Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,331
- 33,141
Jitahidi kukimbia vyakula vyenye tindikali?? (Acid) kama Limau, ndimu, binzari, maharage, pombe kali au pombe kwa ujumla nk ...1. Tiba ya Vidonda vya tumboVidonda vya tumbo
Dawa yenyewe ni hivi, chukua kokwa la parachichi, likatekate vipande vidogo vidogo kisha anika juani mpaka likauke. Baadae saga ili kupata unga laini. Chukua yai la kuku wa kienyeji, pasua utoe kile kiini chenye rangi ya njano, changanya na ule unga ambao umeandaa awali, koroga ili kupata mchanganyiko mzuri.
Kisha mpe mgonjwa wako anywe kijiko kimoja mara tatu, baada ya siku tatu atakuwa amepona.
Baada ya hapo akitaka kujua kama amepona au la, anaweza kufanya test ya kawaida kabisa kwa kula maharage, au chakula chenye pili*2 au akaenda kupima hospitali kabisa.
2. Dawa ya vidonda vya tumbo tumia Dawa ya Hii ya Kienyeji - Ukiamka Asubuhi kabla ya kula kitu kojowa mkojo wako mwenyewe kwa kipimo cha Glasi moja uwe anakunywa mkojo wako kila siku Asubuhi kabla ya kula kitu kwa muda wa Siku Saba kisha uende kupima hivyo Vidonda vya Tumbo Vitapona na kukauka kabisa Mwambie jaribu kutumia hiyo Dawa itakusaidia Sana.
View attachment 36242
The Boss,
Vidonda vya tumbo (peptic ulcer disease) hutokea kwenye mfuko wa chakula (gastric ulcers) na pia kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenal ulcers). Tumbo ni kati ya sehemu mwilini ambazo huzalisha acid kwa jili ya kusaidia kwenye uyeyushaji wa chakula na katika kulinda utumbo na uambukizo wa vimelea vinavyoleta magonjwa.
Kama tujuavyo acid hii yaweza kuunguza sehemu hii ya utumbo na hivyo kusababisha madhara. Kuna njia tumboni ambazo zinaulinda utumbo usiweze kupata madhara haya ya acid, mojawapo ikiwa ni utando wa mucous tumboni lakini pia regulation katika utengenezaji wa acid ili isije ikazidi. regulation hii ni automatic mwilini. Regulation na uzalishaji wa acid hufanywa chini ya matakwa ya mfumo wa neva. Kwa hiyo acid lazima iwepo kwa ajili ya umuhimu wake, lakini isiwepo kwa kiwango kinachoweza kuleta madhara (hii ndio essence ya regulation).
Vidonda vya tumbo hutokea pale ambapo kunakuwa na uzalishaji mwingi wa acid kupita kiasi au pale ulinzi wa tumbo dhidi ya acid unapopungua. Acid hutengenezwa na chembe hai tumboni zinazoitwa parietal cells.
Sababu za vidonda vya tumbo
1. uzalishaji wa acid nyingi tumboni - hii husababishwa na kuongezeka kwa chembe hai zinazozalisha acid, chembe hizi zaweza kuongezeka kwa sababu ya cancer (gastrinoma - husababisha ugonjwa wa acid nyingi unaoitwa Zollinger - Ellison Syndrome), lakini chembe hizi pia zaweza kujigawanya bila mpangilio (hyperplasia) hivyo zikawa nyingi na kusababisha uzalishaji wa acid kuongezeka.
2. Kutokuwepo na uwiano kwenye regulation ya uzalishaji wa acid, kunatakiwa kuwe na uwiano kati ya vile vitu vinavyoamuru uzalishaji wa acid na vile vinavyozuia. Inapotokea vile vinavyoamuru uzalishi vikavizidi nguvu vile vinavyozuia uzalishaji basi acid huzalishwa kwa wingi na hivyo kusababisha vidonda.
3. uambukizo wa bacteria aina ya Helicobacter pylori . Hawa huharibu ule utando unaolinda utumbo na hivyo kufanya acid iweze kupenya na kusababisha vidonda
4. Kuna dawa pia ambazo mgonjwa akitumia sana zaweza kumsababishia michubuko na vidonda tumbo, dawa hizi ni zile za jamii ya NSAIDs (Non steroidal anti-inflammatory disease) kama aspirin, brufen, indomethacin (indocid) na zote za jamii hii.
Mechanism ya utokeaji wa vidonda ni complex na nadhani nimeelezea kwa kifupi na lugha ambayo naamini imeeleweka.
Matibabu yapo ambayo hukusisha dawa zinazopunguza utengenezaji wa acid, dawa zinazoua bacteria wa H. Pylori lakini na upasuaji endapo hizi dawa zitashindwa. Vidonda vya tumbo hupona kabisa endapo mtu atapata matibabu sahihi.
Ili upate matibabu sahihi inabidi kwanza upate uchunguzi sahihi na ugonjwa sahihi ujulikane. Kwa yeote mwnye dalili za ugonjwa huu tafadhali usinunue dawa pharmacy, nenda hospitali, unaweza kufanyiwa uchunguzi na ukapewa tiba muafaka. Kipimo kiitwacho gastroscopy ndicho hutumiwa kupima na kugundua vidonda vya tumbo kwa uhakika.
The Boss, yangu ni hayo tu.
hivi nini kinasababisha acid kuwa nyingi mwilini?
madhara yake?
uhusiano wa acid nyingi na vidonda vya tumbo ukoje???
tatizo la acid nyingi linatibika?????
vyakula vipi mtu asile?kwa mda gani??????
Vidonda vya tumbo vinatibika hata hospitali ndugu yangu,tafuta mshiko tafuta daktari bingwa atakufanyia uchunguzi,utaandikiwa dawa na utapona cha msingi ni kuzingatia masharti na kumaliza tiba,maana hapo ndo kwenye mtihani! Pamoja na matangazo ya dawa za kienyeji yanayoungwa mkono na baadhi ya wataalam MIMI SIKUSHAURI KUTUMIA DAWA ZA KIENYEJI KWA SABABU,tz hatuna technologia ya kutengeneza dawa kutoka miti shamba katika hali ya usafi unaokubalika,kwa hiyo unaweza kupona vidonda lakini ukapata tatizo la figo au ini SAWAAA!
Ndg zangu naomba msada nasumbuliwa na vidonda vya tumbo je tiba yake nini au siluhusiwi kutumia nin.nashukulu kwa ushilikiano wenu
vp ndg yng je hapo kwenye masharti umenitisha nakuomba japo unidokeze japo kidogo nami nifahamu japo hata dondoo