Mwana Mpotevu
Platinum Member
- Sep 7, 2011
- 3,295
- 2,500
Wakuu
Kuna taarifa za kuibuka kwa ugomvi na kutokuelewana baina ya waziri mpya wa habari, utamaduni na micchezo Dr Fenela Mukangara na katibu mkuu wake Seth Kamuhanda. Chanzo halisi cha kutokuwepo kwa maelewano kati yao hakijawekwa bayana. lakini imejidhihirisha wiki hii pale katibu mkuu huyo Kamuhanda alipokataa kwenda kumuwakilisha waziri kwenye mkutano wa wahariri mjini Morogoro.
Awali waziri alikubali kuhudhuria kama alivyoalikwa na MCT lakini baadae akasema atamtuma katibu mkuu wake. Hata hivyo baada ya siku kufika, katibu mkuu huyo alikataa kumuwakilisha waziri huku akiwataka waandaaji wamtafute waliyemwalika na yeye hana muda huo wala mwaliko haukuwa wake.
Hii imerejesha kipindi cha Shamsa Mwangunga na Blandina Nyoni kule Maliasini ama Blandina na Lucy Nkya kule afya. Nitaendelea kuwajulisha na hasa nikipata chanzo halisi cha ugomvi wao.