Uhonzolomo wa maghufuli na balozi Mrango | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhonzolomo wa maghufuli na balozi Mrango

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sabato masalia, Dec 8, 2011.

 1. S

  Sabato masalia JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  "UHONZOLOMO" ni neno toka katika lugha ya watani zangu wazaramo,walugulu na wakwele lenye maana ya jambo la hatari linalofanywa na mtu na athari zake ni kubwa katika jamii mtu mwenye kufanya hivyo huitwa MHONZOLO yaani mtu hatari wa kuogopwa, hii ndio hali iliyopo wizara ya ujenzi tangu bwana Maghufuli kupewa wizara akisaidiana na katibu mkuu wake aliyeongezewa muda balozi Herbert Mrango imekuwa vurugu mtindo mmoja.

  Juzi Maghufuli,Mrango na kibaraka wao wao mkurugenzi wa TANROADS bwana Mfugale wamefanya kitendo cha ajabu, hatari na cha aibu baada kufanya uteuzi kinyume na taratibu, wameteuwa mameneja wapya wa mikoa wa TANROADS kinyemelea bila kutangaza nafasi hizo, hiyo ni kinyume na taratibu.

  kama hilo halitoshi Maghufuli kampa ukaimu ukurugenzi wa barabara bwana Nyamhanga huyu bwana alikuwa Kagera na ndiye aliyefanya Blanda badala ya barabara kupita toka Buzilayambo- Biharamulo akageuza kuipitisha Chato kumfurahisha Maghufuli ikawa scandal kubwa walipoingia akina Kawambwa na Chambo walimtoa huyu bwana na kumhamishia Rukwa,alipokuwa kagera pia alimjengea hoteli Maghufuli, Maghufuli analipa fadhila kampandisha na kumhamisha muharibifu huyu kamtoa Rukwa na kumleta Dar kuwa kaimu mkurugenzi wa barabara , mwingine ni Julias Ndiamkama alifukuzwa kwa ufisadi Tanroads amemrudisha tena umeneja mkoa wa Dar es salaam,huyu alipokuwa meneja wa mkoa wa Dar kabla Maghufuli kuhamishwa wizara hiyo ndie aliyemjengea Maghufuli ghorofa oysterbay leo Maghufuli kalipa fadhila kwa kumrudisha tena fisadi huyu ili aendeleze uharibifu na kumnufasiah tena Maghufuli. hizo ndio mbio za Maghufuli 2015 anaweka watu wa kukusanyia pesa za kampeni.
   
 2. k

  kalanjadd Member

  #2
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maghufuli ni hovyo sana ila anajuwa kuficha makucha yake, kumgundua inataka umakini sana
   
 3. yode

  yode Member

  #3
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watu mna mambo mtu asifanye jema. uliopost jambo hili una data??/
   
 4. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Bado nakumbuka kauli ya Mama Sophia Simba aliposema CCM hakuna msafi'kila nikijaribu kuangalia viongozi waliopo CCM ndipo nazidi kuiamini kauli ya Sophia Simba
   
 5. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hata mzee makamba kama ulizikiliza hotuba yake baada ya kuondolewa ukatibu mkuu alisema hajafanya makosa peke yake ,hata lowasa alimuarifu jk kuhusu dowani ccccccccmmm giza

   
 6. Possibles

  Possibles JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  Hizi habari ni za uwongo na majungu.Kuna uwezekano mtoa uzi huu ni muathirika katika reshuffle hii.
   
 7. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maaelezo ya mtoa mada ni kama kilio cha mkosaji vile,lete data kuthibitisha hayo madai,vinginevyo tutaelewa kuwa ulikuwa unanyatia hizo nyadhifa na ulipozikosa basi unaporomosha tuhuma bila ushahidi,Kweli CCM hakuna msafi ila hata uchafu ulioko upo wenye nafuu.
   
 8. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #8
  Dec 8, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado endeleeni kutujuza ila tu kuwe na udhibitisho wa tuhuma kwani hapa ni kwa great thinkers bwana.
   
 9. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Ogopa sana mwana CCM anaeongea kwa msisitizo huku akiwa na tabasamu la kidwanzi!! ni wabaya sana hao....
   
 10. D

  Divele Dikalame Member

  #10
  Dec 8, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani mwenye thread hakukurupuka kaleta tuhuma ni muhimu kuzifanyia kaz,i ni vyema tukamshukuru kwa kutustua na kutujuza juu ya kinachoendelea hapo wizara ya ujenzi
   
 11. H

  Heri JF-Expert Member

  #11
  Dec 8, 2011
  Joined: Aug 28, 2007
  Messages: 242
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Sababu moja ya Mrema kuondelewa Tanroads ilikuwa kutangaza nafasi za manager za mikoa. Leo hii wanateua watu. Utawala bora ingekuwa ni kutangangaza nafasi hizo na pawe na mchakato transparent katika kuchagua hao managers.
  Ingekuwa Mrema amefanya haya mabadiliko pangekuwa na kelele nyingi tu.
   
 12. G

  Gud gud Member

  #12
  Dec 8, 2011
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama hayo yana ukweli basi bora Magufuli kaoza kidogo awo kina KAWAMBWA hata kama waliingilia mbona yao sivyondivyo wao ndo WAMEOZA kabsaaaaa
   
 13. N

  NewOrder JF-Expert Member

  #13
  Dec 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 489
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Katika hadithi yote hii inayohusu hotel, nyumba nk inaonekana kama si mambo yanayoweza kuthibitika. Kinachoweza kuthitika ni uteuzi wa hawa jamaa bila kutangaza nafasi za kazi. Hili ndilo la msingi.

  Shutuma ya kupindisha barabara inasikika kama uzushi tu. Si rahisi kwa jambo hili kufanyika ngazi ya mkoa wakati kuna mkurugenzi wa barabara.
   
 14. saimon111

  saimon111 JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2013
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,712
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa ni tatizo sana nae, maana kuna rafiki zangu ni wahandisi kwenye hiyo wizara ya ujenzi wanasema jamaa ni mtu wa 10% vibaya mno
   
 15. B

  Bijou JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2013
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145

  Ni fisadi tu huyo nyumba ZA oyster bay nimeziona na nika shangaa!!!!!!! Mishahara ya serikali inajulikana, hata Kama ukisema mkopo kuna dhamana, lambada Kama aliweka uwaziri Kama dhamana, RIP Tanzania
   
 16. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2013
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Inaelekea wewe ni mtu wa majungu sana.
  Mrema hajambo?
  Mlikula na Mrema bila kusaza, Magufuli kasafisha madudu yenu, na sasa mko benchi.
  Hivi siku hizi wachina hawawtembelei?
   
Loading...