Ugonjwa kwenye miti ya matunda (naomba msaada).

ROKY

Senior Member
May 4, 2011
179
195
Wadau wa kilimo, naomba msaada kwenye changamoto hii ya ugonjwa kwenye miti ya matunda.
Ugonjwa huu pia umeshambulia miembe, mistafeli na mipapai.
Pichani ni mti wa mpera umepata ugonjwa kama inavyoonekana.
Huu ni ugonjwa gani? na matibabu yake ni nini?

Asanteni.
upload_2016-12-26_17-0-27.png
 
the horticulturist

JF-Expert Member
Aug 24, 2012
1,814
2,000
Huo sio ugonjwa hao ni wadudu wanaitwa mealy bugs ,kwa kuwapunguza hakikisha kwanza unazuia sisimizi shamban kwako maana sisimizi wa kwenye miti ndio wanawasambaza na kuwalinda hao wadudu ,dawa piga dawa itakayoingia ndani ya mti na kuwaua wakiufyonza (systemic) kama vile actara 25wg,selecron 720ec,folimat,riyazinon 60 ec
 
Asante sana mkuu.
Je hizo dawa zina madhara yoyote kwenye matunda yalitoko kwenye miti husika ya matunda kwa sasa??
Maana nataka kutumia dawa hizo haraka na baadhi ya miti iliyoshambuliwa na wadudu hao ina matunda yanayokaribia kukomaa kama mapapai, maembe na mastafeli.
 
Zamaulid

JF-Expert Member
May 25, 2009
17,880
2,000
Huo sio ugonjwa hao ni wadudu wanaitwa mealy bugs ,kwa kuwapunguza hakikisha kwanza unazuia sisimizi shamban kwako maana sisimizi wa kwenye miti ndio wanawasambaza na kuwalinda hao wadudu ,dawa piga dawa itakayoingia ndani ya mti na kuwaua wakiufyonza (systemic) kama vile actara 25wg,selecron 720ec,folimat,riyazinon 60 ec
Kuna dawa niliuziwa kwa tatizo kama alilolisema mdau...inaitwa ivory...lkn bado naona hao wadudu wapo kwenye mstafeli wangu
 
kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
37,045
2,000
Mkuu hivi hii ni kweli eeh? Naona wengi wanarecomend hii.... Pilipili inaua wadudu wa aina gani?
ndio inaua wadudu, inatumika sana kwenye kilimo hai (organic) sio pilipili tu, kuna kitunguu swaumu na nyanya pia...
 
KIKAZI

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
1,161
2,000
ndio inaua wadudu, inatumika sana kwenye kilimo hai (organic) sio pilipili tu, kuna kitunguu swaumu na nyanya pia...
mkuu unaweza kutupa msaada jinsi ya kutengeneza hizo dawa yani pilipili,kitunguu swaumu na nyanya asante.
 
ROKY

Senior Member
May 4, 2011
179
195
Asanteni sana wadau wote mliochangia hapa.
Nitafanyia kazi kila hoja.
Thanks.
 
kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
37,045
2,000
naomba nitumie somo Zima la kiilimo cha nyanya , kitunguu swaumu
binamu, mimi sijasomea kilimo zaidi ya kushiriki katika mafunzo ya kilimo hai kama transalator na kama mtumishi katika shirika linalofanya mambo ya ushirika na kilimo, naamini watu watakupatia,
 
ladyfurahia

JF-Expert Member
May 10, 2011
13,944
2,000
binamu, mimi sijasomea kilimo zaidi ya kushiriki katika mafunzo ya kilimo hai kama transalator na kama mtumishi katika shirika linalofanya mambo ya ushirika na kilimo, naamini watu watakupatia,
asante binamu ila hata kidogo ukinipatia kinanitosha hasa mwanzo wa kujua mambo ya kilimo binamu
 
kabanga

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
37,045
2,000
asante binamu ila hata kidogo ukinipatia kinanitosha hasa mwanzo wa kujua mambo ya kilimo binamu
binamu nitakuongopea, zaidi ya kujua kidogo kwenye kutengeneza mbolea za organic na dawa zake vingine sijui....!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom