Nimekuja leo tena katika mwendelezo wa maelezo mazuri. Unajua tukiwa marafiki kunavitu tunapashana na kuelezana ili hatimaye urafiki wetu udumu na uzidi kusonga mbele japokuwa hatuonani. Unajua vitu vingi duniani huwa vinapitia katika hatua Tatu. Kwa mfano katika mambo ya computer kuna INPUT - PROCESSING - OUTPUT. Vile vile katika mambo ya uzazi mambo yako hivyo hivyo lazima kupitia katika hatua tatu.
Leo ninaongelea hizi hatua tatu katika kufikia hatima ya kila mmoja wetu. Unajua katika ndoto ya kila mmoja lazima kuna hatua tatu. Mwanzo wa ndoto, ndoto kufanyiwa kazi na hatimaye ndoto kuonekana.
Hatua ya kwanza huwa ni nzuri sana na mtu hupata nguvu ya kufanya hiyo mipango aliyo ipanga. Mtu anaweza akatoa ahadi vizuri sana na mkaongea vizuri. Furaha inapatikana mwanzo wa ndoto.
Hatua ya tatu huwa nzuri au isiwe nzuri. Kwa sababu sababu inategemea hatua ya pili. Mimi hapa ninaongelea matokeo mazuri na hatima ya mtu katika ndoto yake. Kumbuka "muota ndoto hafi" kama huna ndoto katika maisha mda wowote waweza kufa kwa maana huna maana katika dunia.
Unajua katika hatua ya pili ndio pale watu wanakata tamaa na wanashindwa kuelewa hivi kweli ndoto walizo nazo ni za ukweli au sio. Watu wengi hawaelewi ugumu wa hatua ya pili au wanakuwa hawajui kama wapo katika hatua ya pili.
Mtu anakuwa na ndoto ya kuwa tajiri mkubwa na anataka wakati huo huo awe tajiri hilo haliwezekani ni lazima upitie hatua ya pili ili ufikie ndoto.
Kuna kitu kingine nina taka niongee hapa. Unakuta mwanamke kaolewa amekaa na mme kwa mda fulani kwenye ndoa. Unakuta anaanza kujikakamua na kujiona kama yeye ni malikia, hafanyi kazi yoyote na kutaka kuishi katika hatua ya tatu wakati hajafikia. Hakika huyo hatafikia ile ndoto yake kwa sababu anaangamia kwa kukosa maarifa.
Unapokuwa unaujenzi wa nyuma imara ni lazima kwanza uchimbe shimo kwaajili ya msingi. Unajua shimo maana yake ni nini. Unapotea kwanza na hauonekani halafu baadae ndio unakuja kuonekana na nyumba imara. Huwezi ukafikia hatima ya ndoto bila kupitia hatua ya pili.
Hatua ya pili inahitaji uvumilivu wa hali ya juu. Utatukanwa utasemwa vibaya na kila jambo baya utalipata. Hatua ya pili sio rahisi ni ngumu sana. Ndio kipindi watu hukata tamaa. Hivi umewahi kujiuliza kwanini watu huwa ni wasumbufu sana kwenye miaka 18 - 45? na hivi unajua vifo vingi huwa vinatokea katika kipindi hicho? ni kwa sababu ni kipindi cha hatua ya pili. Ni kipindi cha kupata ujuzi ili uje uishi kwenye hatima yako.
Ninayo maneno mengi sana ya kuongea cha zaidi ni kupata kujua katika kila wazo unalowaza kufanya kumbuka kuna hatua ya pili. Ndio utapata nguvu ya kufikia hatima yako.