Uhalisia wa maisha ya baadhi ya watumishi wa umma, msoto na changamoto zake

Ujinga ni mzigo. Hakuna kitu kibaya kama kujaza ujinga kichwani mwisho wa siku na kujiita Profesa lakini huna hata secondary source of your income. Wasomi wengi ni wajinga sana.

Kama unaona unachokifanya hakikupi manufaa achana nacho fanya mambo mengine. Tatizo la wasomi wengi ni waoga siyo risk takers na ndiyo maana mnazidi kulialia mitandaoni.

Ujinga huo. Kuna kazi nyingi za kufanya mkuu. mshauri huyo profesa afungue genge duka au sehemu ya kuuza chips mtaani kwake. Hakika atakuwa mbali baada ya miaka 5 kuliko kung'ang'ani kitu kinachomtesa katika maisha yake na kumletea umasikini. Kumbuka hakuna mtu aliyekuwa billionaire kupitia mshahara.

Nawashauri waache kulalamika na kulialia mitandaoni ukiwemo na wewe. Chukueni hatua stahiki. Jifunze kuwa wajasiriamali kuliko kutumikishwa mkuu. Na kwa sasa kama ujuavyo ile pensioni ya kustaafu haiotolewi zamani. Hivyo ukistaafu tu lazima ufe kwa msongo wa mawazo kama hukujiandaa vyema.

Hii hoja ndiyo inathibitisha ujinga wa wasomi. Unafikiri kwamba Rais ndiyo atakuletea maisha mazuri? think beyond the box brother.

Mkuu shituka na chukua hatua stahiki. Mbali na hapo utaendelea vivyo hivyo mpaka unastaafu kwa kuchuku salary advance.

Hiyo ndiyo faida ya kuajiriwa mkuu.

Acha ujinga jitume haswa mkuu. Rais au serikali haitakuletea maisha mazuri. Tengeneza vyanzo vingi vya mapato brother.

Una changamoto kwa sababu umekubali kutumikishwa mkuu. Jitathimini upya mkuu. Kama unachokifanya hakikuletei faida yoyote tambua kwamba you are wasting your time.

Kuwa na kitambi tasfiri yake ni kwamba wewe ni masikini wa kutupwa wa akili na mali usiye jali afya yako.

Angalia sasa wasomi wa aina gani tuliyo nao. Unaogopa kuokota makopo kisa elimu? tena Tena elimu yenyewe una digrii ya ualimu. You can't be serious brother. Work & think smart brother.
Naomba niwe kinyume na wewe, ni kweli muda fulani kutokana na hali ilivyo inabidi utafute kitu cha ziada cha kufanya.

Shida inakuja upande wa taaluma yako kamwe huwezi kuitendea haki. Siku zote huwezi tumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.

Sidhani kama nchi zilizoendelea unaweza kuta daktari ana kitu cha ziada kama biashara n.k

Ndo maana basi huduma zao huwa bora, ukija huku elimu mbovu, afya mbovu n.k

Shida inaanzia hapo kwenye maslahi. Maslahi yanakuwa madogo na kufanya watumishi waangalie utaratibu mwingine unaopelekea ufanisi mdogo kwenye taaluma/sekta husika.

Matokeo yake ndo hayo huduma kuwa mbovu.
 
Nimecheka kama mazuri!!

Angalau umetusemea.

Ila mwambie huyo Prof mihogo ya elfu mbili anaweka kwenye tumbo gani?

Mi hiyo buku 2

Nakula mihogo ya jero

Mishakaki 3 Mia Tisa

Na juisi ya miwa jero.

Naburudikaaaaaa
Yeye ana watoto saba. Na wengine international schools wanasoma. Endelea na ubaharia tu sijui familia utaanzisha lini. Kumbuka fimbo ya egemeo uzeeni au taabuni ni familia yaani watoto.
 
Tatizo wapinzani ndiyo wamesababisha yote hayo. Saivi kila Mtumishi wa serikali angekuwa millionaire ila wapinzani ndiyo walikuwa kikwazo.
 
Yeye ana watoto saba. Na wengine international schools wanasoma. Endelea na ubaharia tu sijui familia utaanzisha lini. Kumbuka fimbo ya egemeo uzeeni au taabuni ni familia yaani watoto.

Nani kakwambia kwamba sina familia.
 
Endelea kujitia mjuaji na huku watu wanadai stahiki zao
EndendUjinga ni mzigo. Hakuna kitu kibaya kama kujaza ujinga kichwani mwisho wa siku na kujiita Profesa lakini huna hata secondary source of your income. Wasomi wengi ni wajinga sana.

Kama unaona unachokifanya hakikupi manufaa achana nacho fanya mambo mengine. Tatizo la wasomi wengi ni waoga siyo risk takers na ndiyo maana mnazidi kulialia mitandaoni.

Ujinga huo. Kuna kazi nyingi za kufanya mkuu. mshauri huyo profesa afungue genge duka au sehemu ya kuuza chips mtaani kwake. Hakika atakuwa mbali baada ya miaka 5 kuliko kung'ang'ani kitu kinachomtesa katika maisha yake na kumletea umasikini. Kumbuka hakuna mtu aliyekuwa billionaire kupitia mshahara.

Nawashauri waache kulalamika na kulialia mitandaoni ukiwemo na wewe. Chukueni hatua stahiki. Jifunze kuwa wajasiriamali kuliko kutumikishwa mkuu. Na kwa sasa kama ujuavyo ile pensioni ya kustaafu haiotolewi zamani. Hivyo ukistaafu tu lazima ufe kwa msongo wa mawazo kama hukujiandaa vyema.

Hii hoja ndiyo inathibitisha ujinga wa wasomi. Unafikiri kwamba Rais ndiyo atakuletea maisha mazuri? think beyond the box brother.

Mkuu shituka na chukua hatua stahiki. Mbali na hapo utaendelea vivyo hivyo mpaka unastaafu kwa kuchuku salary advance.

Hiyo ndiyo faida ya kuajiriwa mkuu.

Acha ujinga jitume haswa mkuu. Rais au serikali haitakuletea maisha mazuri. Tengeneza vyanzo vingi vya mapato brother.

Una changamoto kwa sababu umekubali kutumikishwa mkuu. Jitathimini upya mkuu. Kama unachokifanya hakikuletei faida yoyote tambua kwamba you are wasting your time.

Kuwa na kitambi tasfiri yake ni kwamba wewe ni masikini wa kutupwa wa akili na mali usiye jali afya yako.

Angalia sasa wasomi wa aina gani tuliyo nao. Unaogopa kuokota makopo kisa elimu? tena Tena elimu yenyewe una digrii ya ualimu. You can't be serious brother. Work & think smart brother.
 
Wafanyakazi mishara
Kwanza nikiri hii habari sijaiandika mimi, ukweli nimeipata Twitter (kitu pekee nilichoandaa ni kichwa cha habari tu hapo juu)

Sasa tuanze kusoma.

Mheshimiwa Rais, nakusalimia kwa heshima na taadhima, Mimi kijana wako naendelea kulitumikia taifa nikiwa kituo changu cha kazi hapa Mlimani, kuna jamaa wengine wanapaita Jalalani, ingawa silipendi kabisa hili jina.

Kilichonisukuma kukuandikia ni baada ya kukutana na Profesa mmoja akinunua mihogo kwa ajili ya chakula cha mchana, mitaa ya jirani na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Profesa huyo kapandishwa cheo mwaka jana, lakini bado hajaanza kulipwa mshahara wa uprofesa hadi sasa.

Nilipomuuliza kwanini ananunua mihogo ya Sh2,000 akadai kuwa ‘purchasing power’ yake ni kidogo na haijaongezeka tangu uingie madarakani. Nilimkemea kwa niaba yako kwa sababu anakuonea; umekuwa ukipambana kukuza uchumi wa nchi.

Ingawa kiukweli wako wafanyakazi wengi wa kundi lake ambao hadi sasa wanalilia kulipwa mishahara stahiki kwa muda mrefu, lakini hawaoni dalili zozote. Na wengine bado wanasubiri malimbikizo.

Ukiacha maprofesa, wapo manesi, walimu, waganga, mabwana na bibi shamba na mifugo, askari polisi, magereza, uhamiaji, makarani, makatibu muhtasi, wakunga, waganga wa maabara, mafundi umeme, wakufunzi na wahadhiri, na wengine wengine. Orodha ni ndefu, nao kilio chao ni hicho hicho.

Nimekusanya sahihi zao kutoka maeneo mbalimbali ya Tandahimba, Newala, Namtumbo, Madaba, Ludewa, Makete hadi Ileje, Nkasi, Mlele, Buhigwe, Kakonko, Karagwe, Ngara, Busega, Itilima, Mkalama, hadi Rorya. Nilitaka niwakatae jamaa wa kutoka Runzewe, Katoro na Bwanga nikiamini wanaweza kukufikishia wao wenyewe, lakini nikaona si vibaya ngoja niwawakilishe.

Ila mawaziri, makatibu wakuu, majaji, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya hawahusiki na msamaha.

Wafanyakazi wengi uwezo wao wa kufanya manunuzi ni mdogo. Kiasi kilichokuwa kinaingia mwaka 2016 ndo hicho hicho hadi mwaka 2021, wanatamani waone nafuu fulani kwenye uwezo wao wa kuhimili manunuzi kwa ajili ya kuhudumia familia.

Naona kama wenzetu wa Bodi ya Mikopo walinusa hilo mapema . Wao wakaweka kipengele cha ‘value retention fee’ toka 2016 kulinda thamani yao ya hela. Walijua kila mwaka thamani ya hela inashuka kwa asilimia sita na ikifika 2021 hela waliyoweza kumpatia mwanafunzi 2016 itakuwa haitoshi 2021, hivyo wakapachika hicho kijamii kinaitwa ‘value retention fee’.

Ukiacha Bodi ya Mkopo kutukata asilimia 15 ya mkopo, kuna hawa jamaa wa TRA nao naona wameamua kutukomalia zaidi wafanyakazi tuwe na TIN. Wamesema bila TIN mwezi huu wa Januari tunatoka bila bila kwenye akaunti zetu.

Mheshimiwa Rais, naomba nichukue nafasi hii kuzishukuru benki tunazopitishia mishahara yetu. Ingawa wanatengeneza faida, lakini huwa wanatuokoa. Baada ya mshahara kuingia wakakata hela yao waliyonikopesha mwezi uliopita. Nilipochungulia kilichosalia kikawa hakitoshi kunifikisha wiki moja mbele, basi siku hiyo hiyo nikakopa tena ‘salary advance’. Sasa hivi ndo ‘salary advance’ ndio mkombozi wetu.

Mheshimiwa, siyo kwamba tunapenda kuishi hivi, ila majukumu ya kifamilia ni mengi na uwezo wa kuyamudu kwa hiki tunachopokea ni mdogo, maana wakataji ni wengi.

Sitaki kuingia nao ugomvi lakini mishahara yetu inachukuliwa na TRA, HESLB, NHIF, PSSF/NSSF kwa sehemu kubwa.

Mheshimiwa Rais, nisikuchoshe na maneno mengi. Wafanyakazi wenzangu walioko Serikalini wameniomba nije kukuomba radhi, kama wakati wowote tangu ukiwa waziri hadi Rais kuna mahali tulikukosea, tunaomba msamaha. Maisha yetu huku mtaani ni magumu, hatuna furaha, baadhi yetu tuna sura za uzee kumbe bado vijana.

Ndoa zetu sasa hivi ziko hatarini, wake zetu wanatudhania wote tuna tabia za wangoni kumbe shida yetu ni hela. Tuna changamoto nyingi za kifamilia, kijamii na binafsi.

Sasa hivi hata viongozi wa dini tunawaona kama wapiga dili kwa sababu nao hawajui tumesahauliwa kwenye ‘value retention’ ya mishahara yetu, utawasikia wakisema, ‘safari hii tegemeza jimbo ongezeko ni asilimia 40 ya mwaka jana’.

Wakiangalia vitambi vyetu wanajua tuna hela kumbe thamani ya mifuko yetu bado ni ile ile ya mwaka 2016.

Tuonee huruma Mheshimiwa Rais, usishangae asilimia kubwa ya wafanyakazi wa Serikali tukianza kukusanya chupa tupu mtaani na kuzigombania kwenda kuuza. Natumaini wewe ni baba mwenye huruma utasikiliza maombi yetu ya msamaha.

Imeandikwa na Faraja Kristomus, mwandishi anafundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anapatikana kwa simu ya mkononi 0787525396
Proffessor mshahara milioni tano kwa mwezi anakula muhogo wa elfu 2 eti purchasing power ndogo!!!!

Mleta mada kama kweli unafundisha UDSM ajira yako nina mashaka nayo upeo wa uelewa wako uko chini mno
Ulipataje hiyo ajira?
 
Huu ni ubinfsi munajiwaza ninyi kupandishwa mishahara na si wasiokuwana hiyo mishahara waajiriwe nao wapate kipato.

Mihogo ya 2000 kama meal ya mlo mmoja hiyo pesa ni ya milo ya siku mzima ya mtu.
Serikali haiwezi kuajiri watu wote mzee ujiajiri tu usije kuwakataza watumishi wetu wasiongee na serikali iboreshe maslahi yao
 
Mara zote nimekuwa nikisema waziri wa Fedha DR. Mpango na katibu wako walipeni stahili zao watumishi wa umma ili kupunguza changamoto za ukali wa maisha,
walipeni marupirupu yao kwa wakati, walipeni malimbikizo yao ya mishahara kwa wakati ili waweze kujikimu kimaisha, acheni kukalia haki zao, wapeni ili Mungu azidishe baraka ktk Taifa letu.
 
Back
Top Bottom