Uhamiaji chunguzeni kampuni ya Capital Drilling

mwibagi2015

Member
Jul 29, 2015
98
42
Napenda kupongeza kwa taasisi hii kupata "Boss" mpya.

Natambua kabisa maafisa mbalimbali wa Serikali ni members/wanapita huku JF kama kisima cha habari za uhakika.

Leo napenda kuzungumuzia Kampuni ya Uchimbaji Madini iliyoko Mwanza Capital Drilling (T) LTD na ku-operate katika migodi ya Geita, North Mara, Bulyanhulu na sites ndogo ndani ya nchi yetu.

Hii Kampuni imeajiri wafanyakazi wengi sana kutoka nje "Expats" ambao wanafanya kazi zinaweza kufanywa na Watanzania na kwa ufanisi mkubwa.
Njia wanazotumia kupata vibali vya kazi yaani work and residential permits ni hii hizi;

1. Kwa rushwa, hao jamaa wamekuwa nchini kwa mda mrefu hivyo wanafahamiana na officers wote Mwanza na Geita. Baadhi ya maofisa wa uhamiaji ambao si waminifu ndo hucheza huu mchezo kupata fedha kwa njia ya rushwa na kutoa vibali.

2. Kudanganya utaalamu/taaluma na nafasi zao za kazi (educational level, experience and position/title)
Mfano, utakuta kibali cha mfanyakazi huyu ni Senior drill supervisor lakini achofanya kila siku ni kupaka mashine vilainishi( greasing) au kusambaza mafuta kwenye mitambo na magari ya Kampuni.
Hii yote hufanikiwa kwa kupata ushauri kutoka kwa maofisa wa uhamiaji katika maeneo hayo.

3. Baada ya Serikali ya awamu ya tano kushika madaraka kidogo kutoa hofu kwa kiasi fulani sasa expats wapya hulipia vibali vya mda "Business visa" kama consultant huku ni wafanyakazi wa kawaida yaani waajiriwa wa Kampuni.
Mfano, nafasi za storemen kutoka Zambia x 2 (Mwanza), Misri x 2 (Geita na North Mara)

4. Kampuni hii inamiliki Kampuni tofauti zinazofanya kazi tofouti ambazo ni Welforce International inahusika na gyro survey na Stealth Global Industries inahusika na manunuzi sehemu mbalimbali duniani. Hizi Kampuni hazijasajiliwa nchini hivyo hawalipi kodi yoyote. Wafanyakazi wa hizi Kampuni mbili ni kutoka nje na wanaomba vibali kupitia capital drilling huku wakijua siyo kweli.

Kwa leo naomba niishie hapo wakuu, tukipata mrejesho chanya kutoka Serikalini next time nitaweka wazi majina na vibali vya Wafanyakazi wote kutoka nje wasio hitajika ndani ya nchi kwa nafasi zao. Asante.
 
Wao wanakimbizana na manji tu kwa maslahi ya kisiasa hasa kumuunga mkono lowasa wakati wa uchaguzi.chuki,ghiriba hasira,visasi
 
Hao capital drilling hawana shida!wasijingize tukwenye siasa

Ova
 
watanzania chuki dhidi ya wawekezaji na watu wenye pesa inatuisha lini? mbona tunakuwa na roho nyeusi kiasi hiki! aah
 
Hivi drilling ndio uchimbaji madini siku hizi? Rekebisha maelezo yako
 
Napenda kupongeza kwa taasisi hii kupata "Boss" mpya.

Natambua kabisa maafisa mbalimbali wa Serikali ni members/wanapita huku JF kama kisima cha habari za
uhakika.

Leo napenda kuzungumuzia Kampuni ya Uchimbaji Madini iliyoko Mwanza Capital Drilling (T) LTD na ku-operate katika
migodi ya Geita, North Mara, Bulyanhulu na sites ndogo ndani ya nchi yetu.

Hii Kampuni imeajiri
wafanyakazi wengi sana kutoka nje "Expats" ambao wanafanya kazi zinaweza kufanywa na Watanzania na kwa ufanisi mkubwa.
Njia wanazotumia kupata vibali
vya kazi yaani work and residential permits ni hii hizi;

1. Kwa rushwa, hao jamaa wamekuwa nchini kwa mda mrefu hivyo wanafahamiana na
officers wote Mwanza na Geita. Baadhi ya maofisa wa uhamiaji ambao si waminifu ndo hucheza huu mchezo kupata fedha kwa njia ya rushwa na kutoa vibali.

2. Kudanganya utaalamu/taaluma na nafasi zao za kazi (educational level, experience and position/title)
Mfano, utakuta kibali cha mfanyakazi huyu ni Senior drill
supervisor lakini achofanya kila siku ni kupaka mashine vilainishi( greasing) au kusambaza mafuta kwenye mitambo na magari ya Kampuni.

Hii yote hufanikiwa kwa kupata ushauri kutoka kwa maofisa wa uhamiaji katika maeneo hayo.
3. Baada ya Serikali ya awamu ya tano kushika madaraka
kidogo kutoa hofu kwa kiasi fulani sasa expats wapya hulipia vibali vya mda "Business visa" kama consultant huku ni wafanyakazi wa kawaida yaani waajiriwa wa Kampuni.

Mfano, nafasi za storemen kutoka Zambia x 2 (Mwanza), Misri x 2 (Geita na North Mara)

4. Kampuni hii inamiliki
Kampuni tofauti zinazofanya kazi tofouti ambazo ni Welforce International inahusika na gyro survey na Stealth Global Industries inahusika na manunuzi sehemu mbalimbali
duniani. Hizi Kampuni hazijasajiliwa nchini hivyo hawalipi kodi yoyote. Wafanyakazi wa hizi Kampuni mbili ni kutoka nje na wanaomba vibali kupitia capital
drilling huku wakijua siyo kweli.

Kwa leo naomba niishie hapo wakuu, tukipata mrejesho chanya kutoka Serikalini next time nitaweka wazi majina na
vibali vya Wafanyakazi wote kutoka nje wasio hitajika ndani ya nchi kwa nafasi zao. Asante.

Hee haya wamekusikia watakwenda
 
Kuna nafasi nyingine wageni huajiriwa kwenye makampuni ya kigeni kutokana na sheria. Sheria inampa haki mwekezaji kuajiri idadi fulani ya watu anaowaamini toka nje kwenye nadasi fulani ambazo yeye anaona ni muhimu kufanya hivyo.

Pili kuna shida ya uaminifu kwa watanzania wengi wanapoajiriwa, ndiyo maana kuna baadhi ya makampuni huajiri Wanepali kama walinzi wa kusimama magetini, siyo kwa sababu ya ujuzi bali kwa sababu ya uaminifu.

Maeneo kama hayo ya store, yanahitaji sana uaminifu kuliko utaalam. Wewe mwenyewe hujasema kama unafanya kazi kwenye kampuni hiyo au pengine umefukuzwa kazi, na ukaona kuna namna unaweza kulipiza kisasi maana Watanzania wanapenda sana visasi hata pale ambapo wao ndiyo wenye makosa.
 
Ujinga wetu ndio unatughalimu tunashindwa kuweka mazingira mazuri ya sisi wenyewe kuchimba madini yetu hadi hao pua ndefu waje kuchimba huku wanatunyanyasa
 
NI MPUMBAVU TU NDIYE ANAYEAMINI KUWA WAGENI WATATUTOA KATIKA LINDI LA UMASKINI KWA KURUHUSIWA KUJA KUCHIMBA MADINI YETU.

NI WAZALENDO NA WENYE AKILI TU KAMA MWL NYERERE AMBAO WALIUPINGA UPUUZI HUU AMBAO LEO UNATUNYANYASA. NAMUUNGA MKONO MHESHIMIWA RAIS MAGUFULIKWA JUHUDI ZAKE ZA KUFUFUA UZALENDO NA UCHUMI WA NCHI YETU NA KUKATAA UTWANA NA UPUMBAVU UNAOONEKANA KUTUKOLEA WATANZANIA.
 
Wao wanakimbizana na manji tu kwa maslahi ya kisiasa hasa kumuunga mkono lowasa wakati wa uchaguzi.chuki,ghiriba hasira,visasi
Sidhani kama kuna mtu ana akili timamu atafikiria kuwa uhamaji walikuwa hawana habari ya kuajiriwa kwa wageni hawa, ila wameona uhamiaji imebadilishwa uongozi na kwa hali ya kisiasa sasa bomu litalipuka kwa hiyo wakaamua kuilipua Quality, ili kumpata Manji.
 
Napenda kupongeza kwa taasisi hii kupata "Boss" mpya.

Natambua kabisa maafisa mbalimbali wa Serikali ni members/wanapita huku JF kama kisima cha habari za uhakika.

Leo napenda kuzungumuzia Kampuni ya Uchimbaji Madini iliyoko Mwanza Capital Drilling (T) LTD na ku-operate katika migodi ya Geita, North Mara, Bulyanhulu na sites ndogo ndani ya nchi yetu.

Hii Kampuni imeajiri wafanyakazi wengi sana kutoka nje "Expats" ambao wanafanya kazi zinaweza kufanywa na Watanzania na kwa ufanisi mkubwa.
Njia wanazotumia kupata vibali vya kazi yaani work and residential permits ni hii hizi;

1. Kwa rushwa, hao jamaa wamekuwa nchini kwa mda mrefu hivyo wanafahamiana na officers wote Mwanza na Geita. Baadhi ya maofisa wa uhamiaji ambao si waminifu ndo hucheza huu mchezo kupata fedha kwa njia ya rushwa na kutoa vibali.

2. Kudanganya utaalamu/taaluma na nafasi zao za kazi (educational level, experience and position/title)
Mfano, utakuta kibali cha mfanyakazi huyu ni Senior drill supervisor lakini achofanya kila siku ni kupaka mashine vilainishi( greasing) au kusambaza mafuta kwenye mitambo na magari ya Kampuni.
Hii yote hufanikiwa kwa kupata ushauri kutoka kwa maofisa wa uhamiaji katika maeneo hayo.

3. Baada ya Serikali ya awamu ya tano kushika madaraka kidogo kutoa hofu kwa kiasi fulani sasa expats wapya hulipia vibali vya mda "Business visa" kama consultant huku ni wafanyakazi wa kawaida yaani waajiriwa wa Kampuni.
Mfano, nafasi za storemen kutoka Zambia x 2 (Mwanza), Misri x 2 (Geita na North Mara)

4. Kampuni hii inamiliki Kampuni tofauti zinazofanya kazi tofouti ambazo ni Welforce International inahusika na gyro survey na Stealth Global Industries inahusika na manunuzi sehemu mbalimbali duniani. Hizi Kampuni hazijasajiliwa nchini hivyo hawalipi kodi yoyote. Wafanyakazi wa hizi Kampuni mbili ni kutoka nje na wanaomba vibali kupitia capital drilling huku wakijua siyo kweli.

Kwa leo naomba niishie hapo wakuu, tukipata mrejesho chanya kutoka Serikalini next time nitaweka wazi majina na vibali vya Wafanyakazi wote kutoka nje wasio hitajika ndani ya nchi kwa nafasi zao. Asante.
SI HIYO TU ATEMBELEE NA POLYSUCS(seasalt) ubungo DSM
 
Back
Top Bottom