Elizabeth Dominic
Platinum Member
- Dec 7, 2007
- 4,555
- 3,659
Ujue maybe anachukulia sababu mtandao wa IPP uko chini...........nimejaribu kuufungua haufunguki, lakini kama nikithibitisha kuwa analeta uongo nitakuwa mtu wa kwanza kumreportkama mtoto vile...si uweke link basi watu wakuelewe unang'ang'ana kulazimisha uaminiwe ilihali una kithibiotisho? weka link ya hiyo habari kuwaprove wrong wanaopinga
Naunga mkono hoja 100 kwa 100 hii habari haipo NIPASHE MODS acheni kulegea mnasababisha JF inakuwa kijiwe cha porojo na mambo ya uongo!!
kama mtoto vile...si uweke link basi watu wakuelewe unang'ang'ana kulazimisha uaminiwe ilihali una kithibiotisho? weka link ya hiyo habari kuwaprove wrong wanaopinga
nimesoma gazeti la nipashe leo lote na sikuona habari hiyo.......
hiyo ndio haswa taswira yenu kwa miaka yote hiyo 50, asa kwa nini nijisumbue... thats what defines you and your partyNa wewe ni mmoja wa wavivu wa kufikiri. Unataka utafuniwe kila kitu wakati umeshaambiwa mtandao ni IPP MEDIA?
Kalagabahu!
nimesoma gazeti la nipashe leo lote na sikuona habari hiyo.......
Acha maneno soma HAPA. Acheni kujaza server humu....lo!
Jamaa yuko sahii according to IPP Media, ebu mfungue muone.............mimi sijaona mgogoro wowote zaidi ya tofauti katika majadiliano..........Muongo mkubwa ww.
Magwanda nyie ni kaskazini tu, Kusini sahauni. Mtatoana roho bure.
Mmesikia kuna gesi ya kufa mtu huko ndio mnajidai kujipeleka?
Ukiona hivyo ujuwe kila mtu analake na hapo ndio walipopatia nafasi ya kupumulia. Kimeshanuka huko. Mzee Mtei hataki Slaa agombee tena Urais na Slaa anahakikisha anaweka timu yake itakayomtetea wakati ukifika. Mbowe kastukia, "mpaka kieleweke" .
tena anahitaji kanga huyuWewe Ngoromiko nae! Sasa watu wakitofautiana katika maamuzi fulani ndio "kinawaka?" Hiyo heading ya uzi wako imekaa kiushambenga zaidi!
Ziara ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika mikoa ya Kanda ya Kusini, imehitimishwa kwa viongozi wa juu wa chama hicho, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk.
Willbroad Slaa kutofautiana.
Hali hiyo ilisababisha msuguano mkali ndani ya kikao cha ndani cha tathmini kilichofanyika mjini Ruangwa muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi
Likangara mjini hapa.
Kutibuana huko kulitokana na Mbowe kukataa mpango wa Dk. Slaa kutimua viongozi katika maeneo mbalimbali ambako ziara hiyo imefanyika wakiwemo viongozi karibu wote wa wilaya Ruangwa mkoani Lindi.
Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu (CWT) wilayani Ruangwa, ambapo Mbowe alipinga hatua ya Dk. Slaa kutaka baadhi ya viongozi akiwemo Mwenyekiti wa Wilaya Abdallah Mang'onyola na mlezi wa chama hicho wilayani hapa Juma Lichonyo ambaye awali alikuwa mwenyekiti wa mkoa wa chama hicho waachie madaraka.
Kikao hicho kilichoanza majira ya saa 2: 30 usiku hadi saa tano, kilifanyika baada ya kumalizika kwa mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali na kupata mafanikio kidogo.
Habari za ndani za uhakika zinasema kuwa mahudhurio hafifu ya watu ndiyo yamemsukima Dk. Slaa kuamuru kufukuzwa kwa baadhi ya viongozi hao akidai wamekisaliti chama hali iliyomfanya Mbowe kupinga, akisema
mpango huo unasababisha chama kulegalega.
Kwa mujibu taarifa za uhakika mkutao huo ulilenga kufanya thathmini baada ya ziara ya viongozi wa Chadema wilayani hapa kukosa watu wengi katika mikutano yao tofauti na matarajio yao hivyo kudai ni hujuma zinafanywa na
viongozi waliowatimua.
CHANZO: NIPASHE