Gullam
JF-Expert Member
- Dec 1, 2013
- 5,240
- 3,932
Salamu wana body.
Kwanza nianze kuwatakia waislamu wote funga njema ya mwezi mtukufu.
Leo kwa mara ya kwanza nimepita feri kupitia mwendo kasi, mara niliposhuka tu kivukoni terminal nikapatwa na haja ndogo, nikaona si uungwana kujibana wakati huduma ya choo ipo pale. Nikatoa dinari yangu, ili ninue ile huduma, lakini ghafla nilipo ingia ndani mambo niliyoyakuta nilishindwa kuvumilia.
Nilijiuliza maswali mengi mengi yasio na majibu, je kama kweli wameshindwa kuvilekebisha hivi vyoo ambavyo huduma yake inalipiwa, wateweza kweli kutengeneza stendi zao, au hata magari yao yatakapo haribika? Chonde chonde watanzania tuache kasumba ya kizamani, mradi usio hata na miaka mitatu hali iko hivi kweli!! Wajuzi wa mambo njooeni muwashauli hawa waungwana. Naambatanisha na picha hapa chini.