Saguda47
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 10,788
- 18,696
Wapendwa hamjambo?
Naomba tuangalie hii "jamii" ijulikanayo kama "WASIOJULIKANA"
Kabla ya kwenda mbali tujiulize maswali yafuatayo:-
1. Wasiojulikana ni akina nani?
2.Wanafanya hayo wayafanyayo kwa masilahi ya nani?
3. Nani kiongozi wa wasiojulikana?
4.Je, ni kweli hawajulikani?
Maswali hapo juu yamebaki mafumbo makubwa japo ni maswali rahisi kwani jamii nzima iko kwenye taharuki kubwa baada ya hivi karibuni kuibuka matukio yanayotekelezwa na hao " wasiojulikana".
Katika maana ya haraka, watu Wasiojulikana ni watu ambao jamii nzima haiwatambui au haina taarifa yoyote kuhusu wanakoishi, wanakula wapi, wanapumzika wapi, wanaurafiki na nani n.k.
Kwa mantiki hiyo jamii imebaki katika fumbo kuu mno kuhusu hii dhana ya "wasiojulikana".
Bahati mbaya sana imefika wakati baadhi yetu tumeanza kuzituhumu baadhi ya taasisi na idara zetu za kiulinzi kuwa huenda ndiyo " Wasiojulikana"
Idara zinazohisiwa na wachache wetu ni:-
(a) Idara ya usalama wa Taifa (TISS)
(b) Jeshi la polisi Tanzania (PT)
Taasisi tajwa hapo juu ni moja ya vyombo mhimu sana katika ulinzi wa taifa letu, Pengine kwa kutojua sawia majukumu ya vyombo hivi ndio sababu baadhi yetu tumekaririwa tukisema hadharani wasiojulikana wanatokana na taasisi tajwa hapo juu.
Yafuatayo ni baadhi tu ya matukio yaliyohisiwa kutekelezwa na hawa watu wasiojulikana:-
1.Kutekwa na kuteswa kwa dr. Ulimboka.
2. kupotea kwa Ben Saanane.
3.Jaribio la kumuua Tundu A. Lissu
4.Kutekwa kwa msanii Roma mkatoliki.
5.Kutekwa kwa Mo Dewji
6. Kuchomwa kwa nyaraka za mawakili kule Dar es salaam.
7. kupotea kwa Azory n.k
Wanaovihusisha vyombo ama taasisi hizi za kiulinzi wanasahau matukio yafuatayo:-
1. Matukio ya mauaji huko kibiti
Takribani raia na polisi wapatao 40 waliuliwa huko Kibiti na watu ambao walikuwa hawajulikani,
2. Mauaji ya Amboni- Tanga
3. Uhalifu na uporaji katika maeneo tofauti ya nchi yetu,
Licha ya mengi yanayotokea, jamii inapaswa kujua kuwa, wasiojukana ni coverbed tu ya magenge ya kihuni na kihalifu yenye lengo la kuleta taharuki katika jamii ya Kitanzania na kuvichafua vyombo vyetu hasa TISS.
Utekaji wa raia na mauaji holela ni kiashiria kikuu cha upotevu wa amani katika taifa lolote lile duniani. Je, tumefikia huko hata sisi?
La hasha! imani yetu iko katika vyombo vyetu vyote vya ulinzi na usalama, ambavyo kikatiba ndio "Coercive instruments" of our state. Jamii inapaswa kufahamu kuwa, Ukatili ( sadism) wowote unaofanywa na mtu, taasisi au kundi fulani ni hatia kama hatia zingine za kijinai bila kuangalia mtu huyo katokea taasisi gani au kundi gani la kijamii, hii itaondoa uoga usithibitika ( fear of unknown) baina ya wanajamii na kuondoa dhana kuwa wasiojulikana ni taasisi imara inayopewa nguvu na baraka kutoka "JUU".
Wahalifu hupata nguvu wanapotenda tukio na kuiacha jamii ikifarakana kwa kuishutumu serikali kwani huendelea kufanya mambo yao undercover ambapo ni ngumu kufahamu nani ndio mhalifu.
Tuipende Nchi yetu, Tusikubali kukata tamaa kwa kuamini mambo yasiyo na uthibitisho wowote wa kisheria.
Tuibue uhalifu popote ili kuzisaidia taasisi zetu za kiulinzi kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha.
Mjadala uko wazi.