Napenda kupongeza na kuunga mkono juhudi za serikali kuhakiki vyeti feki. Ni kazi kubwa na nzuri sana imefanyika sasa naomba basi upanuliwe wigo wa uhakiki. Naipongeza sana serikali ya JPM lakini ili kulimaliza tatizo hili kabisa kabisa panua wigo. Fanya uhakiki hata huko sekta binafsi vitakuwepo vingi zaidi tena ya vilivyopo serikalini. Kama serikali inaowatumishi wachache ukilinganisha na sekta binafsi na imepata watu wengi hivyo je uwiano utakuwaje kwa sekta binafsi? Tena ningetamani hili lifanyike kabla hata ya kuajiri huko serikalini maana inawezekana mkaja kuajiri wengine feki kutoka sekta binafsi.
Aidha pia uhakiki huu uende hata kwenye taasisi zote za elimu ili kama wapo pia wanafunzi ambao wanavyeti feki nao waondolewe sasa mapema.
Lakini pia itengenezwe blacklist database yawekwe majina ya wote wenye vyeti feki au wanaotumia cheti kimoja watu wengi ili mwajiri yeyote akishapata wafanyakazi kabla ya kuwaajiri anajiridhisha kutoka kwenye database.
NAUNGA MKONO UHAKIKI NA NIMEPENDA SANA KAZI NZURI, CHAPA KAZI