Uhalali wa uraia wa Mhe. Moudline Castico BLW

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
Si jambo la kuficha kuwa Moudline Castico ni Mzambia wa kuzaliwa na wa kukulia. Kuhamia kwake Tanzania kumetokana na kumfuata mumewe Joseph Castico.

Alijipenyeza kufikia cheo cha juu kwenye chama CCM ( chama kinachowabeba wakuja) na umaarufu wake kuzidi kuenea mpaka pale alipojikwaa dole na kuangukia kwenye kundi la wanaodai haki zaidi ya wazanzibari.

Wakati huo Mwl. Nyerere alikuwa bado yuko hai na kuonekana waziwazi kukerwa na kauli zake , alikiamuru chama kimvue madaraka na moja ya sababu zilizotolewa kuwa alikuwa si mwanachama halali wa CCM kwa vile alikuwa si raia wa Tanzania. Yeye ni Mzambia.

Tunajinabu na kujinasibu kuwa tunafuata nyayo za hayati baba wa Taifa , hivi ni nani aliothubutu kufuta uamuzi wa Nyerere na kuuhalalisha tena uraia wake? Au kwa vile anatoka chama tawala CCM?

Nimeshtushwa kusikia sasa ameteuliwa kuwa mjumbe wa BLW, hii ina maana kuwa anaweza pia kuteuliwa kuwa Waziri na baadae hata kugombania urais! Ni hatari

Zanzibar inavurugwa vipandevipande; imeanza kutawaliwa na Mmalawi Akaja....... na sasa inaelekea itakwenda kwa Zambia

Nielewesheni wana bodi
 
Kuna uraia wa aina nyingi inawezekana aliisha omba uraia siku nyingi na akawa raia halali cha jaribu kufanya kazi achana na kuchunguza maisha ya watu.
 
Kama ameomba uraia na kukubaliwa kuwa RAIA halali basi anastahili kuwepo kwenye nafasi yeyote kwa sababu ni Mtanzania kamili sasa.
 
Kunyang'anywa kwake uraia kumetokea More tahan 16yrs ago kwa hivyo una ushahidi gani kama hajaomba uraia?

Kwa hivyo kama tayari ni raia wa Tz ana haki zote za msingi. lakini kuwa Rais wa Zanzibar hilo haliwezekani... Kama ataweza kupindua au kubadilisha kipengele cha katiba hiyo itawezekana..

Hivi unajua Mzanzibari yeyote ni anaweza kuwa Raisi wa Tanzania lakini sio kila mtanzania anaweza kuwa raisi wa Zanzibar
 
Kuna uraia wa aina nyingi inawezekana aliisha omba uraia siku nyingi na akawa raia halali cha jaribu kufanya kazi achana na kuchunguza maisha ya watu.
lazima tuchunguze wazanzibari tumechoka kutawaliwa na wakuja. Inashangaza kuwa kama ingekuwa Tanzania bara ingelikuwa issue, Watanzania wa kuzaliwa akina Jenerali Ulimwengu uraia wake ulipingwa, Shekh Ponda nae akaambiwa si mtanzania, ni sisi tu wazanzibari tusiwe na haki ya kuhoji, uraia tena hata wa kujiandikisha?
 
Kama ameomba uraia na kukubaliwa kuwa RAIA halali basi anastahili kuwepo kwenye nafasi yeyote kwa sababu ni Mtanzania kamili sasa.
Na unamjua mzanzibari ni nani? Unaju pia mzanzibari wa kuandikishwa hawezi kushika wadhifa wa uongozi na kutawala Zanzibar?
 
Nashauri hili suala lipeleke uhamiaji kama hutaridhika na majibu yao nenda mahakamani. Hapa hakuna mwenye majibu mkuu.
 
Naombeni kueleweshwa; hivi mtu aliyeomba uraia anaruhusiwa kua kiongozi kwenye ngazi kubwa kama ya uwaziri? Sheria zetu zinasemaje?
 
CUF si hawalitambui balaza la wawakilishi,kwa madai uchaguzi wa march 20 ulikuwa haram,kwahiyo kila kinachofanyika kuhusu serikali ya Zanzibar,rais wao Shein na wawakilishi wao ni haram.
Kwahiyo hakuna haja ya kujadili haram.
 
Ya Zanzibar anayajuwa Ali Karume na wanamapinduzi wenzake wao wanaishi mwaka 47.
 
lazima tuchunguze wazanzibari tumechoka kutawaliwa na wakuja. Inashangaza kuwa kama ingekuwa Tanzania bara ingelikuwa issue, Watanzania wa kuzaliwa akina Jenerali Ulimwengu uraia wake ulipingwa, Shekh Ponda nae akaambiwa si mtanzania, ni sisi tu wazanzibari tusiwe na haki ya kuhoji, uraia tena hata wa kujiandikisha?
nauliza wazanzibari asili yao ni wapi?
 
Back
Top Bottom