Ugonjwa gani huu?

Ugonjwa gani huu?

ASHA NGEDELE

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
784
Reaction score
327
Habarini humu..

Kwa ambao mshalima au wataalamu wa tikiti naomba ushauri huu ni ugonjwa gani na nini athari yake?

Nlidhani itakua chawa lakini mmea wote nimekagua hamna chawa. Pia kuna manyunyu yalipiga kidogo siku kama tatu kabla ugonjwa kuingia kwahio nimepiga Megasin, Ivory na Xantho..

Je tiba hii iko sahihi ama natakiwa kufata ushauri upi?
20170805_143843.jpg
20170805_143343.jpg

Asha [emoji6]
 
Maranyingi ukiona Jani limekunjamana kama hivyo ni wadudu walioko chini ya jani wanaofyonza majani (plant sap) na hatimae jani kupoteza muonekano wa kawaida..

Hivyo hali hiyo huwa husababishwa na wadudu wajulikanao kama Aphids au wadudu mafuta, au Mealybug / vifun'gata. Ila kama sio hao basi angalia chanzo cha mbegu uliotumia yawezekana ikawa na maambukizi ya viral disease.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majani yameshambuliwa na ukungu wa majani, kazania dawa pindi mvua zinaponyesha
 
POLESANA

DALILI ZINAONYESHA NI VIRAL DISEASES (VIRAL LEAF CURL

CHANZO KIKUBWA HUENEZWA NA WADUDU JAMII YA VIPEPEO WADOGO WEUPE (WHITE FLIES), AU WADUDU MAFUTA (AMPHIDS), UGONJWA WENYEWE VIRAL LEAF CURL HAUNA DAWA ILA UNACHOWEZA KUFANYA NI KUDHIBITI HAO WADUDU-VECTOR WANAOAMBUKIZA/KUSAMBAZA UGONJWA.

Tumia Sumu yeyote ya wadudu yenye Cypermethirin na Imidacloplid, au Cypermethrin na Pyrphrivos, au Imidacloplid na Chlorophyrivos, ndani yake changanya na Xantho au Megasin, au Multi Power Plus 78/76WP au Copper Oxycloride unayoipata katika Tan Copper au Blue Copper ili kuweka ujoto kwa mmea kuzuia faungus kumea kwa sababu ya hilo baridi/unyevu. Sumu za wadudu unazoweza kutumia ni _Kwa majina ya kibishara, zinaitwa, Prosper, Dududall, DuduCypermethrin, Buffalo, Blast, Actara etc

ILI KUBOOST UKUAJI NI VYEMA UKAPAGA LISHE KIDOGO YA YARA MILLER JAVA, AU NPK YA 17:17:17 ILI KUIMARISHA LISHE NA KUCHOCHEA NEW LEAVES KUTOKEZA, UKIWEZA NA JUU YA MIMEA PIA PIGA STARTER BOOSTER KAMA , POLYFEED STARTER, AU OMEX, AU MURPHY AU SUPER GROW, AU VIJIMAX, AU POTPHOS

Polesana

kilimomaarifa.tajiri Upepo wa Pesa Kilimo Kilimo Faida msaada please! hii ni fungal ama viral? na dawa gani zafaa?
 
POLESANA

DALILI ZINAONYESHA NI VIRAL DISEASES (VIRAL LEAF CURL

CHANZO KIKUBWA HUENEZWA NA WADUDU JAMII YA VIPEPEO WADOGO WEUPE (WHITE FLIES), AU WADUDU MAFUTA (AMPHIDS), UGONJWA WENYEWE VIRAL LEAF CURL HAUNA DAWA ILA UNACHOWEZA KUFANYA NI KUDHIBITI HAO WADUDU-VECTOR WANAOAMBUKIZA/KUSAMBAZA UGONJWA.

Tumia Sumu yeyote ya wadudu yenye Cypermethirin na Imidacloplid, au Cypermethrin na Pyrphrivos, au Imidacloplid na Chlorophyrivos, ndani yake changanya na Xantho au Megasin, au Multi Power Plus 78/76WP au Copper Oxycloride unayoipata katika Tan Copper au Blue Copper ili kuweka ujoto kwa mmea kuzuia faungus kumea kwa sababu ya hilo baridi/unyevu. Sumu za wadudu unazoweza kutumia ni _Kwa majina ya kibishara, zinaitwa, Prosper, Dududall, DuduCypermethrin, Buffalo, Blast, Actara etc

ILI KUBOOST UKUAJI NI VYEMA UKAPAGA LISHE KIDOGO YA YARA MILLER JAVA, AU NPK YA 17:17:17 ILI KUIMARISHA LISHE NA KUCHOCHEA NEW LEAVES KUTOKEZA, UKIWEZA NA JUU YA MIMEA PIA PIGA STARTER BOOSTER KAMA , POLYFEED STARTER, AU OMEX, AU MURPHY AU SUPER GROW, AU VIJIMAX, AU POTPHOS

Polesana
Asante kwa ushauri wako mkuu, ila nina maswali mawili

1. Je kama huu ugonjwa viral je ikiwa ni Ukungu/Fungal tiba inakuaje

2. Mmea unaathirika vipi na nini athari kwenye uzalishaji wa matunda.
 
KAMA UGONJWA NI WA FUNGUS, DAWA NI HIZO UNAZOTUMIA NA HIZO NILIZOZISEMA, MULTI POWER, RIDOMIL GOLD, SUCCESS, MISTRESS, EBONY, VICTORY, DAMKA//ODEON/BANKO, AGRIFOS 400 ETC,,,, etc

MAJANI NDIO JIKO LA MMMEA, YAKIATHIRIKA HAMANA CHAKULA KINACHOTENGENEZWA, HAMANA MATUNDA WALA MAUA=HASARA (MMEA KUFA)

Sawa nashukuru. Just another small one, hivi kama dawa zina viambato tofauti lakini zote ni za fungus au wadudu, ni sawa kuzichanganya pamoja kwa wakati mmoja?
 
Iko hivi, huwezi changanya dawa mbili za wadudu kwa mda mmoja au dawa mbili za ukungu kwa muda mmoja!!

Unaweza changanya dawa moja ya wadudu na moja ya fungus kwa mda mmoja not otherwise!!
 
Nimekuuliza hivyo makusudi. Kuna mkulima mwenzangu jirani na shambani kwangu kaniambia itakua umechanganya sumu ndo mana jani liliathirika ni jani changa. Nimezungumza na shamba boy kaniambia kachanganya dawa nne pamoja mbili za wadudu na mbili za fungus plus booster.

Je ni kweli mchanganganyiko wa hizi chemicals unaweza kuchoma majani kiasi hiki?

Hamna sehemu penye madhara ya chemical hapo..unalima kwenye joto kwenye baridi?binafsi sio dalili ya ugonjwa wa ukungu hapo ni wadudu au viral au baridi...huo mchanganyiko wa vitu vinne kulikoni una ugomvi na afya ya mmea au

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuuliza hivyo makusudi. Kuna mkulima mwenzangu jirani na shambani kwangu kaniambia itakua umechanganya sumu ndo mana jani liliathirika ni jani changa. Nimezungumza na shamba boy kaniambia kachanganya dawa nne pamoja mbili za wadudu na mbili za fungus plus booster.

Je ni kweli mchanganganyiko wa hizi chemicals unaweza kuchoma majani kiasi hiki?

Asha [emoji6]
Ni sawa na wewe umeze painkiller kama dicloper na panadol kwa muda mmoja..utakua unatafuta matatizo!! kuhusu ugonjwa wa wa mimea kilimomaarifa.tajiri ameshautolea maelezo hapo juu!!

Ila unaweza kumix dawa moja ya wadudu na moja ya fungusi na kwenye mchanganyiko huohuo unaweza weka na booster pia!! ila sio uweke dawa mbili za wadudu na mbili za fungus!! sio sahihi...
 
Yeah nafahamu hii lakini ni practice ya shamba boys wengi sana hii ni sawa na wale wanaochanganya NPK na CAN.. Ni normal practice na sio kwamba nimemwelekeza hivo kijana. All in all nimeelewa

Asha [emoji6]
 
Back
Top Bottom