Mnamo tarehe 22 Feb majira ya saa nne asubuhi katika jengo la ofisi za kampuni za ndege katika kiwanja cha ndege cha Mwl.Julius K.Nyerere, makachero watatu wa kike wa uhamiaji waliingia ofisi za kampuni ya ndege ya Etihad Airways na kufanya mahojiano mafupi na dada mmoja raia wa Kenya aitwae Mercy Mutegi ambaye ni Meneja na kisha kuondoka nae kuelekea ofisi za mkoa za Uhamiaji zilizopo jengo la makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Walimuhoji kwa siku hiyo na kumuachia kwa dhamana ya kubaki na hati yake ya kusafiria. Walibaini kuwa dada huyu yupo nchini toka mwezi September 2015 bila kibali cha kazi na amekua akiishi Double Tree by Hilton kwa wakati wote. Baada ya zoezi la kumuita kila siku na kumuachia jioni, hatimaye walimtorosha nchini tarehe 26 February na ndege ya KQ485 iliyoondoka saa 12 jioni kuelekea Nairobi badala yakufuata utaratibu wa kumuondoa mhamiaji yeyote haramu. Kwa sasa wako katika hatua za kuhakikisha dada yule anapata kibali cha kazi baada ya kupokea mlungula kutoka kwa Meneja wa viwanja vya ndege Africa wa kampuni ya Etihad ambaye amakuja kwa ajili ya kazi hiyo ya kumtoa na kuhakikisha kibali cha kazi kinapatikana ili aweze kurudi mara moja. Nchi hii kuna watendaji wameoza kwa rushwa na itakua ngumu sana kutumbua haya majipu. Uhamiaji uwanja wa ndege kweli hawana taarifa za watu wa namna hii na wamekua wakifanya nae kazi wakati wote bila hata kuhoji?