Ni posti ya zamani, lakini si mbaya kuchangia!
Kubwa kwanza la kueleweka ni kuwa 'scholarships' si utapeli ama wizi kama tunavyotaka wengine wafahamu. Jambo lingine la kufahamu ni kuwa hakuna sehemu yeyote ambayo usipokuwa makini utajikuta unadondokea kwa 'wajuaji' na kulizwa. na hivyo ndivyo kwenye utafutaji wa 'scholarships'. Ukiona umelizwa kwenye kutafuta 'scholarships' ni heri ufute mawazo ya kusoma nje kwa 'scholarships', maana ni wazi unakuwa umedhihirisha kuwa utashi wako ni mdogo sana. 'Scholarships' zipo nyingi sana ambazo zinakuhitaji wewe mwenyewe kusoma maelezo na kutuma maombi. Unapotapeliwa maana yake hata kujishughulisha kuzisoma hutaki, unataka umuwachie mtu mwingine akufanyie kazi, hapo ndipo matepeli wanawatafuna.
Lakini jambo lingine, ni kweli 'scholarships' zinapatikana kwa ushindani sana, hasa miaka ya hivi sasa ukilinganisha na zamani. Hii lakini haimaniishi kuwa kuzipata ni bahati, si kweli, bali ni namna vile unavyoweza weka makarabrasha yako ama kutumia vyema usaili unaofanyiwa kuwashinda wengine. Na hapa pia ndipo Wabongo tunachemka, sisi mara nyingi mawazo ya kusoma nje kwa 'scholarships' yanatujia tunapokumbwa na kitu (mf. kazini hakuendi vyema, unasema nitafute tu shule nje niende; kuna rafiki yako umemtamania nawe unakuja tu na wazo la harakaharaka na mimi niende nje). Hii si rahisi kupata 'scholarships'. Upatikanaji wa 'scholarships' unahitaji 'commitment' hasa ya kutaka kusoma, kwa maana unaweza tuma maombi mara nyngi sana na kukosa. Kama ilivyo biashara, unavyokosa ndivyo unakuwa umeijua zaidi 'scholarships', mfano muda wa kufunguliwa, muda wa mwisho wa maombi, mahitaji yake, nk. Awamu ijayo unakuwa na maaandalizi mema zaidi ya mwanzo. Maana yake kama ulishawahi kuomba na kukosa 'scholarships' nyingi, unajikuta una "profiles' la kutosha kucheza nalo kwa awamu zinazofuata. Hii ndiyo sababu mwanzo nimesema inahitaji 'commitment', ukikurupuka tu unataka kusoma kisa ofisini umezinguana na bosi (unataka kumkimbia kwa muda), njia ya 'scholarships' haikufai.
Hitimisho: Tunapeana uzoefu tu, linapokuja suala la kuamini kila mmoja ana haki ya kuamini vile anavyoona ni sahihi.