Ugomvi wa mawaziri na makatibu wakuu warejea; sasa ni Dr Mukangara Vs Seth Kamuhanda...

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Wakuu
Kuna taarifa za kuibuka kwa ugomvi na kutokuelewana baina ya waziri mpya wa habari, utamaduni na micchezo Dr Fenela Mukangara na katibu mkuu wake Seth Kamuhanda. Chanzo halisi cha kutokuwepo kwa maelewano kati yao hakijawekwa bayana. lakini imejidhihirisha wiki hii pale katibu mkuu huyo Kamuhanda alipokataa kwenda kumuwakilisha waziri kwenye mkutano wa wahariri mjini Morogoro.

Awali waziri alikubali kuhudhuria kama alivyoalikwa na MCT lakini baadae akasema atamtuma katibu mkuu wake. Hata hivyo baada ya siku kufika, katibu mkuu huyo alikataa kumuwakilisha waziri huku akiwataka waandaaji wamtafute waliyemwalika na yeye hana muda huo wala mwaliko haukuwa wake.

Hii imerejesha kipindi cha Shamsa Mwangunga na Blandina Nyoni kule Maliasini ama Blandina na Lucy Nkya kule afya. Nitaendelea kuwajulisha na hasa nikipata chanzo halisi cha ugomvi wao.
 
Sawa kabisa, nani alimwambia huyo waziri kwamba katibu mkuu ni errand boy wake? Anatakiwa ajue mipaka yake na kuheshimu wenzie,
 
Vita ni Vita Mura!Waelewe kuwa hali hiyo haina tija ktk utendaji!Hasa huyo Tume ya katiba.
 
CCM OYEE...
Mwanzo wa ngoma ni lele.
Mchelea mwana kulia hulia yeye
Lakuvunda halina ubani
Maji yakisha mwakiga hayazoleki,
Sikio la kufa halisikii dawa.
La kuvunda halina ubani.
CCM IS DYING SLOWLY
Wakuu
Kuna taarifa za kuibuka kwa ugomvi na kutokuelewana baina ya waziri mpya wa habari, utamaduni na micchezo Dr Fenela Mukangara na katibu mkuu wake Seth Kamuhanda. Chanzo halisi cha kutokuwepo kwa maelewano kati yao hakijawekwa bayana. lakini imejidhihirisha wiki hii pale katibu mkuu huyo Kamuhanda alipokataa kwenda kumuwakilisha waziri kwenye mkutano wa wahariri mjini Morogoro.

Awali waziri alikubali kuhudhuria kama alivyoalikwa na MCT lakini baadae akasema atamtuma katibu mkuu wake. Hata hivyo baada ya siku kufika, katibu mkuu huyo alikataa kumuwakilisha waziri huku akiwataka waandaaji wamtafute waliyemwalika na yeye hana muda huo wala mwaliko haukuwa wake.

Hii imerejesha kipindi cha Shamsa Mwangunga na Blandina Nyoni kule Maliasini ama Blandina na Lucy Nkya kule afya. Nitaendelea kuwajulisha na hasa nikipata chanzo halisi cha ugomvi wao.
 
Kwa mbali nawasikia wana Msondo ngoma.

"Nidhamu ya kazi, ni msingi, wa maefanikio mema kazini. Viongozii, na wafanyakazi, lazima wote tuwe na nidhamuuuu.
Migogoroooo, na migonganooo, ya kazini, ni ukosefu wa nidhamu"

Shout if you remember thia.

Siku hizi hata muziki wetu watu hawahimizi vitu kama hivi, tumebakia "Ndama mtoto wa ng'ombeeee"
 
....safi mkuu kwa kuwakumbusha!....chukua like....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom