Click Hapa
JF-Expert Member
- Jan 27, 2013
- 479
- 206
Wewe KIBE! ishu ya kugoma gesi kugomewa na wanamtwara haikuanza jana ni muda wabunge wa upinzani kwa muda mrefu walipigia kelele bungeni kuhusu mgawanyo wa mapato, mwaka jana wananchi wa mtwara waliandamana sana kupinga, hadi baadhi wakaja ikulu ya dar, na kama utakumbuka vizuri kuna BIBI alilaani kwamba wakichimba tu bomba litatowa maji na sio gesi........., akatumwa mn'goa kucha mmoja kwa bibi wananchi wakamshtukia nusura auwawe akakimbia gari lake likachomwa moto. wananchi wa mtwara wakaendelea kuwa na msimamo kwamba gesi haitoki..kwa hiyo yanayofanyika ni ya wanamtwara wenyewe na sio msukumo toka nje.
1. Silaha za wananchi ni mabomu ya uvuvi,mishale na mapanga ambayo yapo kila siku,miaka yote hayajaagizwa kutoka nje ya nchi.
2. Hivi wewe unataka kuniambia mwananchi akidai haki zake eti "katumwa na wachochezi'' kana kwamba yeye hana akili timamu.......unataka kutuambia hata wazee wetu wapigania uhuru waliambiwa na watu wa nje kwamba nchi zetu zilikuwa zinanyonywa na wakoloni.
3. Hata kama makosa yalifanyika nyuma kwa mikoa ya tabora,shy,mza,mara (migodi ya dhahabu na almasi) sio lazima turudie mtwara.
4. Ingekuwa Mza,A-town,Dar,Moshi serikali ya CCM ingekuja na jibu rahisi kwamba CDM inachochea, ingekuwa Zenj CUF wangetuhumiwa, Sasa mtwara tunadanganya ''mkono wa nje"
5. Wewe kama Mtz em pita vijiwe vya watu wa kawaida Kariakoo,manzese,tandale,Tmk,Kndoni,Mza,Arusha,Musoma,Bk jaribu kuuliza au kusikiliza maoni ya wananchi ndio uende kuwaambia wakuu wako pale lumumba.
6. Tunataka masahihisho yaanzie mtwara, mji ufanane kama miji maarufu ya uchimbaji wa madini kule africa kusini tusirudie makosa ya mwanza,Shy,Tbr,Mara nk.
7. Unaposema mtwara ni mbali, unamaanisha mbali na wapi? kwasababu wanaihitaji gesi watalipia gharama za usafiri kuifuata sababu ni adimu.
8. Eti Mtwara hamna wataalamu ni uongo, Nchi yetu haina wataalamu ndio kwanza wameenda shule.......kama hiyo ni sababu bomba lingejengwa kumwaga gesi urusi ndio kuna wataalam.
9. Wasomi wote wako Dar sababu ya ajira na asilimia zaidi ya 90% si wazawa wa Dar, ni matumaini yangu kwamba hata bomba lingekuwa mtwara bado wasomi wangelifuata mtwara kupata ajira nzuri, mbona migodi ya dhahabu haijahamishwa Tbr,Shy nk lakini vijana wasomi kibao wanakimbilia huko kupata ajira nono.
Kwahiyo ni vema kukaa chini na kuja na suluhisho la juu juu, kwa sasa serikali ya CCM haiwezi kudanganya watu, sababu watu wamekufa kahama,mererani,tarime kwa manufaa ya viongozi walafi pasipo hata manufaa kwa mwananchi. Pia wananchi wakipinga usiuite uhaini, tatizo lako na CCM hamjui kwamba hata Polisi na JWTZ ni watanzania na hawafurahishwi dhuluma kwa wananchi...................
Ntunga: Umenena mambo ya msingi kwa yeyote mwenye upeo na nia ya kuelewa.
Serikali yetu kwa sasa imekuwa na tabia ya kuwa na majibu mepesi kwenye maswali magumu, viongozi wetu wa serikali wamekuwa wavivu wa kufikiri na kutafuta suruhu ya hoja zilizo nzito kama hili suala la Mtwara sasa, bila kufikiri kwa umakini wanakurupuka na kuanza kulihusisha suala hili na siasa na hasa wakikinyooshea kidole CDM, mimi nasema huu ni uvivu wa kufikiri na kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu.
Mwl Nyerere aliweza kuiongoza na kuiunganisha nchi hii kwa sababu hakuwa mvivu wa kufikiri na hakuwa na majibu mepesi kwa maswali magumu, mkikumbuka vita ya Uganda (Amin) wakati wa Mwl. wanachi waliweza kuwa mstali wa mbele kupambana na Nduli Id Amin, watu walijitolea kwa hali na mali zao, enzi za Mwl aliposema siasa ni kilimo watu walikwenda mashambani, wananchi walifurahia kusikiliza hotuba za Mwl radioni nyakati zile watu walikuwa na shahuku ya kujua leo Mwl ataongea nini.
Mambo haya hayakuja tu hivi hivi, Mwl alikuwa na tabia ya kuwa pamoja na wanachi kwenye shida zao, alikuwa tayari kuwaelekeza wananchi kupenda kufanya kazi (kujitegemea), aliwaeleza wananchi wachukie aina yoyote ya udharimu, unyonyaji, wizi, rushwa, ufisadi na kila aina ya jambo lolote lisilo sawa. Mwl alipenda wananchi waelimike wawe na uelewa wa mambo.
Mwl hakuwaonea aibu wale wote watumishi wa serikali waliotumia madaraka yao vibaya (kujinufaisha)
Azimio la Arusha lilikuwa na maana yake, Mwl kafa akilililia, hakuwahi kujua ni kwa nini viongozi wetu walilifuta
Kwa kufanya hivyo wananchi waliipenda nchi/serikali yao na chama chao.
Tukubali tusikubali, CDM kwa sasa ndo wenye uwezo wa kuwajenga Watanzania, Watanzania wa leo kwenye mikutano ya CDM tumeona kwa roho nyeupe kabisa, kwa utashi, pamoja na ugumu wa hali kifedha, lakini wamekuwa wakichangia hizo hizo kidogo kidogo kujenga CHAMA (M4C), wengine wamekuwa wakibeza suala hili, ila lina maana kubwa sana kwa wananchi.
Leo hii kwa serikali hii haya yote hayapo tena (hivi utawaelezaje wananchi kilimo kwanza wakati wewe hulimi, unaiba tu fedha za umma) na viongozi wa serikali yetu hawana namna tena ya kuyatafakari haya (wamekuwa wavivu wa kufikiri), wamebakiwa kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu. Kila linalotokea wanadai ni siasa (suala la kuchinja wanasema ni siasa CDM, viongozi wa dini kushambuliwa wanasema siasa CDM, waandishi wa habari kushambuliwa wanasema siasa CDM, shambulio la Arusha wanasema siasa CDM, kila kitu ni CDM, hata leo hii tamko la serikali Bungeni (Nchimbi) kwa wenye kuelewa wameelewa kuwa alikuwa analenga CDM, haya ni majibu mepesi kwenye maswali magumu)
Kwani ufuaji wa hiyo Gesi ukifanyika hukohuko Mtwara kuna tatizo gani??????? Wanamtwara wanataka kwao huko ambapo Serikali imepaacha siku nyingi kimaendeleo nao wapate hivyo vyanzo vya ajira, mambo yajengwe huko huko. Wanamtwara hawajasema gesi iwanufaishe wao tu, hapana wanataka mambo yajengwe huko kwao, pawe na maendeleo.
Hivi kwa nini kila kitu iwe ni Dar tu??????? (au basi serikali iwe wazi tu tabia hizi za 10% kwenye mikataba ndo inawaletea shida, kwamba kuna kampuni ambayo tayari wameshakula 10% ya mkataba wa ujenzi wa Bomba Mtwara - Dar hivyo wanaona noma kuvunja mkataba huo, lakini kwa nini waingie makubaliano ya kusafirisha gesi kutoka Mtwara - Dar bila kwanza kuwashirikisha Wanamtwara????, hii ni tabia iliyojengeke ya kutowashirikisha wananchi kwenye maamuzi, ni jambo baya mno na gharama yake ni kubwa)
Serikali yetu ifikie sehemu iache kuwa wavivu wa kufikiri.
Suala la Mtwara ni jepesi sana ila Serikali imeamua kulikuza na sasa limekuwa kubwa sana.
Serikali ijenge mtambo wa kufua hiyo gesi hukohuko Mtwara, na mengine yote yaanzie huko na kuelekezwa kwingineko.
Kwa lazima kila kitu kiwe ni Dar tu???????