Ugonjwa wa presha (blood pressure) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa presha (blood pressure)

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jan 14, 2013.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,431
  Likes Received: 4,307
  Trophy Points: 280
  UGONJWA WA PRESHA (BLOOD PRESSURE)  [​IMG]

  [​IMG]


  Presha ya kawaida isiwe zaidi ya 140/90mmlHg.
  Presha ikiwa haitibiwi huharibu mishipa ya damu katika macho, misuli ya moyo kuwa minene , kusababisha mshutuko wa moyo (heart attack), mshipa ya damu safi kuwa migumu, figo kushindwa kufanya kazi (kidney failure) na kiharusi (stroke).
  Presha kwa mwanamke mjamzito inaweza kusababisha kifafa cha mimba na kufanya hata kiumbe kufa tumboni. Hivyo ni muhimu kuchunguza presha ya wanawake wote wajawazito.

  Visababishi vya presha kuwa juu

   • Chumvi nyingi
   • Unene uliozidi
   • Umri mkubwa au uzee
   • Figo ikiwa haifanyi kazi
   • Historia ya ugonjwa wapresha kwenye familia
   • Ugonjwa wa kisukari
  Dalili ya mtu mwenye ugonjwa wa presha
  Mara nyingi presha haina dalili hadi ilete madhara na hivyo huitwa( silent killer ) muuaji wa kimyakimya
   • kichwa kuuma
   • kizunguzungu
   • kubanwa na pumzi
   • kutokuona vizuri
   • kichevuchevu

  Vitu vinavyo changia hali presha kuwa mbaya zaidi ni

   • Kula chuvi nyingi
   • Unene uliozidi
   • Kutofanya mazoezi mara kwa mara
   • Kunywa pombe nyingi
   • Uvutaji wa sigara
  Tiba ya ugonjwa wa presha


   • Mojawapo ya tiba ya presha ni kuacha vyakula vyenye chumvi kabisa kama itatumika iweke kidogo ya ladha wakati chukula kipo jikoni.
   • Pia mazoezi kwa ajili ya kupunguza uzito ni muhimu kwa tiba ya ugonjwa wa presha. Jitahidi kutenga mda wa mazoezi angalau dakika 30-60 mara tatu kwa wiki.
   • Epuka vyakula vyenye mafuta na lehemu maana vinaganda kwenye mishipa ya damu na kusababisha presha.
   • Daktari atakapo baini kuwa presha yako ipo juu, kulingana na aina na kiwango cha presha atakushauri kuhusiana na vyakula na jinsi ya kubadili mwenendo wa maisha au atakuanzishia dawa mara moja. Ni muhimu uelewe kuwa utakao anzishiwa dawa hutakiwi kuziacha maisha yako yote vinginevyo hali ya presha itarudi kama mwanzo.
   
 2. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2013
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,982
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  huu ugonjwa siku hizi unawapata watu wengi sana.
  ahsante kwa darasa mkuu.
   
 3. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2013
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,725
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  mkuu MziziMkavu toa darasa na kwenye mtu mwenye low pressure
  nilipima pressure ikawa 94/63 hapo vipi?
  huwa nafanya mazoezi kwa wiki mara mbili kwa muda wa dk 30
  na nina uzito wa kilo 52
  naomba mashauri
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,431
  Likes Received: 4,307
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kichwa Ngumu Presha ya kawaida isiwe zaidi ya 140/90mmlHg.Kwa kilo ulizokuwa nazo ni poa uwe unakula matunda na mboga za majani.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2013
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,431
  Likes Received: 4,307
  Trophy Points: 280
  HYPOTENSION : Low Blood Pressure
  Ifahamu Presha ya kushuka


  Nini presha ya kushuka ?


  Hypotension ndio jina alinalotumika kuelezea presha ya kushuka (90/60 mm Hg) ambayo huonekana kutokuwa na sababu iliyoifanya itokee.Kipimo cha presha huwa na namba mbili. Namba moja huwa juu na nyengine huwa chini.

  Hypotension (haipo juu). Kwa watu wengi presha hii huwatia kizunguzungu na kuwaangusha. Presha hii ikiwa ya muda mrefu husababisha mtu kupata maradhi ya mshtuko.Watu wenye afya nzuri, hasa wakimbiaji, presha ya kushuka huwa ni dalili ya uzima kwao.
  Si rahisi kuziona dalili kwa mtu mwenye presha ya kushuka hata kama imedumu kwa muda mrefu. Mara nyingi matatizo ya kiafya huwa ni

  dalili ya presha ya koshuka pale mtu presha yake inaposhuka ghafla. Wakati huo wa matatizo ya kiafya, damu kidogo hufika katika ubongo. Hali hii humfanya mtu awe na kizunguzungu au kuumwa na kichwa kusiko kuwa kukubwa. Kushuka ghafla kwa presha mara nyingi humtokezea mtu pale anapofanya jambo la haraka kama mtu aliyekaa na kutaka kusimama mara moja. Kitaalamu presha hii inajulikana


  kama postural hypotension, orthostatic hypotension, au neurally mediated orthostatic hypotension.

  Postural hypotension inachukuliwa ni hali ile ya kushindwa kwa mfumo wa mawasilianao unaojiendesha wenyewe mwilini kufanya kazi yake kikamilifu (autonomic nervous system). Mfumo huu huendesha na kuongoza vitendo visivyo vya hiari (involuntary vital actions), kama vile

  mapigo ya moyo kubadilika kutokana na jambo lililotokea kwa wakati uleopo. Kwa kawaida unapoinuka, kiwango fulani cha damu yako kinakuwa kimebaki sehemu ya chini (miguuni). Kukiwa hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa na mwili wako, hali hii itasababisha presha yako kushuka. Katika hali hii mwili wako unafanya nini ?


  Mwili wako unapeleka taarifa kwenye moyo na kuamuru uongeze usukumaji wa damu ambao utaizidi mishipa yako na kuifanya kuwa membamba hali itakayopelekea kuifanya presha yako kubakia ileile. Ikiwa jambo hili halikufanyika au limaefanyika polepole sana, presha yako itashuka ghafla. Hapa ndipo mtu unapomuona anaguka ghafla.


  Kwa ufupi athari ya maradhi ya presha ya kushuka na ya juu huongezeka kadri mtu anapokuwa na umri mkubwa na pia kubadilikabadilika kadri umri unavyoongezeka. Jambo jengine la kufahamu ni kuwa, ufikaji wa damu kikawaida kwenye ubungo unapungua kadri umri unavyoongezeka. Inakisiwa kiasi cha asilimia 10 mpaka 20 ya watu wenye umri unaozidi miaka 65, wanapata tatizo la presha yao kushuka.


  Ni kiwango gani cha presha kinapofika ndio huwa maradhi ?
  Hakuna kiwango maalum kinachojulikana ambacho ni sawasawa kwa watu wote kikifika ndio kinaitwa maradhi. Kiwango ambacho kwako ndio uzima, basi huenda kwa mwenzako ikawa ni maradhi. Katika presha ya kushuka, madaktari wengi huchukulia kuwa tayari mtu ana

  maradhi pale aambapo kiwango chake cha presha kinafuatana na dali za maradhi yenyewe.

  Hata hivyo, baadhi ya wataalamu wanachukulia tayari mtu ana maradhi ya presha ya kushika pale vipimo vinapoonyesha kiwango hichi 90/60 mm Hg. Tufahamu kuwa kiwango cha namba inayosomwa chini katika kipimo cha presha (80/60 mm Hg ), hichi huonyesha tayari mtu huyu

  anapresha ya chini hata kama kile cha juu ( 90/80mm Hg) kina namba iliyozidi 100. Mfano ikiwa umepimwa presha na ukapata kipimo hichi 115/60 mm Hg, presha yako itakuwa ipo chini. Na kama umepata kipimo hichi 115/50 mm Hg, sio kwamba presha yako itakuwa ipo chini tu, bali presha hii itakuwa si ya kawaida.

  Dalili za maradhi


  Kama nilivyokwisha tangulia kusema, presha inaweza kuwa sawa kati ya watu wawili lakini ikawa na matokeo tofauti. Presha hiyo inayoweza kuwa sawa na ikawa na matokeo tofauti si yenye kipimo hichi 120/80 mm Hg. Presha yenye kipimo hichi 120/80 mm Hg, ndiyo nzuri na watu wenye presha hii wanakuwa na afya nzuri. Kitu muhimu ni kujua, mabadiliko gani yanaleta tatizo katika presha hata inapelekea kuwa si ya kawaida.

  Presha nyingi za watu wanapopimwa huwa zinakuwa kati ya 90/60 mm Hg (presha iliyo chini) mpaka 130/80 mm Hg (presha iliyo juu). Mabadiliko ya kushuka presha upande wa chini, hata kama kidogo kiasi cha 20 mm Hg, hupelekea matatizo kwa baadhi ya watu ( hasa watu wasiofanya mazoezi kila siku).

  Mtu mwenye mazoezi ambae presha yake nzuri (120/80 mm Hg) akapimwa presha na kupata kipimo hichi, 110/60 mm au 120/70 mm Hg, mtu huyu hatakuwa na tatizo lolote la presha

  Kuna aina tatu za presha ya kushuka :

  Ø Orthostatic sambamba na postprandial orthostatic (Orthostatic hypotension, including postprandial orthostatic hypotension)
  Orthostatic, hii ni aina ya kwanza ya presha inayosababishwa na kubadili mazingira uliyonayo kwa ghafla, maranyingi hutokea kwa mtu anayesimama kutoka alipolala. Presha hii haidumu muda mrefu, kiasi cha sekunde chache mpaka dakika moja. Ikiwa presha hii itatokezea

  baada ya kula, basi itakuwa ni hatua ya pili (postprandial orthostatic) .Hatua hii ya pili huwapata zaidi wazee na wenye presha ya juu.

  Ø Neurally mediated hypotension (NMH)
  NMH kama ilivyo kifupisho cha presha aina ya pili, huwapata zaidi vijana na watoto. Presha hii hutokea pale mtu anaposimama kwa muda mrefu. Maranyingi huwapata sana watoto.

  Aina hii ya pili ya presha ya kushuka maranyingi husababishwa na hali zifuatazo :

  Utumiaji wa pombe
  Utumiaji wa dawa za kutibu presah ya juu.
  Utumiaji wa dawa za kumtoa fahamu mtu wakati wa kufanyiwa upasuaji

  Mambo mengine yanayosababisha presha kushuka ni pamoja na :
  Ugonjwa wa Kusukari
  Mtu kula kitu kinachomdhuru
  Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida
  Maradhi ya kuharisha
  Kuzimia
  Maradhi ya moyo
  Maradhi ya kustuka

  Ø Severe hypotension hii ni aina ya tatu ya presha ya kushuka ambayo hutokana na kpoteza damu
  Kwa muhtasari, dalili za presha ya kushuka ni pamoja na :

  Kuona kizunguzungu/kuumwa na kichwa kusiko kuwa kukubwa
  Kuzimia
  Kushindwa kuzingatia
  Kushindwa kuona vizuri ghafla
  Kuona baridi,
  Kujihisi kuchoka sana
  Kuvuta pumzi kwa tabu
  Kutapika
  Kuhisi kiu

  Hali zinazosababisha kupata presha ya kushuka.

  Kinachosababisha presha ya chini bado hakijatambulika hasa. Chanzo chake hakiko wazi. Hata hivyo mambo yafuatayo yanaweza kuhusiswa nayo :
  Kuwa na mimba
  Matatizo ya homoni mwilini, maradhi ya kisukari, au upungufu wa sukari mwilini
  Utumiaji mkubwa wa dawa
  Ulaji wa dawa za presha unaopindukia kiwango (Overdose) kwa mtu mwenye presha ya juu.
  Maradhi ya moyo
  Maradhi ya figo

  Nani anapata presha ya kushuka ghafla ?

  Presha ya kushuka ghafla inayompata mtu anapoinuka ghafla, inaweza kumpata mtu yeyote kwa sababu tofauti zikiwemo,
  o kuharisha sana,
  o kukosa chakula ( njaa kali) kwa muda mrefu,
  o kusimama kwa mapigo ya moyo, au
  o kuchoka kupita kiasi.
  o Pia inawezekana ikawa ni urithi wa maradhi,
  o umri mkubwa,
  o matumizi ya dawa,
  o utapiamlo na
  o mambo mengine kama kupatwa na madhara ya jambo fulani.
  Nini kinaifanya presha inayoshuka iendelee ?

  Pia Presha ya kushuka mara nyingi huwapata watu wanaotumai dawa kwa kutibu presha ya juu (hypertension). Pia huwapata wajawazito au wagonjwa wa kisukari. Mara nyingi wazee nao hupata maradhi haya hasa wale walio na presha ya juu wakiwa wanaendelea kutumia dawa zao za presha.


  Baadhi ya maradhi ambayo yanasababisha presha kushuka kuendelea ni pamoja na

  ü ukosefu wa vitamin mwilini,
  ü madhara kwenye uti wa mgongo, na
  ü kensa hasa kensa ya mapafu.
  Wakati gani wa kuchukua hatua za matibabu

  Matibabu huanza na hatua zako wewe mwenyewe. Wakati utakapojiona presha yako inashuka, kaa chini au lala chali na unyanyue miguu yako juu. Wakati yanafanyika haya, ufanyike utaratibu wa kuonana na daktari haraka. Pia ufanyike utaratibu wa kuonana na daktari yanapoonekana mambo yafuatayo yamemkuta mtu :

  Maumivu ya kifua
  Kizunguzungu
  Kuzimia
  Homa kali sana
  Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida
  Kupumua kwa tabu

  Pia afuatwe daktari haraka ikiwa baada ya hayo yaliyotokea, kuongezeka na haya yafuatayo :
  Mtu anapata matatizo makubwa ya mkojo
  Kushinwa kula au kunywa chochote
  Kuendelea kuharisha au kutapika kwa muda mrefu

  Matibabu na Dawa

  Presha ya kushuka ambayo haijulikani chanzo chake wala haileti dalili au inampa mtu kizunguzungu anaposimama, mara chache inaweza kutafutiwa matibabu. Ikiwa zipo dalili, matibabu yataendana na chanzo chenyewe na daktari atashughulikia hicho chanzo. ( kuharisha,maradhi ya moyo, kisukari). Ikiwa presha ya chini imesababishwa na matumizi ya dawa kwa matibabu, basi matibabu yake huwa kubadili dawa nyengine ua kuacha kutumia dawa kabisa.


  Ikiwa hakuna uhakika wa sababu za presha ya kushuka au hayapatikani matibabu yaliyo sahihi, matibabu sahihi yatakuwa ni kuifanya presha yako ipande na kuondoa zile dalili zanazokupata inapokujia.
  Kwa kutegemea umri wako, hali yako ya kiafya na aina ya presha uliyonayo, mambo haya yanaweza kukusaidia :

  Ø Kuongeza matumizi ya chumvi. Matumizi ya chumvi lazima yawe kwa kipimo, kwani chumvi nyingi hupandisha presha. Kabla hujaanza kuongeza matumizi ya chumvi, ni vizuri uwasiliane na daktari ili akupe kiwango cha matumizi.


  Ø Kunywa maji mengi. Kunywa maji mengi kunamsaidia kila mtu sio mtu mwenye presha ya chini tu. Tunapozungumzia maji tunalenga zaidi vinywaji na sio maji peke yake, lakini vinywaji vyenyewe view ni maji, maji ya matunda maziwa na hata kahawa au chai. Tahadhari ichukuliwe kwa vinywaji vya viwandani kwani huwaletea matatizo baadhi ya watu.


  Ø Kuvaa mavazi yenye kubana. Haya ni mavazi ya mpira ambayo yanavaliwa sehemu za miguuni. Mavazi haya yanasaidia kufanya damu yako isikae miguuni na iendelee kwenye mzonguko wake kikawaida.
  Ø Matumizi ya dawa. Zipo dawa mbalimbali ambazo zinatumika kufuatana na hali ya presha uliyonayo.
  Matibabu hospitalini.

  Presha ya kushuka inayomtokezea mtu mwenye afya nzuri ambayo haina dalili zozote na haimletei matatizo yeyote, hatahitajika kutumia dawa.Ikiwa zipo dalili, atahitaji matibabu kutokana na hizo dalili zilizoonekana.Ikiwa presha ulokuwa nayo inatokana na matumizi ya dawa, daktari atakubadilishia dawa nyengine au utaacha matumizi ya dawa. Wale wenye NMH pamoja na matumizi ya dawa, inabidi waache tabia


  ya kusimama muda mrefu. Kimtazamo presha ya chini inatibika hata kufikia mtu kuwa na presha ya kawaida.
  Napenda nichukue nafasi hii kuwafahamisha kuwa, bila kubadili mfumo wa maisha ulionao, hata ukikusanyiwa dawa nzuri za dunia nzima kwa kutibu maradhi yako hutopata uzima wowote. Kubadili mfumo wa maisha si katika kuishughulikia presha tu, bali kwa maradhi yote ndio

  tiba sahihi. Nini dawa zinafanya ?. Dawa zinalazimisha kuurudisha mfumo katika hali yake ya kawaida tu. Baada ya dawa kutoa msaada wake huu, kinachotakiwa kwako wewe kuendeleza mfumo huo unaofaa ambao dawa zimekurudishia tena.
  Kwa kutegemea sababu za kupata presha uliyonayo, unaweza kuchukua hatua zifuatazo :

  § Kunywa maji mengi, kuacha kunywa pombe, Kula vyakula kiafya (kula nafaka, matunda, mbogamboga, kula mifupa ya samaki na hata ya ndege[kuku,njiwa nk]) Tupendelee kuku wa kienyeji zaidi. Ikiwa kuongeza chumvi katika chakula, basi usizidishe vijiko viwili vya chai kwa siku na ni vizuri sana upate ushauri kwa daktari.


  § Kujenga utamaduni wa kuinuka taratibu ulipo kaa ua kulala. kulalia mto, ikiwa unapenda kunalalia ubavu, pendelea kulalia upande wa kulia (kila unapozungumzia presha, basi jambo la kwanza la kukumbuka ni moyo, moyo wako uko upande wa kushoto, kitendo cha kulalia upande wa kushoto kinaweza kuupa tabu moyo katika utendaji wake wa kazi).


  § Kuwa na tabia ya kula chakula kidogo katika mlo wako. Kufanya hivyo kunasaidia presha yako kutoshuka baada ya kumaliza kula. Jipangie utaratibu wa kula mara kwa mara ili uweze kula chakula cha kutosha. Punguza kula vyakula vyenye uwanga kwa wingi kama vile, mbatata, wali na mikate. Kula chakula pamoja na chai au kahawa. Ni vizuri haya yote utakayoyafanya ukawasiliana na daktari kabla.


  Kinga ya presha.

  Ikiwa wewe ni mzima au tayari una presha ya kushuka, daktari atakushauri hatua za kuzuia isitokee au isiendelee au kuipunguza. Hatua hizo ni pamoja na :
  1. Kuacha unywaji wa pombe.
  2. Kuepuka kusimama muda mrefu ( hasa ikiwa tayari una NMH)
  3. Kunywa maji kwa wingi
  4. Kuinuka taratibu kutoka ulipokaa ua kulala
  5. Kuvaa mavazi ya kubana miguuni (ikiwa tayari unayo)
   
 6. m

  mrs saronga Member

  #6
  Jun 25, 2013
  Joined: Jun 15, 2013
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu, nasumbuliwa na Presha yakupanda sana,Swali ni kwamba nimeshafikia stage ya kumeza dawa Je? nikipima Presha ikiwa normal bado niendelee kumeza dawa?
   
 7. F

  FESTO MANDE New Member

  #7
  Mar 20, 2015
  Joined: Feb 24, 2015
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana mpendwa mm nauliza mke wangu mazingira anayokaa ni ya kumpa joto sana je inaweza kuwa chanzo cha pressure kushuka?
   
 8. r

  revelianalphonce Member

  #8
  Apr 26, 2016
  Joined: Oct 27, 2015
  Messages: 10
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Naomba ushauri Hali imenitokea ghafra juzi coz ndo mara yangu ya 1 nikapimwa presha 154/93 nikapewa dawa jana nimeenda wanasema bado 150/91 je niendelee kutumia dawa na nipumzike mda wote na niendelee kupumzika?
   
 9. r

  revelianalphonce Member

  #9
  Apr 26, 2016
  Joined: Oct 27, 2015
  Messages: 10
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Mzizi mkavu please majibu
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2016
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,431
  Likes Received: 4,307
  Trophy Points: 280
  Mkuu una miaka mingapi wewe ? Angalia chini hapo Umri wako na Kiwango gani cha Presha unachotakiwa uwe nacho .

  MARADHI YA PRESHA KWA UMRI WAKO.jpg
   
 11. r

  revelianalphonce Member

  #11
  Apr 27, 2016
  Joined: Oct 27, 2015
  Messages: 10
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Mkuu nina miaka 30 kwa jana nimeenda hospital tena kucheck jioni presha ikawa 148/121 kama dakka 5 doctor mwingne akanipima pale pale majibu tena 135/95 je inaweza kuwa machine hiyo mbovu au laa?
   
 12. r

  revelianalphonce Member

  #12
  Apr 27, 2016
  Joined: Oct 27, 2015
  Messages: 10
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Nina miaka 30 kwa jana nimeenda hospital tena kucheck jioni presha ikawa 148 /121 doctor akashangaa kama dakka5 akaja doctor mwingne akanipima
  pale pale majibu tena 135 /95 sasa wakasema nirudi leo please naomba ushauri kuwa je machine inaweza kukosea majibu
   
 13. r

  revelianalphonce Member

  #13
  Apr 27, 2016
  Joined: Oct 27, 2015
  Messages: 10
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Nina miaka 30 kwa jana nimeenda hospital tena kucheck jioni presha ikawa 148 /121 doctor akashangaa kama dakka5 akaja doctor mwingne akanipima pale pale majibu tena 135 /95 sasa wakasema nirudi leo please naomba ushauri kuwa je machine inaweza kukosea majibu? Make nipo njia panda mkuu!!
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2016
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,431
  Likes Received: 4,307
  Trophy Points: 280
  Mashine inafanaya kazi ila Presha yako inashuka na kupanda hiyo Presha yako nenda tena kamuone daktari
   
 15. lameckkawawa

  lameckkawawa JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2016
  Joined: Sep 13, 2015
  Messages: 854
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 80
  Mzizimkavu kuna ndugu yangu Ana presha yakupanda now ila panda hadi kifikia hadi 300 na ana umri 32 nani mjamzito kuna mdaa unapigua na kupanda apo nini mtazamo wako
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2016
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,431
  Likes Received: 4,307
  Trophy Points: 280
  Anione mimi nimpe Dawa Presha yake iwe sawa.
  Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
   
 17. mzibua chemba

  mzibua chemba JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2016
  Joined: Jul 18, 2016
  Messages: 480
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 80
  presha I nafika 300?
   
 18. TheNinja

  TheNinja JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2016
  Joined: Jul 29, 2016
  Messages: 252
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 60
  Nini matibabu ya pressure ya macho MziziMkavu
   
 19. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2016
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,431
  Likes Received: 4,307
  Trophy Points: 280
  Dawa ya kutibu Maradhi ya presha ya macho aka (Glaucoma)
  ninayo ukihitaji .Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
   
Loading...