DR. MWAKABANJE
JF-Expert Member
- Nov 7, 2012
- 1,976
- 3,127
Moja kati ya maamuzi ya awamu hii yanayotutesa baadhi ya watumishi wa umma ni uhamisho wetu au wenza wetu kutoka sehemu moja kwenda nyingine ili kuishi na familia husika.
Hili jambo limejadiliwa sana hapa lakini kwa masikitiko makubwa hakuna mahala popote wala kwa njia yoyote wahusika wamewahi kutolea maelezo suala hili,angalau basi hata kama kuna utaratibu mpya tujulishwe.
Sio siri maisha yamekuwa magumu mno halaf kuishi mbali na familia ni kuniongezea mfuko wa cement kg 50 wakati kilo 30 zinanihenyesha, hapa wafanyakazi tunateswa kisaikolojia. Viongozi wetu kuwa na huruma na moyo wa kujali wengine, fikiria mke na mtoto pamoja na binti wa kazi yuko Tanga halafu baba Songea kwa mshahara uleule toka mwaka juzi wawili hawa wote walipe nyumba, umeme, maji, chakula nk wakati wangekaa pamoja bejeti ingeshuka hapo bado gharama za nauli kutembeleana na bahati mbaya Tanga au Songea si kwa wazazi wao kwa hiyo inabidi tena kusafiri kuwatembelea wazazi.
Binafsi kazi imekuwa chungu kwangu.