UHABA WA SUKARI: Serikali mkoani Kagera yasitisha uuzwaji wa sukari kwa bei ya jumla

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Serikali mkoani Kagera imesitisha uuzwaji wa sukari kwa biashara ya jumla, badala yake imetenga maduka maalumu kwa kila kata yatakayohusika kuwauzia wananchi sukari kwa bei elekezi ya Serikali,lengo likiwa ni kuondoa uhaba wa sukari na kuwaondolea kero wananchi.

Kwa mujibu wa Afisa Biashara mkoani hapa Isaya Tendega,uamuzi huo umefikiwa mara baada ya kubaini kuwa wapo baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya jumla wanaotumia changamoto ya upungufu wa sukari na kuiuza kwa bei ya juu tofauti na bei iliyoelekezwa na Serikali.

Tendega amesema kuwa hali ya Sukari iliyoko katika kiwanda cha kuzalisha Sukari cha Kagera ni yakutoshereza kwa wananchi wa mkoa wa Kagera,ingawa changamoto ya kuwepo uhaba wa Sukari inachangiwa kwa kiwango kikubwa kwa Wafanyabiashara kutoka nje ya mkoa kufika Bukoba kuchukua Sukari kwa bei yeyote wanayoitaka wao na kuufanya mkoa kukabiliwa na changamoto hiyo.

Amesema maduka maalumu husika yatakuwa yakisimamiwa na halmashauri za wilaya na Manispaa,hivyo kuwaomba wananchi wa mkoa wa Kagera,kuwa na uvumilivu kwa hatua ya utekelezaji huo inaendelea na kufikia Mei 2(Jumatatu)huduma ya maduka hayo itakuwa imeanza kuwahudumia wananchi.

Uhaba wa Sukari mkoani Kagera imekuwa changamoto kwa wananchi,hali inayosababisha wauzaji wa jumla kuuza sukari kwa bei ya 125,000/ huku bei ya rejareja ikiuzwa kati ya shilingi 2,400 hadi 2600/=huku lawama nyingi zikielekezwa kwa Serikali.
 
Hiyo nzuri sana. Ifanyike kwa mikoa yote. Hivi viwanda vya sukari viwe na maghala ya kuhifadhi sukari yao wenyewe, na kuanzia hapo maduka teule yachukulie sukari hapo.
 
Hali ni mbaya,tumerudi enzi zile nchi ilipotoka vita vya Uganda,bidhaa adimu,hivi kweli tutafika? Na hapa hata Mwaka bado wananchi wanaisoma namba kwa kunywa uji wa chumvi,ila wakome,na wao wanatumbuka kwa staili hiyo,sukari ifike hata elfu kumi kwa kilo
 
i'm having Deja Vu...tunarudi enzi za Nyereree, ila kama ndio itaboresha maisha ya wa tanzania poa
 
Wamezuia uingizaji wa mchele kinachofuata ni kuwa na maduka teule ya kuuza mchele
Upuuzi mtupu
 
Serikali ya Nyerere ilikuwa na haki ya kufanya makosa kama haya kwakuwa ndio mara ya kwanza watu wanajifunza kuongoza serikali, sasa hii ya Magufuli sijui tuielezeje. Kuna kila dalili ya ujinga wa mtu mmoja kwenye hii serikali kulazimishwa kuwa ujinga wa kitaifa. Magufuli constitutes majority of one in this government.
 
Hata hayo maduka yatakayopewa Sukari yatakuwa ya watu wale wale wajanja waliotoka mikoa jirani maana pesa hazishindwi chochote,ngoja tuone pili kiwanda kinatakiwa kutangaza bei elekezi ili wananchi waijue
 
Hii ni sawa na kupoteza hela chumbani mwako na kuamua kwenda kuitafutia chini ya taa za barabarani kwa kuwa kuna mwanga mkubwa wa taa.

Kosa lilikuwa ni kupiga marufuku uingizaji wa sukari huku tukijua (au hatukujua!?) kwamba viwanda vyetu ni chakavu mno na havina uwezo wa kukidhi mahitaji
 
Msikilize huyo mwingine waliemkamata na kumuacha akielezea costs zake binafsi na kwanini wengine tunasema hawa jamaa wazalishaji wana strategy mbovu in the first place kufikia malengo ya serikari na tatizo moja wapo lazima wawekeze kwenye distribution centres za sukari kama lengo kuweka standard prices.
 
Hii ni sawa na kupoteza hela chumbani mwako na kuamua kwenda kuitafutia chini ya taa za barabarani kwa kuwa kuna mwanga mkubwa wa taa.

Kosa lilikuwa ni kupiga marufuku uingizaji wa sukari huku tukijua (au hatukujua!?) kwamba viwanda vyetu ni chakavu mno na havina uwezo wa kukidhi mahitaji

We ni jipu la kwenye makalio, hakuna tatizo la wingi wa sukari, tatizo ni hujuma, sukari imefichwa thats it.
 
Upuuzi mtupu. Hatuwezi kufika kokote kwa utaratibu huo. Utaratibu wa namna hiyo uliishinda serikali enzi za kiongozi jasiri kabisa Sokoine.

Tena serikali iangalie sana. Kwa kadiri inavyozidi kuwabana zaidi wauzaji ndivyo hali itakavyokuwa mbaya zaidi.
 
kwahiyo tunarudi kwenye maduka ya ushirika!!!! hivi hii nchi ina watu wenye akili timamu kweli??
 
We ni jipu la kwenye makalio, hakuna tatizo la wingi wa sukari, tatizo ni hujuma, sukari imefichwa thats it.
Really? Serikali imeagiza tani 11,000 za Sukari kujaribu kupambana na uhaba wa sukari. Huku nyumbu wanaimba kwamba hakuna uhaba wa sukari.
 
Back
Top Bottom