Ugunduzi 2020: Ili abiria wasife katika ajali ya ndege basi watengeneze viti vya kufyatuka kama marubani wa ndege vita

FrankLutazamba

JF-Expert Member
Aug 9, 2018
449
408
Nimeliwaza wazo hili kwa kina na kuona kuwa ikiwa ndege vita marubani hupona itokeapo ajali kwa kufyatuka na kiti basi ni possible ndege za abiria kuwa na mfumo huo ila wazingatie mwavuli uwe na uwezo wa kuelea katika maji.na pia wapitishe watumishi wa ndege codes maalumu kabla ya kufyatua ikiwa ndege IPO hatarini. Pia kila kiti kifungwe GPRS. Boeing lifanyieni kazi.
 
Wasiwasi wangu altitude ambayo ndege ya abiria inasafiri mara nyng inakuwa juu la tabaka la kawaida la hewa.. afu pili itabid dunian wote tufundishwe matumizi ya parachute kabla ya kupanda ndege mkuu...usidhan wanavuta tu kama kwny movie
 
Hapa tunalenga sana ndege za ndani ya nchi(Anga ya kitaifa na si kimataifa)mfano 11 September watu wangepona kwani ndege zilikuwa futi chache toka ardhini kama ghorofa ya sabini tu kumbuka world trade center ilikuwa na ghorofa 110 na ndege nyingi hupata itilafu zinapopaa au kutua.rejea kuwaka moto kulipoanzia mkiani huko uturuki ktk ndege moja.
 
Mkuu ni wazo zuri. Baada ya hizo siti kutengenezwa ziwekewe na mitungi yake ya hewa ya oxygen na makoti ya baridi maana kwa umbali ambazo hizi ndege zinafika kitakachowaua watu baada ya kutoka ni upepo mkali, kushindwa kuvuta hewa, na usalama wa eneo watakaloshukia. Kwa mfano watu wengi sana wangepona kwenye titanic na wengi waliokolewa ila mazingira ya baridi ndio kilichowaua wengi.
 
Nimeliwaza wazo hili kwa kina na kuona kuwa ikiwa ndege vita marubani hupona itokeapo ajali kwa kufyatuka na kiti basi ni possible ndege za abiria kuwa na mfumo huo ila wazingatie mwavuli uwe na uwezo wa kuelea katika maji.na pia wapitishe watumishi wa ndege codes maalumu kabla ya kufyatua ikiwa ndege IPO hatarini. Pia kila kiti kifungwe GPRS. Boeing lifanyieni kazi.
Watakusikia maana tuko nao humu ndani ya chungu
 
Ni gharama kubwa sana kile kiti kinafyatuliwa na mtambo hakijifyatui chenyewe .Kila kiti kuwekewa mtambo wa kufyatua ni gharama na itachukua space kubwa mno kati ya kiti na kiti kingine na ndege itakuwa na uzito mkubwa mno sababu ya hiyo mitambo ya ufyatua viti
 
Watengeneza ndege waliliona Hilo kabla hujazaliwa.
1. Ndege za kivita Mara nyingi zina operate nchi kavu na huwa na mtu mmoja au wawili. Sasa midege mingine Ina watu zaidi ya Mia tano halafu Ina gorofa. Wale wa floor ya chini itakuaje.
2. Hizi ndege hua zina pita juu ya bahari kubwa sasa hitilafu ikitokea huko Kati Kati ya Atlantic itakuaje.
3. Jiulize kwanini air Force one ndege inayombeba abiria muhimu kuliko wote duniani haina hivyo viti wakati ikulu ya marekani Ina bajeti ya kumwaga?
 
Ni gharama kubwa sana kile kiti kinafyatuliwa na mtambo hakijifystui chenyewe .Kila kiti kuwekewa mtambo wa kufyatua ni gharama na itachukua space kubwa mno kati ya kiti na kiti kingine na ndege itakuwa na uzito mkubwa mno sababu ya hiyo mitambo ya ufyatua viti
Wazo limtolewa, lifikishwe mahali husika, wataalam walifanyie kazi, mwenye wazo afaidike nalo. Wacha kuleta mawazo ya kujikatisha tamaa na mawazo ya kimasikini
 
Wazo limtolewa, lifikishwe mahali husika, wataalam walifanyie kazi, mwenye wazo afaidike nalo. Wacha kuleta mawazo ya kujikatisha tamaa na mawazo ya kimasikini
sikatishi tamaa ndege za jeshi mtambo wa kufyatua kiti uko nyuma Wazo lake sio jipya
 
Back
Top Bottom