Ugonjwa wa Kutapika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa Kutapika

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Feb 23, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  [h=1]Kutapika[/h]Kutapika kwa kawaida ni dalili ya kuonyesha kuwa, kuna shida tumboni, umekula chakula kilichoharibika au una mafua.
  Unapoumwa sana na kichwa na kupata shida zingine za kiafya, au uja uzito, vinaweza kumfanya mtu atapike. Mara nyingi kutapika sio hoja lakini nyakati zingine, ni muhimu mtu aende atazamwe na daktari.Kuna uwezekano kwamba, unapotapika sana unaweza kuishiwa na maji ya kutosha mwilini.

  Namna ya kutibu kutapika:

  • Nusu saa au saa moja baada ya kutapika, kunywa maji kidogo kidogo ama vinywaji visivyo vileo.Usinywe mara moja au kwa wakati mmoja.
  • Pumzika vya kutosha
  • Baada ya tumbo kutulia jaribu kula vyakula vigumuvigumu kama vile mkate mkavu ,ndizi au kitu kizitozito na kitamu kama halua.
  • Meza dawa ya kuzuia joto na maumivu ya mwili ya Panadol au Tylenol.

  Muite daktari iwapo:

  • Unaishiwa na maji mwilini.Ukisikia kiu sana , midomo kukauka, mgonjwa kukojoa mkojo uliokolea na huwa anahisi usingizi au kizunguzungu ama huhisi kichwa kikiwa chepesi mno.
  • Shingo kuwa gumu lisiweze kugeuka
  • Unatapika zaidi ya mara kumi kaw siku ama ushindwe kumeza maji yoyote pasipo kutapika.
  • Unahisi maumivu makali ya kifua
  • Utapike damu ama vitu vinavyofanana na kahawa iliyosagwa.
  • Unatapika ukiwa na joto jingi la nyusi 38oc au zaidi ya hapo kwa zaidi ya siku mbili.
  • Unatapika kwa zaidi ya Juma moja .
  • Unashtukia tu ukiwa na maumivu makali ya tumbo ambayo huendelea kuwa machungu.
   
 2. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  hongera sana mkuu kwa management nzuri ya kutapika,kweli kutapika ni hatari sana maana ukitabika sana kunasababisha kukosekana kwa usawia wa fluid na madini mwilini ambapo kunaweza pelekea mtu akapata hypovolemic shock
   
 3. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tks kaka mzizi.

  Ila hii sentensi moja hapa kwetu Bongoland haitumiki:
  Hii ni ya ulaya
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Feb 25, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Kwani huko bongo hakuna Private doctor? najisahau kuwa kama na nyinyi mupo Ughaibuni Samahani. huku kila mtu ana Daktari wake ingawa Ma Hospiatli ni ya kumwaga kuwa na Daktari na wakili (advocate) ni vitu vya kawaida huku.
   
Loading...