yoga
JF-Expert Member
- Jan 6, 2013
- 1,820
- 8,477
Mwanzo wakati zoezi la uhakiki wa watumishi wa uma linaanza nilidhani serikali inayo nia njema ya kuboresha kadhia ya utumishi! Nilidhani serikali ina nia ya kupunguza matumizi na kuwaondoa wàtumishi hewa na kubakiza wale halali na fedha inayobaki au kurudishwa kupelekwa kwenye miradi mbali mbali au huduma za kijamii.
Zoezi mpka sasa limefanyika mara nne, kufanyika kwa zoezi hili kulisababisha mambo makuu manne muhimu kwa watumishi kutokufanyika.
1. Kusitishwa kwa ajira mpya serikalini
2. kusitishwa kwa annual incriment ya mtumishi ya kila mwaka
3. Kusitishwa kwa promotion za watumishi
4. Kusitishwa kwa uhamisho wa watumishi
Toka mwaka 2015 mtumishi wa nchi hii analipwa kiwango kile kile cha mshahara kinyume na mkataba wake wa ajira na sheria za utumishi na ajira za nchi hii.
Kuna watumishi wa aina mbili kwa mtazamo wangu, kuna watumishi wenye vipato vikubwa (wasimamizi) mfano wakuu wa idara mbali mbali kama Maafisa elimu, Afisa ardhi, Wakurugenzi, na nk. hawa mishahara yao inaanzia milioni 2.5 nakuendelea.
Wapo watumishi wenye vipato vya chini, mfano waalimu, wauguzi, na nk hawa vipato vyao vinaanzia laki 7 na 60 kushuka chini bila makato yoyote!! Mfano mwalimu mwenye degree mshahara wake ni 760,000/= ukiondoa makato yake ambayo ni bima, kodi, loan bord, Cwt, anabaki na laki 5 na 20 elfu!! Kama sijakosea kwa mwezi.
Uhakiki huu sasa megeuka chaka la serikali kukwepa kupandisha madaraja ya watumishi, kuwaongezea annual incriment yao ya kila mwaka na hata kuwanyima uhamisho ambao wengi wanajigharamikia.
Umefanya wawe watu wa stress, maisha kuwa magumu zaid hasa baada yakuongezewa makato makubwa kwenye mishahara yao!! Kunawatu wanasema au wanapenda kuwaambia "acheni kazi kama mnaona mambo ni magumu"
Hiyo nikauli ya ajabu kuwai kusikika, hembu tuulizane kwa maisha ya sasa unaweza kulipa nyumba, ulipe umeme, ununue maji, ununue chakula, ulipe usafiri upeleke watoto shule kwa salary ya 520,000/ ?
Uhakiki huu sasa umekua kero, napata taarifa umeanza tena mwezi huu, na sasa wanataka barua ya ajira, kitambulisho cha NIDA na vyeti vya shule! Honestly kweli mpaka leo tunafanya uhakiki?
Huu utakua uhakiki wa mara ya tano! Hivi serikali mpaka leo hamjajithibitisha mnao watumishi wangapi halali mpaka sasa? Toka mwaka jana mpaka leo?
Au kwakua imefika mwezi wa saba na mliwaahidi kuwapandisha madaraja na kuwalipa stahiki zao mnaona haiwezekani mmeamua kurudia chaka lenu?
Hembu waoneeni huruma hawa watu, ifike mahala muone aibu na muache kuwa sumbua si makosa yao, ni makosa ya Maofisa Utumishi na Wakurugenzi wenu wa halmashuri kuandaaa data za uongo kuhusu ajira za watumishi.
ifike mahala sasa tuone aibu nibora kuwaeleza watu kuwa tumeshindwa tuvumiliane kuliko kuwa sumbua hivi!! Mnawanyanyasa kwa sababu mnajua hawana way out na wanao umia ni hawa watumishi wa chini.
Kweli ule msemo wa salary is bribe paid at the end of the month to blind your dreams ni wa kweli sana.