Ugonjwa wa Nguruwe unaosababishwa na tegu (cysticercosis) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa Nguruwe unaosababishwa na tegu (cysticercosis)

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Aug 21, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Tegu (Tapeworm) ni aina mojawapo ya minyoo inayosababisha ugonjwa unaojulikana kitaamu kama Cysticercosis na hii inatokana na kuwepo kwa viuvimbe vingi ndani ya viungo vya mwili vilivyojaa majimaji. Aina ya tapeworm inayosababisha ugonjwa huu inajulikana kwa jina la kisayansi kama Taenia solium. Madhara yaletwayo na ugonjwa huu ni makubwa

  ikiwemo ya kiuchumi kwa vile nyama ya nguruwe mwenye ugonjwa hutupwa yote, lakini pia ugonjwa huleta mdhara makubwa umpatapo mwanadamu. Ugonjwa huu upo sehemu mbalimbali za Tanzania na madhara yake yamekuwa ni

  makubwa situ kwa wafugaji bali hata kwa walaji wa nyama ya nguruwe. Tafiti nyingi sana zimefanywa na wataalamu kutoka SUA katika kitivo cha tiba ya mifugo na kubaini uwepo wa ugonjwa huu hasa maeneo ya Mbulu, Mbeya, Iringa, Morogoro na mengine mengi tu. Ugonjwa huu uko karibu maeneo yote duniani isipokuwa haujawi kuripotiwa katika maeneo ya Pasifiki pekee.


  UENEAJI WA UGONJWA HUU
  Ugonjwa huu unasababishwa na tegu (Taenia solium) wakiwa katika hatua ya lava, na nguruwe anaupata ugonjwa huu anapokula chakula kilichochanganyikana na kinyesi cha binadamu chenye mayai ya tegu. Wakati mwanadamu anaupata ugonjwa huu anapokula nyama ya nguruwe yenye ugonjwa huu ambayo haikupikwa vizuri au kwa bahati mbaya akimezaa mayai ya tegu kutoka katika vyakula vilivyochanganyikana na uchafu wenye mayai ya tegu. Mzunguko mzima wa maisha ya tegu ni kama inavyoonekana kwenye kielelezo hapa chini.

  [​IMG]

  Kulingana na kielelezo hapo juu utabaini kuwa kwa asilimia kubwa kinachofanya ugonjwa huu unendelee kushamili katika maeneo ambapo ugonjwa huu upon i kutokana na nguruwe kula kinyesi cha binadamu. Hivyo ufugaji huria wa nguruwe (kuwaacha wajitautie wenyewe chakula) pamoja na watu kujisaidia hovyo bila kutmia choo ni michango dhahili ya ugonjwa huu nan i maeneo ambayo yanapaswa kurekebishwa ili kuzuia mwendelezo wa ugonjwa huu.


  DALILI ZA UGONJWA
  a) Dalili kwa nguruwe
  Kwa bahati mbaya ugonjwa huu una dalili chache sana kwa nguruwe na mara nyingi si rahisi kuziona nguruwe akiwa hai, hivyo huonekana wakati amechinjwa. Uumuhimu wake ni kule kumpata hasa mwanadamu na kupelekea kukataliwa hata nyama ya nguruwe na hivyo kuwa hasara kwa mfugaji. Dalili za ugonjwa huu hasa ugonjwa ukiwa kwa nguruwe wengi ni kama zifuatazo;
  -Mfumo wa fahamu na misuli huwa huvurugika
  -Kuwepo kwa malengelenge katika maeneo kutolea haja kubwa na chini ya ulimi
  -Afya hudhoofika
  -Mapigo ya moyo hushindwa kufanya kazi
  [TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Lava wakiwa chini ya ulimi wa nguruwe[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Ukimchinja nguruwe
  Ukimchinja nguruwe unaweza kuona uvimbe uliojaa maji yenye malengelenge wenye ukubwa wa milimita 5-8 kwa milimita 3-5. Maji yake huwa na rangi ya kahawia au waridi na wakati mwingine kichwa cha lava huonekana kama nukta nyeupe. Na viuvimbe hivyo vinaweza kuonekana maeneo yafuatayo;
  -Kwenye moyo
  -Ulimi
  -Misuli ya mashavuni, mabegani, koromeo, kiwambo kinachotenganisha mapafu na tumbo na misuli ya mbavuni na shingoni.
  -Mara chache viuvimbe vinaweza kuonekana kwenye ini, bandama, ubongo na tezi.
  [TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Nyama ya nguruwe ikiwa imejaa vijiuvimbe maeneo mbalimbali[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Moyo wenye vijiuvimbe vingi vyenye majimaji ndani[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  b) Dalili za ugonjwa kwa binadamu

  Mwanadamu aliyepata tegu wakubwa mwilini mwake ataanza kutoa mayai kwenye kinyesi kuanzia wiki ya 8 hadi 12. Na tegu wakubwa huweza kuishi ndani ya mwili wa binadamu wakitoa mayai na vipingiri vilivyopevuka kupitia kinyesi kwa muda wa

  miaka 30. Hii ni hatari sana kwa usambazaji wa ugonjwa. Dalili za ugonjwa huanza kujitokeza kuanzia wiki moja au miaka kumi na kuendelea tangu awapate hao tegu na mara nyingi lava wakiwa wanakufa.

  Mwanadamu awapo na tegu wakubwa mwilini mwake huwa si rahisi sana kutambua, shida huanza anapokuwa na lava. Mara chache tegu akiwa tumboni mwa binadamu dalili zisizo maalumu kama kuwa mkali bila sababu (anawaka), kupoteza hamu

  ya kula, kupunua uzito na maumivu ya tumbo, kuharisha na kufunga choo zaweza kujitokeza.
  Dalili za ugonjwa huu kwa mwanadamu zaweza kuwa kali kutegemea eneo ambalo lava (vijiuvimbe) wapo ndani ya mwili. Na

  ni mara chache vijiuvimbe vinaweza kufika sentimita 1-2 hasa kwenye ubongo wa mwanadamu.
  -Misuli: Vijiuvimbe kwenye misuli katika maeneo mbalimbali ya mwili kwa kawaida havionyeshi dalili zozote, isipokuwa mabonge ya uvimbe waweza kuyatambua kwa kubonyeza ngozi.
  -Macho: Vijiuvimbe vinaweza kuwa vinaelea kwenye macho na kusababisha macho kutokuona vizuri na hata kutenganisha mboni ya jicho.
  -Ubongo na uti wa mgongo: Vijiuvimbe hivi vya ugonjwa vikiwepo kwenye ubongo na uti wa mgongo huwa na dalili kama kuuma kichwa, kizunguzungu, kuchanganyikiwa, kuyumbayumba (kukosa urari) na kasha kufa. Kwa muda mrefu maeneo mengi hapa nchini na kwingineko barani Afrika wamehusianisha ugojnwa huu na ushirikina hasa mgonjwa unapoenda kichwani na kupelekea kwenye ugonjwa wa kifafa. Hapa ndipo hatari kubwa ya ugonjwa huu, kifafa na kifo kwa mwanadamu.

  Kifafa
  -Ni kawaida ya lava kwenda kwenye mfumo wa fahamu wa binadamu na hasa maeneo ya ubongo. Larva hukaa kwenye ubongo kwa muda mrefu sana kwani hulindwa na kizuizi damu-ubongo. Lakini kwasababu ya lava kufa na kuleta madhara kwenye ubongo dalili za kifafa huanza kuonekana
  [TABLE="align: center"]
  [TR]
  [TD][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]Uvimbe chini ya ulimi wa mwanadamu mwenye ugonjwa[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Jinsi ya kuutambua ugonjwa
  -Dalili zilizotajwa hapo juu zitasaidia kuutambua ugonjwa huu zikiunganishwa na za kimaabara.
  -Kwenye maabara uchunguzi wa kinyesi cha mwanadamu kuangalia uwepo wa mayai ya tegu kwa kutumia darubini hufanyika.
  -Larva wakiwa kwenye ubongo wa binadamu njia za kitaalamu zaidi hutumika kama MRI au CT brain scan. MRI ndicho kipimo chenye uhakika kwani kinauwezo wa kuonyesha hatua ya uvimbe, mahali ulipo na mabadiliko yake. Lakini gharama kubwa za kipimo hiki na gharama za kununua mashine yenyewe imefanya matumizi yake kuwa kwa nchi chache tu ambazo tena ugonjwa huu kwao si tatizo.

  Matibabu ya ugonjwa huu

  Matibabu ya ugonjwa huu yanalenga hasa tegu wakubwa, kwa wadogo wakiwa ndani ya viuvimbe vyenye ngozi isiyorushu dawa kupita huwa ngumu.

  Kwa nguruwe
  : Nguruwe watibiwe kwa kutumia dawa ya minyoo ( Oxfendazole ndiyo dawa inayopendekezwa kutumika kuua tegu na lava-ushauri wa mtaalamu ni muhimu)

  Kwa binadamu
  : Ukiwa nje ya mfumo wa fahamu si wa kutisha na hivyo hauhitaji matibabu maalumu. Dawa za minyoo zinatumika hata kwa wenye lava walio kwenye mfumo wa fahamu japo uponyaji wake si wa uhakika. Lava wakiwa kwenye mfumo wa fahamu upasuaji ili kuondoa uvimbe hushauriwa ufanyike. Lakini matibabu mengine hufanyika yatakayosaidia kushusha dalili za kifafa kabla ya upasuaji kufanyika.

  Njia za kuzuia ugonjwa huu

  Nguruwe: Nguruwe wafugiwe ndani ya mabanda na wasiruhusiwe kutembea nje ya banda
  -Wapatiwe dawa za magonjwa ya minyoo angalau kila baada ya miezi mitatu
  -Nguruwe wakaguliwe na wataalamu wakati wa kuwachinja na wale wote watakaopatikana na ugonjwa waharibiwe.​
  -Chakula na maji wanayopewa nguruwe yawe ni masafi​

  Mwanadamu
  : ​
  -Hakikisha matuzi ya choo nyumbani yanafanyika ipasavyo na epukuka kujisaidia sehemu isiyo na choo.​
  -Hakikisha unapima choo chako angalau mara moja kila baada ya miezi mitatu ili kujua hali yako kwa magonjwa ya minyoo​
  -Tumia dawa za minyoo angalau kila baada ya miezi mitatu ili kutibu magonjwa ya minyoo ambayo hayajaanza kuonyesha dalili. Kama eneo lina watu wengi wenye minyoo hii utibuji wa pamoja utasaidia kuzuia mzuko wa maisha ya tegu (Praziquantel na Albendazole zimependekezwa zitumiwe-ushauri wa daktari muhimu).​

  Kumbuka
  : Mwanadamu ndiye mwenye mchango mkubwa wa kuhakikisha ugonjwa huu unazulikika hivyo elimu ya kutosha kupambana na huu ugonjwa inahitajika kwa kiasi kikubwa sana. Maeneo kama ya Mbeya na Mbuyu

  yameonyesha kuwa ufugaji huria/holela wa nguruwe umechangia kwa kiasi kikubwa sana kwa ugonjwa huu kushamili maeneo hayo ikiwa ni pamoja na kutotumia choo.​
  Kwa maeneo yenye minyoo aina ya tegu, kutibu binadamu na nguruwe kwa wakati mmoja ndiyo njia pekee ya kuondokana na huu ugonjwa.

  Kwa Wale wanaokula Kitomoto Kuleni kwa Raha Zenu ila mujuwe na Madhara yake ni Makubwa
   
 2. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,164
  Likes Received: 1,889
  Trophy Points: 280
  Usijifanye Mtaalam Sana! Kila kitu Kinamadhara!

  HATA FUTARI YAKO


  Wanaongea Sana Humu ni Wale wanaongozwa na Vitabu!

  Kitu chochote Kikituzwa Vizuri Na kuhudumiwa hakuna Madhara Yoyote

  Mi nakushangaa sana Badala utoe Solution kama Mtaalam ni Jinsi gani Mfugo wa Nguruwe ufanywe ili kujiepusha na Madhara unaleta UDINI ndani.
   
 3. undugukazi

  undugukazi JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kila nyama tamu ila hii ya nguruwe ni kiboko aisee...asante kwa ushauri tutaanza kuiosha na maji ya moto kuzuia huo ugonjwa. Ubarikiwe aisee
   
Loading...