Uhamiaji Tanzania

Uhamiaji Tanzania

Ksuley

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2015
Posts
1,166
Reaction score
445
Hbr Ya Asbh Wanajamvi, Leo Napenda Kupata Maelekezo Au Maelezo Kutoka Idara Ya Uhamiaji Tanzania, Swali Na Malalamiko Yangu, Ni Kuhusu Utoaji Wa Hati Za Dharura Za Kusafiria, Ambazo Watumiaji Wengi Ni Madereva Na Wasaidizi Wao, Kutoka Tanzania Kwenda Nchi Za Afrika Mashariki Na Kati, Awali Tulikuwa Tukipata Hati Hizo Kwa Muda Wa Mwaka 1 ,Kwa Gharama Tofauti Vituo Vingi Walichaji Elfu 20 Na Vingine Elfu 15 ,Hakuna Hata Risiti Walau Ile Ya Ticket Ya Bus, Sasa Tokea Mwisho Wa 2017 Utaratibu Umebadilika Kwa Kutoa Toka Muda Mwaka 1 Hadi Ya Safari 1 Tu (Single Journey) Yaani Ukitoka Na Kurudi Imeisha. Hivyo Ikiwa Kwa Mwaka Utasafiri Mara 10 ,Basi Yatupasa Tukate Hati Hizo Mara 10 Pia. Sasa Tatizo Ni Kila Safari Unatakiwa Uende Kwa Wakili Kuapa Kwa Kujaza Form Za Affidavits Na Kulipia Elfu 15 ,Na Hiyo Hati Ya Dharura (Passipot) Elfu 10 ,Passipot Size Elfu 3 ,Photocopy Kuanzia Kadi Za Gari, Leseni Ya Kuendesha Gari Na Kitambulisho Elfu 1.5 .Jumla Elfu 29.5 .Kila Safari. Swali Kwanini Kila Safari Lazima Niende Kwa Wakili Kuapa Tu!!!!?? Kwani Taarifa Za Safari Iiiyopita Zimeenda Wapi, Wkt Naona Anaweka Ktk Kompyuta!!!? Kwanini Mi Nikiwa Naomba Nyingine Nisiihie Kwa Afisa Uhamiaji Tu Kwa Kuchukua Taarifa Zangu Za Mwezi Uliyopita Na Kuthibitisha Kwa Hati Yangu Iliyoisha Ambayo Ninayo!!?!? Haya Kwanini Basi Wasingeiweka Iwe Walau Ya Miezi 6 Tu ,Kama Mwaka 1 Ni Mrefu Na Wao Wanakosa Makusanyo. Hivi Madereva Wana Kipato Kikubwa Kiasi Gani Hadi Kuwabana Na Kuwakamua Hivi Jmn, Sawa Lengo Kukusanya Mapato Mengi, But Hili Si Sawa Jmn, Hili Lipo Pale Uhamiaji Makambako Ndio Nimekumbana Nalo Binafsi. Tunawaomba Wahusika Mlitazame Hili Jmn.
 
Kwa kweli madavoo tuna shida wenzenu uhamiaji shida, ukija Sumatra shida,barabarani huku kwa wazee weupe ndio dddddduuuhhh maumivu ya htar sasa hv hakuna sheria inaumiva ma-davoo km zebra kuwe na mtu asiwepo unatakiwa usmame uspocmama wazee weupe wakikuona iandae tu 30 elf yko.
 
Ndo maana unashindwa hata kuweka kituo kwenye habari yako? Uandishi gani huu mkuu?
 
Mleta mada una hoja ya msingi, uhamiaji walipaswa watumie taarifa zako zilizopita ili kukupatia hati nyingne ya kusafiria dharura badala ya kupeleka taarifa mpya kila wakati unapohitaji kusafiri.
Mie kero yangu kuu kwa hao uhamiaji ni juu ya utoaji wa passport kubwa ya kusafiria......huu ni mwezi wa tatu sasa vigezo vyote nimekamilisha yakiwamo malipo NMB Bank ya Tsh 50, 000/- lakini bado sijapatiwa hati hiyo!
Ukiuliza unajibiwa karatasi zimeisha makao makuu, ajabu ni kwamba pia wanakujibu kama unaharaka nayo sana nenda dar (makao makuu) sambamba na risiti zako za malipo alafu ndani ya siku mbili tatu utaipata hati yako.....haya sio mazingira ya kudaiwa rushwa kweli?!
Tafadhali Mh Waziri na wote wenye dhamana mtusaidie, hii ni kero kubwa.
 
Hbr Ya Asbh Wanajamvi, Leo Napenda Kupata Maelekezo Au Maelezo Kutoka Idara Ya Uhamiaji Tanzania, Swali Na Malalamiko Yangu, Ni Kuhusu Utoaji Wa Hati Za Dharura Za Kusafiria, Ambazo Watumiaji Wengi Ni Madereva Na Wasaidizi Wao, Kutoka Tanzania Kwenda Nchi Za Afrika Mashariki Na Kati, Awali Tulikuwa Tukipata Hati Hizo Kwa Muda Wa Mwaka 1 ,Kwa Gharama Tofauti Vituo Vingi Walichaji Elfu 20 Na Vingine Elfu 15 ,Hakuna Hata Risiti Walau Ile Ya Ticket Ya Bus, Sasa Tokea Mwisho Wa 2017 Utaratibu Umebadilika Kwa Kutoa Toka Muda Mwaka 1 Hadi Ya Safari 1 Tu (Single Journey) Yaani Ukitoka Na Kurudi Imeisha. Hivyo Ikiwa Kwa Mwaka Utasafiri Mara 10 ,Basi Yatupasa Tukate Hati Hizo Mara 10 Pia. Sasa Tatizo Ni Kila Safari Unatakiwa Uende Kwa Wakili Kuapa Kwa Kujaza Form Za Affidavits Na Kulipia Elfu 15 ,Na Hiyo Hati Ya Dharura (Passipot) Elfu 10 ,Passipot Size Elfu 3 ,Photocopy Kuanzia Kadi Za Gari, Leseni Ya Kuendesha Gari Na Kitambulisho Elfu 1.5 .Jumla Elfu 29.5 .Kila Safari. Swali Kwanini Kila Safari Lazima Niende Kwa Wakili Kuapa Tu!!!!?? Kwani Taarifa Za Safari Iiiyopita Zimeenda Wapi, Wkt Naona Anaweka Ktk Kompyuta!!!? Kwanini Mi Nikiwa Naomba Nyingine Nisiihie Kwa Afisa Uhamiaji Tu Kwa Kuchukua Taarifa Zangu Za Mwezi Uliyopita Na Kuthibitisha Kwa Hati Yangu Iliyoisha Ambayo Ninayo!!?!? Haya Kwanini Basi Wasingeiweka Iwe Walau Ya Miezi 6 Tu ,Kama Mwaka 1 Ni Mrefu Na Wao Wanakosa Makusanyo. Hivi Madereva Wana Kipato Kikubwa Kiasi Gani Hadi Kuwabana Na Kuwakamua Hivi Jmn, Sawa Lengo Kukusanya Mapato Mengi, But Hili Si Sawa Jmn, Hili Lipo Pale Uhamiaji Makambako Ndio Nimekumbana Nalo Binafsi. Tunawaomba Wahusika Mlitazame Hili Jmn.
Jiongeze, hati ya kusafiria kubwa unalipia shilingi elfu hamsini. Kwa miaka kumi. Kwa nini usikate kubwa ukakaa miaka kumi bila bughuza?
 
Kwa kweli madavoo tuna shida wenzenu uhamiaji shida, ukija Sumatra shida,barabarani huku kwa wazee weupe ndio dddddduuuhhh maumivu ya htar sasa hv hakuna sheria inaumiva ma-davoo km zebra kuwe na mtu asiwepo unatakiwa usmame uspocmama wazee weupe wakikuona iandae tu 30 elf yko.
MADEREVA WENZANGU HABARINI ZA JUMAPILI. NASIKITIKA SANA NAONA MADEREVA BADO WANAANDIKIWA FAINI KWA KOSA LA KUTO SIMAMA KWENYE ZEBRA NAOMBA KILA DEREVA ASOME VIZURI SHERIA HII NA UIELEWE NA UINAKILI IKIWEZEKANA ANDIKA KWENYE KARATASI SIKU UKIKAMATWA NA ASKARI ASIE IJUA SHERIA MUELIMISHE SHERIA YENYEWE NI HII HAPA CHINI

*JE NI WAKATI GANI NISIMAME KWENYE ZEBRA CROSSINGS AU JE NI AMRI KUSIMAMA KWENYE ZEBRA HATA KAMA HAKUNA MWENDA KWA MIGUU ANAYEVUKA?* Sheria inasemaje?
Sheria ya usalama barabarani kifungu cha 65 kinahusu vivuko vya waenda kwa miguu, yaani pedestrian crossings.
Kifungu cha 65(1) kinamtaka mhandisi mkuu kusimika alama za vivuko vya waenda kwa miguu mahali panapofaa barabarani.
Kifungu cha 65(2) kinatamka kwamba mahali popote ambapo alama itakuwa imewekwa itachukuliwa kuwa imewekwa kihalali na itakuwa halali isipokuwa kama itakanushwa au kuthibitishwa vinginevyo.
Kifungu cha 65(6) kinamtaka kila anayetumia kivuko cha waenda kwa miguu kufanya hivyo kwa tahadhari kubwa na atumia kivuko hicho kuvuka barabara. Aidha kifungu cha 65(7) kinamtaka mtumiaji kivuko huyo kutokanyaga barabara ili avuke *bila kuzingatia umbali na spidi ya magari yanayokuja*
Kifungu cha 65(10) kinasema *itakapotokea mtembea kwa miguu anatumia au anataka kutumia kivuko cha waenda kwa miguu, dereva wa gari atasimama kabla ya kivuko hicho ambacho hakiongozwi na taa za barabarani, ishara za barabarani au askari*. [Hivi vivuko vinavyokuwa vimechorwa barabarani kwa mistari ya pundamilia ambapo mtu anavuka bila usimamizi wa askari au maelekezo ya taa]. Dereva ataendelea tu na safari ikiwa atajiridhisha kuwa hakuna mtembea kwa miguu anayetumia(anayevuka) au anakusudia kuvuka barabara.
HIVYO BASI, JIBU NI KWAMBA sio lazima dereva asimama kwenye kila zebra crossings hata kama hakuna anayevuka, dereva atapunguza mwendo na kuangalia iwapo kuna mtu anavuka au ananuia kuvuka, kama hakuna ataendelea na safari. Kwa hiyo, *dereva atasimama kwenye eneo kabla ya zebra crossing pale wakati wote ambapo kuna mtu au watu wanavuka au wanakusudia kuvuka.*
Ni matumaini yangu tumeelewana. Mwelimishe na mwenzio.
 
Hoja yake ndiyo ya msingi mkuu, tunatofautiana jinsi ya kujieleza hata uandishi , pia wakati mwingine mtu ana andika akiwa na ameghafilika.
Ndo maana unashindwa hata kuweka kituo kwenye habari yako? Uandishi gani huu mkuu?
 
Jiongeze, hati ya kusafiria kubwa unalipia shilingi elfu hamsini. Kwa miaka kumi. Kwa nini usikate kubwa ukakaa miaka kumi bila bughuza?
Mkuu mawazo yako ni mazuri na binafsi ndicho nilichokifanya, tatizo hiyo hati kubwa ya kusafiria hadi kuipata utazungushwa weee hadi ukome.....sasa wakati unazungushwa katikati hapo kuna vijisafari ndo hapo tunalazimika kutumia hati ya kusafiria kwa dharura.
 
Siku hizi hati kubwa ni siku tano mpaka wiki Tu unapata.
 
Mkuu siku tano hadi wiki moja labda ni kwa dar pekee, tulioko mikoani bado sana....
imagine nipo Dodoma, makao makuu ya nchi na sasa ni miezi kadhaa bado nasubiri hati kubwa ya kusafiria kutoka dar!!
 
Unaweza ukamaliza taratibu zote mpaka finger print na bado kupata passport ni shida ukienda uhamiaji unambiwa njoo baada ya wikibili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom