Ugumu wa mwaka 2011 kuanza mapema?

mzambia

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
885
60
Wenye mabasi wataka nauli zipande Send to a friend Saturday, 01 January 2011 11:39 Burhani Yakub,Tanga

UMOJA wa Wamiliki wa Mabasi wa Mkoa wa Tanga (Taboa) na Muungano wa
Wamiliki wa Dadadla Jijini Tanga (Muwata), wametoa mapendekezo ya kupandisha nauli za daladala kutoka Sh 400 za sasa hadi kufikia Sh 700 kwa safari za ndani ya Jiji.

Pia wamependekeza nauli za mabasi kutoka Tanga kwenda Dar es
Salaam, ziwe Sh13,095 kwa mabasi ya kawaida Sh 18,510 kwa mabasi ya daraja la nusu starehe na 20,700 mabasi yenye starehe kamili..

Mapendekezo hayo yalitangazwa juzi na Makatibu wa Taboa na Muwata kwa uongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini (Sumatra) katika
mkutano wa wadau wa usafirishaji.

Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Akiwasilisha mapendekezo hayo, Kaimu Mwenyekiti wa Muwata, Hatwabi Shaaban, alisema hatua hiyo inatokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji.

Alisema bei za mafuta ya kuendeshea magari na vipuri, zimepanda kwa kiwango kikubwa na hivyo kuwafanya wamiliki wa mabasi kuendesha biashara kwa hasara.

Alisema inapendekezwa kuwa nauli za daladala zinazoanzia Sahare, Mikanjuni, Donge na Magomeni
kwenda Raskazone zipande kutoka Sh300 hadi kufikia Sh 400 na yale ya kutoka Kichangani hadi Kituo Kikuu cha Mabasi, ziwe Sh 600.

Alisema nauli za mabasi kutoka Pongwe zinapendekezwa kuwa Sh 700.

Kwa upande wake, Katibu wa Taboa, Juma Tarimo alisema mapendekezo ya nauli za kutoka Tanga kwenda mikoani na wilayani ni ya ongezeko la asilimia
34

Aliiomba Sumatra kukubali mapendekezo hayo ili kuwawezesha wenye mabasi kutoa huduma bora kwa wateja.

Hata hivyo, mapendekezo hayo yalipingwa vikali na wawakilishi wa
wasafirishwaji, ambao waliiomba Sumatra isikubaliane na wasafirishaji
hao kwa maelezo kuwa wanataka kuwaumiza wakazi wa Tanga ambao kipato chao ni
kidogo, ikilinganishwa na mikoa mingine nchini.

Wawakilsihi hao walisema si kweli kwamba gharama za uendeshaji
zimepanda kiasi cha kuwafanya wasafirishaji, kutaka kupandisha nauli kwa viwango hivyo.

"Sijui kwanini wasafirishaji kila siku wanawaona watu wa Tanga ni wa kuwaburuza kiasi wanachotaka wao, hili sisi hatukubaliani
nalo, haiwezekani wapandishe nauli kiasi hicho,"alisema Mariam Siafu mwakilishi wa wasafirishwaji wa Mkoa wa Tanga kupitia Sumatra.


SOSI: MWANANCHI
 
huu ndio muda muafaka kwa watanzania kuamua maamuzi ya hatari ili kuinusuru nchi,otherwise watanganyika watanyonywa na kuujutia utanganyika wao hata zaidi ya ukoloni.
 
Na bado bati, cement, bia, soda, viberiti,mafuta vyote vitapanda bei

usisahau dada poa nao watapandisha bei ya huduma maana matumizi ya kujitunza yatakuwa yamepanda mweeeee!!!!!
 
Back
Top Bottom