Uhaba wa vitanda Kagera wajawazito walala chini

Uhaba wa vitanda Kagera wajawazito walala chini

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322

Wajawazito katika Wilaya ya Kyerwa, Kagera wameeleza changamoto kubwa wanayokumbana nayo wanapohudhuria katika moja ya Kituo cha Afya Nkwenda kwa kulala sakafuni kutokana na uchakavu na ukosefu wa vitanda.

Kupitia changamoto hiyo serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imetoa msaada wa malazi katika kituo hicho kwa ajili ya kuwapunguzia changamoto zinazowakabili.

Akikabidhi msaada huo mbunge wa jimbo hilo Innocent Bilakwate,amesema kuwa serikali imetoa vitanda 20,magodoro 20 na mashuka 50,na kuwasihi walengwa kuvitumia kwa umakini ili viweze kudumu ikiwa ni njia mojawapo ya kupunguza changamoto ya malazi katika kituo hicho.

Muungwana
 
Kuna haja ya kufanya kampeni kama ya madawati kwani ni hatua muhimu ya kiumbe kiukuaji
 
Bado tunalipana posho za laki 4 kwanza
 
Back
Top Bottom