Ugumu wa biashara ni suala la mpito

The hammer

JF-Expert Member
May 17, 2011
2,381
1,760
Nchi hii ni yetu sote,lazima tuipende!

Mambo mengi sana hayaendi sawa kwa kipindi hiki,sijajua kuwa ni suala la mpito tu au ndo la kudumu.Nashindwa kusema ni la mpito kwasababu ya mambo kadhaa yanayofanyika.

1:Leo hii ukienda TRA kukadiriwa kodi kwa biashara mpya,basi unaweza ukajikuta unakata tamaa na ukaacha kuwekeza. Biashara mpya kabisa ila kodi utakayokadiriwa ni kubwa sana kiasi kwamba wengi inawashinda katika hatua za mwanzo tu na nchi yetu hii tatizo la ajira ni kubwa sana na watu wanahitaji kujiajiri katika uzalishaji ili kupunguza tatizo la ajira.Tax holiday haipo,purchasing power ipo chini sana kwa sasa,kodi juu ni lazima hiyo biashara itashindwa katika hatua za mwanzo tu.

2:Kodi kwa biashara ambayo ina exist ni ya kukandamiza,ambayo haina huruma na hakuna negotiation na maafisa wa TRA.Ni kwamba hailipiki. Kuna vilio sana mtaani kuanzia wenye kipato hadi wasio kuwa na kipato.Biashara inategemea namna ambavyo purchasing power ilivyo.Kwa namna tunavyoenda sitegemei kama kutakuwa na uwekezaji mkubwa kutoka nje ya nchi.Kama bank ambapo ni eneo la watu kukopa ili kuendeleza mitaji yao nao wanalalamika UKATA ambapo inaleta hata hatari ya kufilisika,basi kuna sababu za msingi sana kushughulikia hilo maana kulia ukata si sifa hata kidogo kwa watu wanaojibidiisha katika kazi zao.Kuna athari sana za kimaendeleo ya kiviwanda na uwekezaji katika hilo.Serikali ingetolea majibu hayo yote ili watu wajue ni tatizo lonaloshughulikiwa kwa namna gani na kwa kopindi gani.
Denmark ni nchi inayoongoza kwa utozaji wa kodi kwa wananchi wake duniani,karibu 40% ni kodi ila hawalalamiki ila wanafurahia huduma wanazopata.Je,Watanzania tunafurahia huduma tunazozipata?

Na pia kuna kodi na tozo nyingi sana kiasi sidhani kama kina mtu anamajibu kuwa tunachangia asilimia ngapi kwa nchi yetu kwa kodi tunazolipa.

3:Fedha mtaani imekuwa ngumu sana kuipata na hivyo purchasing power kuwa ndogo sana.

Athari zake hili lipo wazi sana.Leo ukienda TBL watakuambia uzalishaji umepungua,AZAM nao hivyo hivyo n.k hapo watapunguza wafanyakazi na kodi itapungua pia.Fedha isibanwe sana...Wananchi kutaabika si kigezo cha kila mtu anatakiwa afanye kazi,atafanya katika lipi na wapi na mtaji gani.

4:Kuagiza bidhaa kupitia bandari yetu imekuwa kama ni namna ya kupiga marufuku bidhaa zisishushwe bandari salama au kuingiza bidhaa kutoka nje.Hatutengenezi magari,sasa magari na mashine mbalimbali tutazitoa wapi ili kuanzisha viwanda vidogo vidogo?Hili lipo wazi sana.

Katika mambo hayo manne nachelewa kusema ni jambo la mpito iwapo hayo masuala hayatarekebishwa.

TRA ijisahihishe katika namna ya ku-negitiate na wateja wao na si mteja kuona ni adhabu kulipa kodi.Ni hayo tu kwa TRA na serikali!!
 
Back
Top Bottom