanachi kama ilivyoripotiwa na mwandishi, kama nilivyosema awali mimi nimezaliwa hapa ninapafahamu vizuri, idadi ya wanachi waliofika, katika mkutano huo ni kubwa na inaridhisha.
labda nieleze sababu chache ambazo nadhan mwandishi wa habari hii hakuzifikiria wakati anaandika habari hii:-
kwanza ifahamike kuwa kwa wilaya ya ruangwa chadema haikuwa na nguvu sana kwan wananchi wengi wamekuwa wakiisikia tu kwenye vyombo vya habar, kwa mara ya mwisho chadema walifanya mkutano mkubwa miaka 8 iliyopita, so kwa mazingira haya haiwezi kuvuna watu wengi kama ccm na cuf ambao kila siku wanafanya mikutano hapa ruangwa. katika mkutano huu niliwaona zaidi vijana wasomi, watumishi wa serikali (halmashaur, polis, etc) vijana na akina mama wajasiriamali (waliokuja kusikiliza sera za cdm), wanafunzi wa sekondar, wananchi kutoka mikoa mingine n.k
pili, mwandishi lazima afahamu kuwa, kwa wilaya ya ruangwa yenye wakazi wanaokadiriwa kuwa 150,000 (sawa na kata 3 DSM) tena waliosambaa (scattered) katika kata mbalimbali (zaidi ya 18) si rahisi kujaza watu wengi kama miji mingine.
tatu ifahamike kuwa, chadema walifanya mikutano asubuh kuanzia saa 4 mpaka saa 9 kwenye kata zote wilayan ruangwa, so mkutano wa jion anaousemea mwandish uliwahusu wakaz wa ruangwa mjini tu (kutoka kata 3) ambao hawazidi 20,000, so wananch wengi wa kata za pembezon (zaidi ya kata 15) hawakufika kwenye mkutano wa jion kwan tayar chadema walishapita kwenye maeneo yao.
na mwisho, eneo ambalo mkutano ulifanyika ni ngumu kukadiria idad halis ya walifika kwan ni katikati ya mji (nyuma ya stend kuu ya mabas) hivyo wanach weng walionekana wamekaa kwenye maduka yao, magari yao, makaz yao, sokon, hotelin, gerej, bar n.k na bado wakaendelea kusikia ujumbe wa chadema uliokuwa unaruka kupitia spika zao kubwa.
kuhusu mkutano wa usiku, ukweli ni kwamba mbowe (m/kiti) hata hakushiriki, nilimwona dr. slaa akiendesha mkutano huu akiwa na waitara, na wengine ambao siwajui. na mkutano huu uliwahusu viongoz wa cdm wilayan tu, waandishi hawakuruhusiwa.
huo ndo ukweli.
wito wangu, cdm watoe tamko kupitia tv na magazeti juu ya uzushi huu, kwan uongo ukisemwa sana mwisho waweza kuaminiwa.
by mwana ruangwa.